Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Taasisi za serikali kutumika kama majukwaa ya dini ni matumizi mabaya sana ya pesa za walipakodi. Wote tupinge huu utaratibu.
Ukileta hoja ya kulipa kodi basi huwezi kuwatoa hao watu wa dini maana nao wanakatwa kodi, ndio maana nauliza hao walipa kodi ni akina nani hao?
 
Taasisi, idara, mifumo au vyombo vyovyote vya serikali visitumike kama platform ya dini yoyote.
Dada mi ni mkristo lkn niseme ukweli kwamba kimtazamo wang naona kama hoja yako haijakaa kitaifa bali imekaa kidini. Na ndo maana hoja hii imekosa wachangiaji wengi, hii ni kwa sababu watu wengi humu wameshachoka na hoja zenye kuleta malumbano ya kidini baina yetu kama Taifa. Wengi humu tumeoleana na kuzaliana ktk imani tofauti. Unakuta baba muislam mama mkristo, au baba mkristo mama muisilam, watoto wanaozaliwa wanapokuwa wakubwa wanaamua wenyewe imani ya kufuata nk, hapo sijaongelea mtaani, mashuleni, maofisini na sehem mbali mbali za miji na nchi kwa ujumla. Umekiri mwenyewe kwamba unafahamu kitambo kuhusu vipindi vya dini vinavyorushwa kila siku asubuh na usiku wakati wa kulala, yan muda wa kufungua vipindi na muda wa kufunga vipindi, pia umekiri kuwa kuna vipindi vya kikristo huwa vinapitishwa kila jumapili kwa ajili yetu sisi wakristo lkn haukuwahi kuja kuhoji chochote kuhusu vipindi hivyo vya jumapili, lkn leo umeona na ndugu zetu na wao wameanza kupewa muda wa kuangalia au kufuatilia vipindi vyao TBC siku ya ijumaa umekuja haraka haraka kuzungumzia habari za kodi, ila wakati walipokuwa wanarusha vya kwetu kila ijumapili bila kupitisha hiki cha ijumaa swala la kodi haukulihoji. Tupendane jamani sisi wote ni taifa moja hao waliotuletea hizi imani kwa sasa wapo mbali baada ya kupuuza mawazo ya aina hii.
 
Siku zote nitapinga kuingiza mambo ya dini yoyote katika mifumo, taasisi na shughuli za serikali.
Kwahiyo hata haya mapumziko ya kazi kwa sikukuu za dini kama Eid na Krismas nazo pia zisiwepo?
 
Tumeshatoka enzi za RTD. Taasisi za serikali zisitumike kama jukwaa la dini yoyote. Mambo ya dini yaishie kwenye nyumba za dini na maisha binafsi ya wenye dini zao.
Uzi wa kijinga. Waislam wamekuwa wakifundisha dini yao kabla ya TBC miaka ile ya RTD na hakuna aliyeona ni jambo lisilo la kawaida.

Enzi za marehemu Sheikh Hemed bin Juma bin Hemed miaka ya 1970-80.
 
Na vile vipindi vinavyoonesha tamaduni za makabila yetu navyo Tv yao ni ipi?
Zingatia haya:

1. Taifa-mtu mmoja mmoja + ndoa + familia + ukoo + kabila

2. Lugha ya Taifa inatokana na lugha za kikabila.

3. Kwa hiyo, vipindi vya kikabila vinavyotumia lugha ya Taifa ruksa ktk TBC

Kumbuka:

4. Hata usajili wa Radio za FM zinazosikilizwa huko mikoani una kifungu kinakataza matumizi ya lugha za kibalia. Yaani, ni lazima zitumie lugha ya Taifa ktk programu zake.
 
TV inayolipiwa kodi na watu wa dini zote, waganga na wasio na dini haitakiwi kutumika kama jukwaa la baadhi ya imani mbili au tatu tu. Na ili kuondoa huo mkanganyiko vipindi vya dini visirushwe katika TV au redio za taifa pamoja na magazeti.
Hizo dini zina vyombo vyake binafsi, ingeleta mantikia kama vingekuwa vipiandi vya dini zisizo na vyombo vya habari kabisa
Wakati kabla Rais hajahutubia kwenye shughuli za kitaifa wanasimama viongozi wa dini na kuliombea taifa na miongoni kwao yupo yule anaswali kihindu..bongo wahindu ni wachache lakini yule yupo siku zote.

