Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

Kabla sijaja Dar miaka ya nyuma nilikuwa nikiambiwa Dar wanawake wote wanajiuza na ni Malaya, siku natoka kijijini babu alinionya sana kwamba Dar wanawake wote wana ukimwi. Dah jamaa mmoja aliyekuja kijijini akaniambia yaani wewe ukitaka mwanamke unamuita tu unamwambia ukamtie anakubali hakuna anaekataa! Doh nilimvamia Dada moja mitaa ya Sinza miaka hiyo ya nyuma sana nikamwambia we Dada twende nikakut.o.m.b.e kilichonikuta nakijua mwenyewe!

Sent using kidole gumba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu Umenichekesh sana, uwe na siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kiukweli sijakulia bushi ila nmekulia Moshi mjini sema nmesoma boarding sana. Mimi Dar nlijuaga kwanza hamna washamba yan kila mtu mtoto wa mjini yani nikiambiwa tuna safari ya Dar naingia kiboriloni nikafanye shopping kwanza nisionekane wa kuja🤣🤣🤣🤣🤣 dah maisha haya....
 
Sema na nyinyi Wachagga mmezidi ushamba, Wasukuma wamewazidi kidogo tu, na ndo maana mkija mjini na mkishaweza kutumia smartphone basi inakuwa taabu tupu... wasomi nyinyi, wenye pesa nyinyi, wenye magari nyinyi... aaaaaaargh; kumbe ni inferiority complex!!

Ukifuatilia hii simulizi yako unakuta kumbe ni matukio ya juzi tu lakini kumbe mkikutana huko Rombo na Kishumundu, huwa mnasimuliana habari za Daraja la Manzese 😅😂😀😂!!!

Ukiwa na hela hata ukizungumza pumba unaonekana una akili mnoooo wakati mwenye PHD anaonekana fala ila mchaga hata akiwa wa kishumundu anaweza kukuingiza mjini na ujanja wako, matapeli sana hao wa kishumundu

Ungekuwa mkazi wa manzese ungeelewa, lile daraja la manzese ukifika jioni au sikukuuu unaona watu wengi wanaoshea sura pale darajani. Watu wengine wanaenda kupata upepo wengine wanapiga picha pale, wengine wanaenda kukaa pale. Watu wanapaona kama Disney World huko America
 
Dar ya mwaka gani unauongelea? Dar ya leo siyo dar inayotamaniwa na watu mikoani hii ujue, dar iliyokuwa inatamaniwa na watu ni dar ya 1961 mpaka 2000, baada ya hapo hakuna jipya lilopo dar mkoani ukalikosa pengine bahari ya Hindi ila vyote mikoani vipo

Dar iliyotamaniwa ni ile mtu wa mkoani anasikia ukiwa dar radio unasikiliza Masaa 24, mtu wa mkoani anashangaa

Ukiwa dar wanawake wanajiuza uwanja wa fisi, Ohio, kinondoni makaburini mtu wa mkoani anashangaa

Ukiwa dar unapanda dala dala mtu wa mkoani anashangaa

Ukiwa dar kuna mikate mikubwa kweli mtu wa mkoani anashangaa

Ukiwa dar week end unaenda Beach mtu wa mkoani anashangaa na anapata hamu akaione dar na zone hivyo vitu

Dar ile mtu wa mkoani akisema naenda dar anaaga mtaa mzima, na siku akirudi mkoani washikaji wanajaa kijiweni kusikiliza story za dar, na anarudi kapendeza maana mitumba mikoani ilikuwa tatizo kwaiyo akirudi mkoani kavaa hata ronya ronya za manzese anaonekana kapendeza maana mkoni kupata nguo nzuri ilikuwa kazi na kama jamaa mjanja atarudi na kanda za radio karekodi miziki radio Tanzania haaa haaa basi anajiona mjanja

Dar ambayo TV na deki ndio zinauzwa mkoani ukuti duka la deki au TV mtu anatoka mkoani anakuja dar kwa lengo la kununua TV na deki [emoji3][emoji3][emoji3] hii nchi imetoka mbali basi tu

