Swali kwa mliokulia vijijini: Mlivyokuwa mnasikia Dar mlidhani ikoje?

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sipati picha hicho kichambo chake

Babu alikuingiza cha kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara ya kwanza kufika Dar nilikuwa STD 2.Nimefika nilikuwa nashangaa magorofa tuu,na watu walivyokuwa wengi,,,magari msululu.Asikwambie mtu lami sasa nilikwenda kuigusa peku kabisa.

Kwa mara ya kwanza naingia Kariakoo purukushani hatari kila mtu namsalimia (mpaka mwenyeji wangu akasema_utachoka kusalimia piga kimya tuu Kariakoo hapa kila mtu na lake).


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa unasalimia kariakoo??[emoji1787][emoji1787][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumba yenyewe imewekwa wavu tuu hakuna vioo
Hewa ya kupigania

Afu jitu likija huku Ileje linashangaa mbona kuna baridi

Unagundua hili chenga kichwani hata Geography ni zero
 
Kwa hapa África mji kama Jonhanesburg ndio mji naona angalau unastahili kuitwa jiji kweli kweli sio kitongoji kama Dar


Sent using IPhone X
 
Enzi hizo nmefaulu form four nikachaguliwa kuja kusoma minaki, siunajua minaki n km ipo dar kidizaini basi kutokana na nilivyokuwa naona ndugu na majirani wanakuja vijijini wameulamba kila nguo niliyokuwa nayo niliiona imechakaa nkabidi nijichangechange ninunue nguo mpya nikidhani dar watu full kupendeza muda wote loooh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nilivyofika nilijutia uamuzi wangu wa kuacha nguo zangu kijijini watu wamechakaa balaa. Nikajagundua kumbe wale ndugu zangu na majirani wakija vijijini huwa wanajichanga na kununua vinguo vipya kutuchanga tu kumbe hamna lolote.
 
Hahahahaha umenichekesha Sana hapo kwenye bonge la mtenki wenye kutu kutu
 
Mimi nilijuaga watu wote wanaishi kama mafront page ya gazeti la sani....yaani watu wanakula good time tu na mapikipiki beach.

Halafu mnaishi kama madege hakuna kwenda shule(maana nlikuwa nachukia shule kiahezi)..mnaakaa vijiwwni tu kwenye magogo mnapiga story tu...ilimradi tu msikutwe na kifimbo cheza mkicheza na lugha ya kiswahili.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Club raha leo showwwww! RADIO TANZANI Jambo, tuimbe sote, pole kwa kazi, Mchana mwema, shambani juma hili, Ombi lako, Jioni njema, gazeti la Sani, Bulicheka, ndege kushusha na kupanda, Meli, Train yalikuwa ni maisha ya watu wa DSM tu ndiyo walihusika kuyatumia.

Ukiingia Dar kwa mara ya kwanza kila mtu ngozi nyororooo! msafiii, amevaa viatu, hata mpiga debe! Magari yanapita mfululizo yaani foleni, tena mazuriii Mikoani mpaka Rais au waziri aende huko ndiyo utaona gari zapita mfululizo! ubwabwa ndaza vya nazi na maharage/ kisamvu ni utamu usiomithirika!
 
Nilipokuwa naenda kwa bibi ningali mdogo niliulizwa sana kuhusu daraja la Manzese na kama Van Damme na Anold wanaishi dar hahaaaaaaaaaaaaaa
 
Cha kushangaza watu wa mkoa ni jinsi watu wa Dar wanavyo meza mboga tu asubuhi bila ugali, kwa kisingizio eti ni supu, mara ya kuku, ng'ombe sijui mbuzi!!! Mkoani kwetu hii ni hasara kubwa sana, kumeza mboga nyingi bila ugali.

Ubwabwa kabisaa tena wa mafuta wanakula na Nyama jamani? huu si uharibifu huu? haya kama haitoshi safari fupi tu kama Mwenge Posta wanapanda gari? Mziki mnene na mispika ya kutosha unapigwa Bar jirani tunaburudishwa tena bure? ajabu sasa wengine wanasema ni kelele!

Mgeni wa Ikulu akija Dar miziki ya Dansi inatoa Burudani la kufa mtu Bureee! muda wako tu! yalinishangaza sana haya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…