Taifa letu halina dini ila mimi na wewe tuna dini zetu.

Kama huwezi kuvumilia kusikiliza masuala ya dini nyingine basi badilisha channel ili wenye kuelewa waendelee na ibada inayowahusu.

Hawezi kufurahishwa kila mtu tena kila wakati.
 
China wanaapa kwa Katiba tu na hakuna mambo yoyote ya kidini yanahusishwa katika viapo au kuendesha serikali.
Waliamua kuwepo utamaduni wa kuapq ukiwa umeshika kitabu cha dini sio wajinga.

Walioamua Mungu ahusishwe katika kiapo cha kisiasa walijua wanafanya nyinyi.

Huwezi kumkwepa Mungu ukafanikiwa.
 
Walipa kodi ni Wahindu, Mabohora,Wabudha, Wakristo, Waisalamu, Waganga, Wachawi, wasio na dini n.k
Ukileta hoja ya kulipa kodi basi huwezi kuwatoa hao watu wa dini maana nao wanakatwa kodi, ndio maana nauliza hao walipa kodi ni akina nani hao?
 
We na ukoo wako mtakua masikini wakutupwa huko Usukumani, yaani we leo ndio umeona TBC inatumika kidini baada ya kuona waislam? Vp jumapili zote huwa huoni ya mapambio? Kweli mmeshikwa make..nde na mmekosa la maana lakujadili, nyie makafiri mna shida sana, wakwenu akiongoza nchi hua mnakuaga vipofu, kwa Taarifa yako mjijue mna matatizo maana kila awamu yenu ndio Taifa huteseka maana neno Haki kwenu hamnaga kabisa
 
Acha kubisha na makondoo mkuu hayana akili
Hoja yako ni nini?
Maandishi ya Madrasa kupita kwenye utepe wa screen umeathiri nini kwenye ulichokuwa unakitazama?
Uvaaji wa hijaab mashuleni unakuathiri vipi, unatambua kuwa kuna Masister wa kikatoliki wanavaa vilemba mashuleni na vyuoni?
 
Kuabudu ni uhuru wa mtu kama hutaki kuangalia wengine wakiabudu kupitia TBC wewe zima TV yako au badili channel.

Huo uwezo wetu wa kuvumilia na kuchukuliana kama tulivyo ndio umetuwezesha kufikisha miaka 60 ya uhuru msidhani ni jambo jepesi tu kama kwenda chooni asubuhi baada ya kuamka.

Nchi yetu haina dini ila kila mtu anayo dini yake na anao wajibu wa kuheshimu dini ya mwenzake.
Umesema kweli tupu
 
Umekwenda nje ya hoja iliyo mezani. Tunajadili hoja hii:

1. Matakwa ya kikatiba ya kutenganisha dini na dola yanaweza kutekelezwa kwa njia kuu mbili: American style or Germany style.

2. German style inabagua baadhi ya dini na kulazimisha baadhi ya walipa kodi kubeba mzigo usiowahusu; wakati American style haina mapungufu hayo.

3. Kwa hiyo, twende na American style?

Kwa hiyo, utaona kuwa hayo mambo ya dansi,mziki,ngoma,makala za biashara,kilimo,ujasiriamali, sio sehemu ya hoja hii.

Kama nasahihisha karatasi ya majibu ya mtihani wa mwanafunzi ningekwambia: Jibu swali uliloulizwa.
Sisi ni nchi huru,kwa nini tufuate wanayofanya Germany au Amerika.Wao mbona hawafuati yetu.
 
Hoja inayohusu lugha za kiarabu na kilatini kutumika kwenye TV ya Taifa sio tatizo dogo kwa sababu kuu tatu.

1. Jambo hilo linakula nafasi ya lugha ya Taifa ambayo ni nyenzo muhimu ya kujenga utaifa.

2. TBC wanao wajibu wa kukuza umoja wa Taifa kwa kutumia lugha ya Taifa, na ndio maana wametofautisga kati ya TBC1, TBC2, etc.