Dar ambao mikoa ya mbali watu wanatumia siku mbili mpaka tatu kufika kutokana na miundombinu ya Barbara

Dar ambayo haifiki uku mbezi mwisho ukifika kimara wewe upo porini ndio dar watu walitamani

Siyo dar ya leo mtu unaishi goba, mandale uko [emoji16][emoji16][emoji16] hii siyo dar inayotamaniwa maana ishakuwa vurugu mechi

leo hii hayo niliyoyasema mikoani yapo, dar ya leo vurugu mechi tupu manzese darajani si kivutio tena madaraja hayo kila kona dar yapo, mikoani yapo

So dar ipi unaisemea wewe?
uchambuzi bora sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umejikumbusha boarding, kuna jamaa tulitoka nae dar kuja kupga shule Singida,
Jamaa alikuwa anakusanya wanafunzi waliotoka mikoani na kuwadanganya dar ilivyo,dah hatar sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafisi nilijua ukifika Dar hautaona mbu, nzi wala mende. Nilijua Dar watu wote angalau wana elimu ya kidato cha nne. Nilijua nyumba zimepangiliwa na niliamini ukiwa Dar unaweza kukutana na Raisi muda wowote barabarani na niliamini kuwa huenda watu wa Dar hupewa kitoweo cha samaki bure eti kwa sababu bahari ya Hindi iko mwambao wa jiji la Dar na yote hayo nikajikuta yako kinyume kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sista aliletewa house girl kutoka bukoba dah aliingia dar saa nane usiku kulivyokucha akatoka nje akaona mazingira akaanza kucheka anawauliza hapa ndo dar?mbona kwa hovyo hivi mnaishije m naondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla sijaja Dar miaka ya nyuma nilikuwa nikiambiwa Dar wanawake wote wanajiuza na ni Malaya, siku natoka kijijini babu alinionya sana kwamba Dar wanawake wote wana ukimwi. Dah jamaa mmoja aliyekuja kijijini akaniambia yaani wewe ukitaka mwanamke unamuita tu unamwambia ukamtie anakubali hakuna anaekataa! Doh nilimvamia Dada moja mitaa ya Sinza miaka hiyo ya nyuma sana nikamwambia we Dada twende nikakut.o.m.b.e kilichonikuta nakijua mwenyewe!

Sent using kidole gumba
Mkuu naomba umalizie kilikukuta nn baada ya kumwambia huyo dada ukamt...e
 
Nadhani wengi wa mikoani nikimaanisha vijijini hudhani Dar es salaam ni kama mbinguni...

yani mambo yote yamenyoka...

Hili jiji ni zuri sana ukiwa na kipato kinachoeleweka na ni chungu sana endapo utakua unaunga unga...



Cc: mahondaw
 
Yote tisa kumi sasa boarding sasa watoto wa Dar walikua wanajiona wametoka sijui Beverly Hills dadeq kulikua na kundi la watoto wa Tabata basi maskini sisi wa mkoa tunajua Tabata is the place to be... afu mi nlijuaga tanki bovu kuna booooonge la mtenki umekaa pale una mikutu sijui 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sikukulia bush but nilikulia Kati ya hii mjini ya southern Highlands. Niliposikia Dar nilifikiri ni bonge la jiji na zuri mno .Mimi mwenyewe Dar es salaam nimefika nikiwa mtu mzima kabisa ukitoa posta Ile na mitaa michache Dar paovyo kabisa. Mixer kariakoo sahizi wamachinga wamejazana kila Kona zamani kariakoo palikuwaga PA ukweli Ila January nilipokuwepo kule pameharibika mno. Miji ambayo nimefika Tanzania ni Mbeya , Arusha , Mwanza n.k. Nchi za nje nimefika Dubai United Arab Emirates na Bangkok Thailand n.k. kwakweli siku nilipofika Dubai ndio nikagundua kama nipo Dunia nyingine na nilipofika Thailand ndio ilivyokuwa mixer flyover na Majengo marefu. Kiufupi majiji ya Tanzania ni vijij vikubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom