Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Hao wenye dini ndio walipa kodi,mbona huhoji barabara,madaraja,mahospitali,mashule,wanatumia hao hao wenye dini?Mlipa kodi ndio mnufaika na kodi,tumia akili.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Nihoji vipi wakati hayo ni mawazo yako, mwambie mleta mada, nimemjibu mpayukaji wa capital letters.
 
Ni kitu cha kushangaza sana,mtu kuhoji watu wa dini, kutumia kitu ambacho kimepatikana na kodi za hao wenye dini, utahoji barabara, kwa nini zitumike na wenye dini, mahospitali, shule, madaraja, viwanja vya ndege, stend za bus, viwanja vya michezo, taa za barabarani, mwisho utahoji kupata vyeo. Mwisho unahoji mavazi, wakati wa dini zote, wamepewa nafasi kuvyaa mavazi ya shule, yanaondena na imani zao, kwa mfano wanafunzi wasiokuwa waislamu, wanaovyaa sketi fupi, blouzi na kichwa wazi wa kike, ndio mavazi yao mpaka kwenye nyumba zao za ibada.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Sikuwahi kulifuatilia hili, ila nadhani wanachofanya ni kutaka kubalance, yani siku ya ijumaa airtime kubwa inakuwa ni kwa dhehebu la kiislamu na siku ya jumapili airtine kubwa ni kwa wakristo.Kwahiyo kama wanapendelea upande mmoja zaidi hapo watakuwa wanakosea...
 
...na ukashangaa..maana ulifikiri hao waislam hawana haki ya kutumia hiyo stesheni ya Luninga..ila wakristo tu siku ya Jumapili? Nafikiri ungeyaacha kama yalivyo!

Soma vizuri. Bandiko linahoji utaratibu mzima wa TBC kutumiwa kidini bila kujali dini gani inatumia chombo hicho
 

Nimehoji utaratibu mzima wa Ijumaa na Jumapili maana naona mambo yanakiuka dhima ya TBC ya kujenga umoja wa kitaifa kwa kutumia lugha ya Taifa na kuendesha programu za kitaifa.

Kwa vile dini tayari zina redio na TV zake nadhani umefika wakati TBC kuachana na mambo haya yanayokiuka kanuni za social justice
 

Hoja hapa ni fupi: ni kwa vipi taasisi za umma kama vile RTD, shule na TBC zinaweza kuwa nyenzo ya kujenga utaifa. Utaratibu wa sasa una dosari. Just my fair opinion
 
Hoja hapa ni fupi: ni kwa vipi taasisi za umma kama vile RTD, shule na TBC zinaweza kuwa nyenzo ya kujenga utaifa. Utaratibu wa sasa una dosari. Just my fair opinion
Kujenga utaifa ndio huko, watu wa dini kutumia miundombinu na vyombo vya umma, kwa vile wao hao watu wa dini, ndio walipa kodi wenyewe. Huwezi kutengenesha, watu(ambao wana dini), na kunufaika na miundombinu na Taasisi zinazotokana na kodi zao. Hivi ulitaka watumie wasio na dini?Wakati hata wasio na dini, wana vipindi vyao, kwa mfano ngoma, taarab, mziki, vipindi vya maigizo, ambavyo yapo madhehebu ya dini mengine, hawakubaliani na hayo, lakini wapo kimya.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 

TV ya taifa inaendeshwa kwa mtindo wa push technology, sio kwa mtindo wa pull technology, ambako mtazamaji huchagua programu gani aangalie

Kwa hiyo, yafaa ionyesha programu za kitaifa pekee, kwa kutumia lugha ya Taifa pekee.

Taasisi za dini zina TV na REDIO zake.

Wajihudumie bila kuhujumu umoja wa kitaifa kupitia mgongo wa kodi ya umma wote
 
Kujenga utaifa ndio huko,watu wa dini kutumia miundombinu na vyombo vya umma,kwa vile wao hao watu wa dini,ndio walipa kodi wenyewe.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app

Hapana, kosa linalofanyika TBC ndio linafanyika kwa msajili wa vyama vya siasa. Kodi ya watanzania wasio na vyama inatumika kulipa ruzuku kwa vyama.

Vivyo hivyo, kodi ya mtu asiye na dini inatumika kuendesha TBC kwa faida ya muumini wa dini Y, etc

Haya mambo sio sawa hata kidogo
 
Ukimsoma vizuri jamaa hana shida na wakristo kutumia TBC, yeye shida yake ni Waislam. Hii ni kwasababu Jpili na siku nyingine amesikia Wakristo wakiendesha Ibada hakushtuka, ila leo ameshituka baada ya kuona swala na ibada za Waislam, ikamtuma

Soma tena hapa ili ujielekeze kwenye hoja ya mwandishi bila kufanya spinning:

 

Hujaelewa hoja, soma tena, kisha ujielekeze ktk hoja
 
...na ukashangaa..maana ulifikiri hao waislam hawana haki ya kutumia hiyo stesheni ya Luninga..ila wakristo tu siku ya Jumapili? Nafikiri ungeyaacha kama yalivyo!

Hujasoma wala kuelewa hoja. Siongelei uislamu. Tuliza kichwa chako, vaa miwani kama macho yana tatizo
 

Mimi sina dini, kwa hiyo sitaki kodi ninayolipa itumike kuendesha shughuli za kidini kama wanavyofanya TBC. Hapo sibanduki.
 
Mods threads kama hizi hazina tija sana sana zitakaribisha malumbano yasiyo na afya kwa jamii. Tafadhalini futeni hii takataka

Maneno haya hayana uhalisi: Threads hizi hazina tija, malumbano hata hayana afya, etc.

Mjadala unaohusu ulinzi wa katiba ya nchi sio jambo la kubeza.

Twende kwa mtindo wa point counter point. Tutafika.

Wenye jaziba watashangaa wakijibiwa kwa hoja na upole.

Hili sio jambo la kufunikwa funikwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…