Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu Umenichekesh sana, uwe na siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kiukweli sijakulia bushi ila nmekulia Moshi mjini sema nmesoma boarding sana. Mimi Dar nlijuaga kwanza hamna washamba yan kila mtu mtoto wa mjini yani nikiambiwa tuna safari ya Dar naingia kiboriloni nikafanye shopping kwanza nisionekane wa kuja🤣🤣🤣🤣🤣 dah maisha haya....
 

Ukiwa na hela hata ukizungumza pumba unaonekana una akili mnoooo wakati mwenye PHD anaonekana fala ila mchaga hata akiwa wa kishumundu anaweza kukuingiza mjini na ujanja wako, matapeli sana hao wa kishumundu

Ungekuwa mkazi wa manzese ungeelewa, lile daraja la manzese ukifika jioni au sikukuuu unaona watu wengi wanaoshea sura pale darajani. Watu wengine wanaenda kupata upepo wengine wanapiga picha pale, wengine wanaenda kukaa pale. Watu wanapaona kama Disney World huko America
 
uchambuzi bora sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umejikumbusha boarding, kuna jamaa tulitoka nae dar kuja kupga shule Singida,
Jamaa alikuwa anakusanya wanafunzi waliotoka mikoani na kuwadanganya dar ilivyo,dah hatar sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafisi nilijua ukifika Dar hautaona mbu, nzi wala mende. Nilijua Dar watu wote angalau wana elimu ya kidato cha nne. Nilijua nyumba zimepangiliwa na niliamini ukiwa Dar unaweza kukutana na Raisi muda wowote barabarani na niliamini kuwa huenda watu wa Dar hupewa kitoweo cha samaki bure eti kwa sababu bahari ya Hindi iko mwambao wa jiji la Dar na yote hayo nikajikuta yako kinyume kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sista aliletewa house girl kutoka bukoba dah aliingia dar saa nane usiku kulivyokucha akatoka nje akaona mazingira akaanza kucheka anawauliza hapa ndo dar?mbona kwa hovyo hivi mnaishije m naondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba umalizie kilikukuta nn baada ya kumwambia huyo dada ukamt...e
 
Nadhani wengi wa mikoani nikimaanisha vijijini hudhani Dar es salaam ni kama mbinguni...

yani mambo yote yamenyoka...

Hili jiji ni zuri sana ukiwa na kipato kinachoeleweka na ni chungu sana endapo utakua unaunga unga...



Cc: mahondaw
 
Yote tisa kumi sasa boarding sasa watoto wa Dar walikua wanajiona wametoka sijui Beverly Hills dadeq kulikua na kundi la watoto wa Tabata basi maskini sisi wa mkoa tunajua Tabata is the place to be... afu mi nlijuaga tanki bovu kuna booooonge la mtenki umekaa pale una mikutu sijui 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sikukulia bush but nilikulia Kati ya hii mjini ya southern Highlands. Niliposikia Dar nilifikiri ni bonge la jiji na zuri mno .Mimi mwenyewe Dar es salaam nimefika nikiwa mtu mzima kabisa ukitoa posta Ile na mitaa michache Dar paovyo kabisa. Mixer kariakoo sahizi wamachinga wamejazana kila Kona zamani kariakoo palikuwaga PA ukweli Ila January nilipokuwepo kule pameharibika mno. Miji ambayo nimefika Tanzania ni Mbeya , Arusha , Mwanza n.k. Nchi za nje nimefika Dubai United Arab Emirates na Bangkok Thailand n.k. kwakweli siku nilipofika Dubai ndio nikagundua kama nipo Dunia nyingine na nilipofika Thailand ndio ilivyokuwa mixer flyover na Majengo marefu. Kiufupi majiji ya Tanzania ni vijij vikubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…