Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari wakuu leo ni kumbukumbu ya miaka sabini tangu kuangushwa bomu la atomic huko Iroshima Japan na kuuwa watu wengi na kuacha madhara kwa baadhi ya vizazi. R i p waliopoteza maisha
Hiroshima ndio ilikuaje? mwenye historia atupie kwa faida ya wengine!
Kipindi kile ndio na balehe nilikua nasoma Malangali middle school Iringa. Kipindi kile ilikua kupata demu si mchezo hata changudoa ulitakiwa umtongoze kama wiki mbili hadi mwezi ndio uone ndani. Du vita ilikua ishaisha tar 30.04,45 wajerumani waliposarenda lkn wajapani chini ya mfalme wao waliomlinganisha na mungu walisema mpaka kieleweke. Ndio rais Truman aliyeshika USA BAADA YA KIFO cha FDR akamuita rubani mmoja aliyeitwa Paul Eliot Jr akadondoshe hicho kitu cha siri walichoita LITTLE BOY au mvulana mtundu. na kweli jamaa alitokea kwenye cambi ya jeshi inaitwa WHITEMAN akaenda na msaidizi wake kumdondosha little boy mjini Hiroshima. Lilipotua ardhini kuliwaka mwanga mara mia zaidi ya mwanga wa jua, kukawa na kishindo kisichoelezeka ndio moto, kwa muda wa sekunde nusu Mji wa Hiroshima (zaidi ya Kariakoo ) ukawa haupo tena, watu walikua wanaungua kama kuni kuanzia kwenye vidole kuelekea mwilini. Waliokufa pale pale lilipotua ni watu 140,000. yaani kama wakazi wote wa Mbeya na viunga vyake. waliokua mbali kidogo kama Kimara walikua ni nyama tupu hakuna mwenye ngozi. waliopelekwa hospitalini ilikua balaa, watu wa tiba hawakutosha, walioungua walikua wanatoa mafunza na harufu ilikua balaa. baada ya siku tatu Truman akaagiza kitu ingine ikashushwe Nagasaki hili waliliita Fatman , liliua watu 80,000 elfu pale pale yaani zaidi ya wakazi woote wa Singida na viunga vyake. Baada ya hilo mfalme Hirohito akakubali yaishe. Truman aliamini kupiga bomu la atomic kutaokoa maisha ya wengi. kwani vita ingeisha mapema. Ikumbukwe kabla mabomu haya hayajapigwa ndege za Marekani zilidondosha vikaratasi kuwaomba wajapani wa sarende lkn wajapani walisema watu wazima hawatishiwi nyau.
Dah... Wajapan walikuwa na roho ngumu kiasi hiko kwanin? Yaan pamoja na mabomu yote hayo hawakusurrender???
Nakumbuka kipindi kile ndio namaliza tuu, Middle school nikajikuta nachaguliwakwenda vitani...
Ooh!wakati huo mimi niko bulma huko india kama kibarua kwenye mashamba ya mpunga,wajukuu zangu😀
Yah nakumbuka nilikuwa na miaka 20 kipindi hicho
Sema nakusikiliza babu:sly:
Kipindi kile nilikuwa na miaka 17 na nilichaguliwa kwenda kupigana vita ya pili ya dunia!
Babu ulipigana upande gani? Na mambo gani ulijifunza katika vita ile?
Kipindi kile nilikuwa na miaka 17 na nilichaguliwa kwenda kupigana vita ya pili ya dunia!
Mmmh!!!! Ulikuwa na miaka mingapi?????? Labda
Kama nilivoeleza hapo juu, nilikuwa na 17, ila bado niko fit na bibi yenu bado namhudumia😛