Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Hoja inayojadiliwa hapa inahusu uvunjaji wa Katiba ibara ya 4(1) na 19(2).
Hayo unayoyaibua ni hoja tofauti.
Anzisha bandiko jingine kwa ajili yake.
 

1. Kule Bungeni huwa wanafanya sala kila waanzapo session, wanamtaja "Mungu" bila kutwambia Mungu yupi, anayesoma dua sio padre, sio shehe, sio mchungaji. Wakati huo huo Katiba ya nchi haina neno Mungu. Ibara ya 4(1) na 19(2) zinataka Bunge kutenganisha shughuli zake na shughuli za kidini. Bado huoni tatizo hapo? Kuna mapokeo yanayovunja Katiba na yanaendelezwa kiajabu tu.

2. Kwenye matukio makubwa ya kitaifa kama sherehe za maadhimisho mbalimbali huwa wanaalikwa viongozi wa dini zote kufanya sala. Kumtaja Mungu katika sehemu kama hizo bila kueleza ni Mungu yupi anatajwa ni ukasuku. Ni Mungu anayekula kitimoto au Mungu asiyekula kitimoto? Mungu mwenye nafsi tatu au MUngu mwenye nafsi moja? Mungu mwenye mwili au Mungu ambaye ni roho tupu? Mungu anayetumia kondomu au Mungu asiyetumia kondomu? Msawali haya machache yanakuonyesha ukubwa wa ukasuku wetu.

3. Kumtaja Mungu katika sehemu za umma ambako kuna watu wanashilia mtazamo tofauto kuhusu hulka ya MUngu, na bila kueleza ni Mungu yupi anatajwa ni uchokozi wa kidini. Kwa mfano najiuliza:

-- Ni Mungu anayekula kitimoto (Mungu Mkristo) au Mungu asiyekula kitimoto (Mungu Muislamu)?

-- Mungu mwenye nafsi tatu (Mungu Mkristo) au MUngu mwenye nafsi moja (Mungu Muislamu)?

--Mungu mwenye mwili (Mungu Mkristo) au Mungu ambaye ni roho tupu (Mungu Muislamu)?

-- Mungu anayetumia kondomu (Mungu Mlutheri) au Mungu asiyetumia kondomu (Mungu Mkatoliki)? Msawali haya machache yanakuonyesha ukubwa wa ukasuku wetu.

4. Kutokana na matatu hapo juu, ni wazi kuwa dua za Bungeni na sala za kufungua matukio ya kiserikali ni uchokozi wa kidini na zinamaanisha uvunjaji wa Ktiba ya nchi ibara ya 4(1) kama ikisomwa pamoja na ibara ya 19(2).
 
Salamu Mpya ya Rais Samia ndio Mwarobaini wa tatizo la salamu za kidini kwenye matukio ya kiserikali.

Vipindi vya "inueni mioyo" na "Quran tukufu" kupitia TBC na RTD vimekuwapo muda mrefu, na vimeongezeka siku hizi.

Kwa hiyo hoja yangu inazo sababu za muda mrefu na sababu za karibuni.

Sasa nasema: Kwa kuwa Vipindi hivi vinavunja ibara ya 4(1) na 19(2) za Katiba ya Tanzania, basi ni batili.

Nataka tujisahihishe.
 
Kuna madaktari wanafanya kazi kwenye hospitali za mashirika ya dini je nao waondolewe?
Kazi ya udaktari sio tendo la kidini. Hivyo, madaktari wa serikali walioko katika hospitali zinazomilikiwa na madhehebu ya dini hawavunji ibara ya 4(1( na 19(2) ya Katiba ya nchi.

Kazi ya uhasibu sio tendo la kidini.Hivyo, mapadre/masista wanaofanya kazi serikalini, kama ilivyo pale ofisi ya RC Dar, hawavunji ibara ya 4(1( na 19(2) ya Katiba ya nchi.
 
Sasa kama TV za kisekta hazifiki ndio tutumie kodi ya umma kueneza dini katika maeneo hayo? Hapana!
Kumbuka wanaotazama hizo TV programs ni walewale wanaokwenda makanisani na misikitini, pia hivyo vipindi vinaonyeshwa siku za ibada zao tu na siyo siku zingine
 
Ayubu Rioba ni takataka..amfate mwendazake chato akawe anafagia kaburi
 
Hizo ibara zinasemaje Mama Amon
 
Kumbuka wanaotazama hizo TV programs ni walewale wanaokwenda makanisani na misikitini, pia hivyo vipindi vinaonyeshwa siku za ibada zao tu na siyo siku zingine
Naona unajali sana matokeo bila kuzingatia mbinu inayotumika kufikia matokeo hayo.
Mwanafunzi akitazamia na kushinda mtihani sawa, hata kama ni Mr. Zero!
Hapana.
Hoja yangu inaanzia kwenye uvunjaji wa Katiba ibara ya 4(1) na 19(2).
Jielekeze kwenye hoja.
 
Inaonekana we punda hujasoma hata ameandika nini.. unawaza ujinga tu muda wote. Ndo maana amesema ni vyema kila dini utumie vyombo vyake vya habari.
 
Mwanasheria anapokosa wateja mda mrefu
 
Kimingi hakuna swali

Mimi hi mkristu, na nimestruggle Sana kuona swali liko wapi

Huwezi kuandika maelezo page tatu justifying what you want people to believe and expect it to be a question

You bias took you far down the road exposing your hatred and intolerance over other religions
 
Haya maswali yako hayana mantiki
 
Katika hoja ya imani si kweli wakristu na waislamu ndio makundi makubwa katika jamii ya watanzania. Wasio na imani hizo ndio kundi kubwa, japo hawapewi nafasi kwa sababu wenye uwezo wa kutoa nafasi wapo kati ya makundi hayo mawili. Ni dhuluma kutumia hela ya walipa kodi wasioa amini kuendesha mambo yasiyo wahusu.
 
Wahindu wanaokwenda kwenye mahekalu kumuabudu Krishna kipindi chao kipo lini?
Kumbuka wanaotazama hizo TV programs ni walewale wanaokwenda makanisani na misikitini, pia hivyo vipindi vinaonyeshwa siku za ibada zao tu na siyo siku zingine
 
Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.
Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana.
Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana.
Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.
Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki.
Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha.
Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.
Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi.
Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.
Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi.
Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote.
Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.
 
..Mbona huku hoji haya hapo kabla..kwanini baada ya tangazo la mashindano ya kusoma qur'an tukufu? kwanini leo?
Actually hii post awali kabisa haikuwa detailed namna hii, nadhani imekuja kuwekwa nyama baadaye baada ya mjadala kuwa mzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…