Naona hujaelewa wazo langu. Basi twende kwa mtindo wa point counter point namna hii:
1. Nilichokisema mimi ni kwamba dini/imani ni sehemu ya utamaduni wa watu/walipakodi.
Jibu: neno dini lina maana nyingi: Kuna dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Kitaifa, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa kikabila, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Wakristo, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Waislamu, dini ambayo ni sehemu ya utamadni waWahindu, dini ambayo ni sehemu ya utamadni wa Wabuda, nk. Unaongelea dini gani na utamaduni gani?
2. Kama kipindi kinachorushwa kinahusu dini/imani (sehemu ya utamaduni wa watu), kama kinavyoweza (kurushwa kikiwa na maudhui) kuhusu uchumi, siasa na jamii, kwa kuzingatia taaluma ya uhandishi wa habari kwa namna ambayo haivunji maadili au sheria za nchi,
Jibu: Dokezo kuu la hoja inayojadiliwa hapa linaanzia kwenye ibara ya 4(1) na 19(2) za Katiba ya Tanzania (1977). Ibara hizi haziongelei uchumi, siasa wala jamii. Zinaongelea kutenganisha shughuliza serikali na shuguli za dini. Hiyo ndiyo fokasi ya hoja.
3. Na kwa vile baadhi ya walipakodi ni waumini pia katika hiyo dini/imani,
JIbu: TBC inatumia kodi ya walipa kodi wote, wakiwemo watu wasio na dini. Haitumii kodi ya baadhi ya walipa kodi.
4(i) Basi, hakiwezi kukiuka utaratibu wa kawaida wa kurusha vipindi vya TV au radio na
Jibu: Hitimisho hilo halitokani na madokezo sahihi, kama nilivyoonyesha hapo juu, na kwa hiyo halina uhalali.
4(ii) hivyo (kwa maoni yangu) hakuna utata wowote katika hili.
Jibu: Hitimisho hilo halitokani na madokezo sahihi, kama nilivyoonyesha hapo juu, na kwa hiyo halina uhalali. Utata upo kama nilivyoonyesha hapo juu.
5. Labada wewe mwenyewe uonyeshe urushaji wa hivyo vipindi vinavyosemwa ulikuwa na utata gani au ulikiuka utaratibu gani wa urushaji wa vipindi.
Jibu: Bandiko langu limeonyesha vema utata. Linao muundo ufuatao: matarajio, uhalisia, ufa kati ya matarajio na uhalisia, mapendekezo ya kuziba ufa, na majibu ya pingamizi tarajiwa. Soma kwa kutulia
6. Kama urushaji wa hivyo vipindi una tatizo, basi tujadili hilo tatizo kuliko kujadili jambo la jumla hivyo.
Jibu: Tatizo ni urushaji wa vipindi vya kidini kupitia TBC kuvunja kanuni ya 4(1) na 19(2) ya Katiba ya Tanzania (1977), na bandiko langu limeonyesha vizuri tatizo hili.