Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Kuna maombi naweza kuacha, lakini si maombi toka kwako. Kwenye hili labda niseme kama template na kila mtu aitumie kulingana na mazingira yake ili afanikishe.Mdakuzi Tujaalie maoni yako tafadhali.
Kwanza, ni lazima awe na sababu (sio moja) zenye faida za moja kwa moja kwake na kwa mke mkubwa. Kwa maana ya kuleta ahueni kwa wote wawili.
Katika sababu ni muhinu kuepuka sababu za kimapenzi au za tatizo la mpito. Pia, zisiwe sababu za kumfanya bora zaidi mke mdogo mtarajiwa, au mwokozi.
Pili, lazima kwenye maelezo aoneshe kuheshimu nafasi ya mke mkubwa na kumfanya ni mwamuzi wa mwisho, na bila maamuzi yake haliwezi kwenda. Yaani asionekani ana maamuzi tayari.
Tatu, kuhakikisha ana uwezo bila shaka wa kumhudumia mke mdogo mtarajiwa bila ya kumega kwa mke mkubwa, au kumpunja (uchumi na mapenzi).
Pia, kuepuka kuwa mwovu kwake, kwa siku za karibuni, hasa za utukutu wa 'kuchepuka'.
Ova