Dar ya mwaka gani unauongelea? Dar ya leo siyo dar inayotamaniwa na watu mikoani hii ujue, dar iliyokuwa inatamaniwa na watu ni dar ya 1961 mpaka 2000, baada ya hapo hakuna jipya lilopo dar mkoani ukalikosa pengine bahari ya Hindi ila vyote mikoani vipo
Dar iliyotamaniwa ni ile mtu wa mkoani anasikia ukiwa dar radio unasikiliza Masaa 24, mtu wa mkoani anashangaa
Ukiwa dar wanawake wanajiuza uwanja wa fisi, Ohio, kinondoni makaburini mtu wa mkoani anashangaa
Ukiwa dar unapanda dala dala mtu wa mkoani anashangaa
Ukiwa dar kuna mikate mikubwa kweli mtu wa mkoani anashangaa
Ukiwa dar week end unaenda Beach mtu wa mkoani anashangaa na anapata hamu akaione dar na zone hivyo vitu
Dar ile mtu wa mkoani akisema naenda dar anaaga mtaa mzima, na siku akirudi mkoani washikaji wanajaa kijiweni kusikiliza story za dar, na anarudi kapendeza maana mitumba mikoani ilikuwa tatizo kwaiyo akirudi mkoani kavaa hata ronya ronya za manzese anaonekana kapendeza maana mkoni kupata nguo nzuri ilikuwa kazi na kama jamaa mjanja atarudi na kanda za radio karekodi miziki radio Tanzania haaa haaa basi anajiona mjanja
Dar ambayo TV na deki ndio zinauzwa mkoani ukuti duka la deki au TV mtu anatoka mkoani anakuja dar kwa lengo la kununua TV na deki 😀😀😀 hii nchi imetoka mbali basi tu
Dar ambao mikoa ya mbali watu wanatumia siku mbili mpaka tatu kufika kutokana na miundombinu ya Barbara
Dar ambayo haifiki uku mbezi mwisho ukifika kimara wewe upo porini ndio dar watu walitamani
Siyo dar ya leo mtu unaishi goba, mandale uko 😁😁😁 hii siyo dar inayotamaniwa maana ishakuwa vurugu mechi
leo hii hayo niliyoyasema mikoani yapo, dar ya leo vurugu mechi tupu manzese darajani si kivutio tena madaraja hayo kila kona dar yapo, mikoani yapo
So dar ipi unaisemea wewe?