Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

Yote tisa kumi sasa boarding sasa watoto wa Dar walikua wanajiona wametoka sijui Beverly Hills dadeq kulikua na kundi la watoto wa Tabata basi maskini sisi wa mkoa tunajua Tabata is the place to be... afu mi nlijuaga tanki bovu kuna booooonge la mtenki umekaa pale una mikutu sijui [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Lilikuwepo tanki lilikuwa bovu ndio chanzo Cha Hilo jinaujenz was barabara wakaja kuliondoa
Sikumbuki lilikuwa tanki Kwa ajili ya nn , ila lilikuwepoo
 
Nakumbuka nikiwa mdogo tulienda kijijni wakati huo Nyerere bado Rais
Basi watu wanajua Kwa vile tunaishi Dar kila siku tunapishana na Nyerere
Ukiwaambia hatumuoni wanashangaa hawaamini unaishi vp Dar halafu humuoni rais?
 
Ushamba mzigo ndugu yangu
Nikiwa moshi tunazungumza na baba mkubwa habari za Manzese darajani, kuna dogo akadandia “pale Manzese kuna mamba wengi sana”. Kichwani nikafikiri anamaanisha labda Ruvu au Wami. Kwa watu ambao tumekulia Dar huwa tunaiona ya kawaida sana ila kwa watu waliozaliwa nje kabla hawajaja Dar wanapaona kama vile ni sehemu ya juu sana

Ngoja niwape kisa kimoja:

Kuna dogo nilienda kwao kumuomba ila aje kukaa dukani Dar, nikiwa kule nyumbani nazungumza watu wa kule nyumbani walikuwa wanashangaa sana, labda jinsi nilivyokuwa kama mzungu. Ila kuna neno nililisikia kuwa “Kiswahili chake sio cha huku kabisa”.

Nikawa napanda kichwa sana huku Dar watu wananichukulia simple ila nimefika sehemu na mie naonekana mtu

Wazazi wakakubali nije na dogo kumleta dukani. Tukiwa kwenye bus kufika mombo tukapata msosi nikamnunulia chips na kuku, dogo kashangaa akasema kwa kirombo “kumbe chips ni mrungu?” akimaanisha “kumbe chips ni viazi?” Dogo katika maisha yake alikuwa anasikia kuna kitu kinaitwa chips ila hakuwa anajua kuwa zinatengenezwa na viazi.

Tukiwa Mombo akamuona mwanamke wa kizungu anavuta sigara dogo hakuamini kabisa kama mwanamke anaweza vuta sigara yani tulipotinga Dar tu nikampa simu azungumze na ndugu zake wote aliozungumza nao kwenye simu kama wamesikia taarifa ya kushangaza sana.

Tulifika Dar, dogo akawa anashangaa kila kitu mpaka anaacha mdomo wazi. Basi nikamtafutia nguo safi nikamweka dukani, kipindi cha mwanzo nilikuwa nasikia furaha sana kwani ukimwachia elfu tatu ya kula mchana unaikuta kama ilivyo. Nikawa namsifia kwa marafiki zangu, “huyu dogo ana uchungu sana na mali hata kama sio yake. Hata chakula cha mchana hali, hii hela ngoja nimwekee nije nimfungulie na yeye duka”. Siku nimerudi nikalala dukani nikawa namuota dada mmoja aliyenicheki PM humu JF (hawanitafutagi sijui PM yangu haina vigezo gani), ila nastuka kutoka ndotoni naona chini kuna mifuko minne ya mikate haina kitu ndani.

Nikajiuliza maswali nani kala hii mikate nikawaza usikute dogo ndio anakula hii mikate ngoja nicheki kwenye mfuko wa matakataka, aisee nikakuta kuna mifuko kama hamsini hivi ya mikate yote imeshaliwa. Nikamwita dogo ajieleze nani anaweka hiyo mifuko akadai kuwa yeye ndio anakula. Nikamuliza kwa mchana huwa anakula mikate mingapi? Dogo akajibu huwa “Anagonga mikate minne na soda moja ya CoCa” Aisee nikampigia simu rafiki yangu nikamwambia aisee dogo noma anagonga mikate minne na soda ya CoCa moja hiyo lunch tu. Dogo kamaliza mtaji wangu wa mkate, jambo la kushukuru sio mpenzi wa bluebanda, maana angenimalizia na mtaji wangu wa blueband.

Swali la kizushi, kwa mara ya kwanza kusikia Dar es Salaam mlikuwa mnachukuliaje? Au wakitoka watu Dar kuja vijijini mlikuwa mnawaonaje? Inawezekana kuna watu walidhani Dar bomba zinatoa maziwa.
Mm nilidhani inakofia kichwani afu ipo kama i i i au ipo kama yai O O O
 
Back
Top Bottom