3. Ukoloni wa lugha ni tatizo lisilovumulika.
Huo unaoita ni ukoloni wa lugha,ndio watalii wanakuja kwa kutuingizia pesa za kigeni,nenda Kilwa,ukaone hela za zamani zimeandika kwa kiarabu,na majengo yenye mijengo ya kiarabu na nenda bagamoyo ukaone,na hizo sehemu zimetengwa kuwa urithi wa dunia.Bado hapo sijakutajia Zanzibar,ambapo pia watalii wanakuja kuangalia hayo maandishi ya kiarabu kwenye milango ya nyumba za kale,na kulipia pesa za kigeni.
 
Kwahiyo hata haya mapumziko ya kazi kwa sikukuu za dini kama Eid na Krismas nazo pia zisiwepo?
Nashauri yawepo, kama watakuwepo na wengine wataoona hawajatendewa haki kwao kutokuwa na sikukuu yao nao wanatakiwa ku-propose siku wanayotaka kuwa yao ya mapumziko wapeleke mapendekezo yao serikalini.
 
Mbona wengine hawana vyama lkn kodi zinatumika kutoa ruzuku kwa vyama? Uliwahi kuhoji? Ni majuzi tu kuna Askofu alisimikwa na tukio lilikua mubashara TBC nako hukuona? Yaani wewe ni mbulula moja ya kisukumaa inahangaika tu na utakufa kwa hii roho ya kichawi, mtangoja karne nyingi sana na nnashangaa mods wanatumbua mimacho kwenye nyuzi za kishetani kama hizi
 
Naona unachanganya mambo. Hebu nirekebishe hivi:

1. Chombo chao cha habaro: KIna nani? Katoliki wana Tumaini TV, KKKT wana Upendo TV, Waislamu wa Iman TV, Watanzania wote wana TBC. Kwa hiyo, masuala ya kisekta yanapaswa kuonyeshwa kwenye TV za kisekta, na masuala ya kitaifa kwenye TV ya kitaifa. Hiyo ndiyo maana ya civic space.

2. Utoaji wa huduma za jamii kama vile afya na elimu kupitia ushirika wa serikali na mashirika ya dini: Dini zinasajiliwa MOHA, shule zinasajiliwa Wizara ya Elimu, AZAKI zinasajiliwa Wizara ya Ustawi wa Jamii. Kwa hiyo, huduma za jamii kama vile afya na elimu sio kazi ya msingi ya taasisi za dini. Zinaweza kufutiwa leseni za shule na hospitali na kubakiza leseni ya MOHA.
Utajipa tabu sana,katika lugha ya kiswahili karibia 30%ni maneno ya kiarabu,hii lugha kuikwepa sio rahisi,hata namba 0123456789,tumefundishwa mashuleni ni namba za kiarabu.Itabidi hata kiswahili na namba tuache kutumia.
 
Mtoa mada wewe ndio mtu hatari zaidi kwa umoja wa kitaifa.Unadhani watu wenye mamlaka hawakufikiria hadi kuruhusu vipindi vya dini kwenye vyombo vya habari vya uma.Kama Kuna kundi unaona halijatendewa haki paza sauti wapewe haki yao.Sio hiko unachokifanya.Hii ni fitna unayoijenga.
 
Siku zote nitapinga kuingiza mambo ya dini yoyote katika mifumo, taasisi na shughuli za serikali.
Dini huwezi kuikwepwa,madhali watu wana dini,hata hao watangazaji,mavazi yao,yanaendana na imani wanazozifuata,mwisho utakuja sema,wasivyae nguo kabisa.
 
Sio sahihi kuchukuwa pesa za walipa kodi kuvipa vyama
Mbona wengine hawana vyama lkn kodi zinatumika kutoa ruzuku kwa vyama? Uliwahi kuhoji? Ni majuzi tu kuna Askofu alisimikwa na tukio lilikua mubashara TBC nako hukuona? Yaani wewe ni mbulula moja ya kisukumaa inahangaika tu na utakufa kwa hii roho ya kichawi, mtangoja karne nyingi sana na nnashangaa mods wanatumbua mimacho kwenye nyuzi za kishetani kama hizi
 
Back
Top Bottom