Nakanusha tamko lako mpaka hapo utakapoweza kuonyesha kosa katika hoja hii:
1. KIla palipo na tofauti za sifa kuna viti zaidi ya kimoja, na kila palipo na usawa wa sifa kuna kitu kimoja.
2. Kuna tofauti kati ya Yesu Mkatoliki na Yesu asiye Mkatoliki:
-- Kwa mfano, Yesu Mkatoliki hapendi wafuasi wake watumie kingamimba isipokuwa njia ya kufuata mzunguka wa ruruba na ugumba katika mwili wa mwanamke (tangu 1968), kwa mfano, wakati Yesu Mlutheri anapenda wafuasi wake watumie kingamimba (tangu 1930).
-- Kwa mfano tena, Kwa mujibu wa Kanuni ya imani, Yesu Mkatoliki ni njia iliyomleta Roho Mtakatifu, wakati Yesu wa Kanisa la Mashariki sio njia iliyomleta Roho Mtakatifu (rejea
the filioque question)
-- Kwa mfano mwingine tena, ni kwamba, wakati wa mchakato wa sonceration, Yesu Mkatoliki anaingia mzima mzima kwenye Mkate na Divai kupitia mchakato unaoitwa transubstantiation, wakati Yesu Mlutheri haingii kabisa na hana experience yoyoye ya mcgakato unaoitwa transubstantiation.
- Na mfano wa nne, Yesu mkatoliki alianzisha sakramenti ya upadre lkn be Yesu mlurheri hakufanya hivyo.
3. Kwa hiyo, Yesu Mkatoliki ni tofauti na Yesu asiye Mkatoliki. Period.
Kukataa hoja hii ni kutangaza kuwa umeshindwa kuelewa
the principle of individuation, na ukakwama kuitumia katika senario ya sasa hivi.
Hata sielewi kwenye metaphysics of the one and many, universals and particulars, na topiki kama hizi walisoma nini na kuelewa nini.
Watu wengi waliopata F ya hesabu au walisoma ungwini wanapata shida kuelewa kanuni hii.
Nakuonyeni:
Enzi za kuwaburuza Waafrika zimepita! Jipangeni kuukabili ukweli.
Kumbukeni:
Uhuru wa Watanzania kufikiri na kusema tunachofikiri hauna mipaka ya kidini, kijiografia, kitaifa, wala vinginevyo.
Tuko macho dhidi ya ukoloni wa kimawazo!