Sioni kama unaelewa maana ya tunu ya uvumilivu. Nitakupa somo:
Fikiria kwamba, kuna mtu A anayemaini kuwa kitendo X ni haramu kidini, na hivyo kuamini kuwa kitendo hiki kinapaswa kupingwa.
Lakini, kwa mujibu wa tunu ya uvumilivu, mtu A anatakiwa kuamini kwamba ni sahihi kujizuia kupinga kitendo X, endapo kitafanywa na mtu baki B, kwa sababu kitendi hicho ni miongoni mwa matendo yanayopaswa kuvumiliwa na wanajamii.
Kwa hiyo, uamuzi wa mtu A kuvumilia kitendo cha B unaonekana kumaanisha kwamba, mtu A anakubali imani kwamba “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” ambazo ni imani mbili zinazopingana kimantiki.
Hata hivyo, kama tunu ya uvumilivu ikitafsiriwa vizuri haitaonekana kuwa na mkanganyiko huu wa kimantiki. Kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya tunu ya uvumilivu, kukubalika na kukataliwa kwa kitendo X kunategemea mazingira ya kitendo hicho.
Yaani, uvumilivu wa mtu A kuhusu imani X, katika mazingira M, haumaanishi kwamba mtu A anapaswa kuonyesha uvumilivu kuhusu imani X, katika kila mazingira mbali na mazingira M.
Ndio kusema kwamba, kitendo X sio haramu kila wakati, kila mahali na kwa kila mtendaji. Yaani, wema wa kitendo X, au ubaya wake, unategenea mazingira ambako kitendi hicho kitafanyika.
Kwa hiyo, tafsiri sahihi ya tunu ya uvumilivu iko hivi: fikiria kwamba kuna mtu A anayemaini kuwa kitendo X ni haramu kidini, na hivyo kuamini kuwa kitendo hiki kinapaswa kupingwa katika mazingira M.
Lakini, kwa mujibu wa tunu ya uvumilivu, mtu A anatakiwa kuamini kwamba ni sahihi kujizuia kupinga kitendo X, endapo kitafanywa na mtu baki B, kwa sababu kitendi hicho ni miongoni mwa matendo yanayopaswa kuvumiliwa katika mazingira N.
Kwa hiyo, uamuzi wa mtu A kuvumilia kitendo cha mtu B unamaanisha kwamba, mtu A anakubali imani kwamba “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” katika mazingira M na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” katika mazingira N.
Ukitumia somo hili katika mjadala wa sasa, maana yake ni hii: “X ni kitendo kinachopaswa kupingwa” katika mazingira M na anakubali imani kwamba “X ni kitendo kisichopaswa kupingwa,” katika mazingira N, ambapo:
- X ni kitendo cha kuendesha programu za kisekta katika TV
- M ni mazingira ya TV ta Taifa TBC
- N ni mazingira ya TV ta taasisi ya kidini kama vile Tumaini TV, Iman TV, Upendo TV, nk.
- Ambapo, mazingira M na mazingira N yote yanapatikana katika nchi moja ya Tanzania.
Huu ndio uvumilivu tuliofundishwa tangu shule ya chekechea, na sio vinginevyo.
Katika Taifa moja, lenye mseto wa kidini, lazima kuwepo na sehemu za umma wote ambako programu za kisekta hazikanyagi. Maeneo hayo ni pamoja na:
- Vyombo vya habari vya Taifa (Hapa, lugha ya Taifa ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
- Shule za Taifa (Hapa sare ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
- Vyuo vya Taifa (Hapa mtaala mmoja ni alama na nyenzio ya kujenga Utaifa)
- Vituo vya usafiri wa umma (Hapa vituo vya mabasi ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
- Maktaba za Taifa Hapa vitabu mmoja ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
- Barabara za Taifa (Hapa barabara ni mfano wa uwepo wa maslahi ya pamoja Kitaifa)
- Nk
Katika maeneo haya ni marufu kuendesha mihadhara ya kidini.
Nadhani somo limeeleweka.