Swali kwa Viongozi CHADEMA: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?

Swali kwa Viongozi CHADEMA: Kumwombea Mbowe ni sehemu ya ibada kwa Mungu yupi?

Naina hata hujaelewa hoja.
NImesema: YESU NI MWANA WA MUNGU.
Maneno YESU na Mungu yana maana nyingi.
Kuna Yesu wa Kanisa la Magharibu, Yesu wa Kanisa la Mashariki, Yesu Mlutheri, etc
Pia kuna Mungu wa Kanisa la Magharibu, Mungu wa Kanisa la Mashariki, Mungu wa Mlutheri, etc
Ukifanya substitutions unapata jibu.
Usinipotezee muda.
Nafanya mambo muhimu kuliko hilo swali lako.
Kwa heri
Mbowe anaombewa kwa miungu yote kwa sababu inaaminika miungu yote inapenda haki.
 
Anajambajamba tu.
Nakanusha tamko lako mpaka hapo utakapoweza kuonyesha kosa katika hoja hii:

1. KIla palipo na tofauti za sifa kuna viti zaidi ya kimoja, na kila palipo na usawa wa sifa kuna kitu kimoja.

2. Kuna tofauti kati ya Yesu Mkatoliki na Yesu asiye Mkatoliki:

-- Kwa mfano, Yesu Mkatoliki hapendi wafuasi wake watumie kingamimba isipokuwa njia ya kufuata mzunguka wa ruruba na ugumba katika mwili wa mwanamke (tangu 1968), kwa mfano, wakati Yesu Mlutheri anapenda wafuasi wake watumie kingamimba (tangu 1930).

-- Kwa mfano tena, Kwa mujibu wa Kanuni ya imani, Yesu Mkatoliki ni njia iliyomleta Roho Mtakatifu, wakati Yesu wa Kanisa la Mashariki sio njia iliyomleta Roho Mtakatifu (rejea the filioque question)

-- Kwa mfano mwingine tena, ni kwamba, wakati wa mchakato wa sonceration, Yesu Mkatoliki anaingia mzima mzima kwenye Mkate na Divai kupitia mchakato unaoitwa transubstantiation, wakati Yesu Mlutheri haingii kabisa na hana experience yoyoye ya mcgakato unaoitwa transubstantiation.

- Na mfano wa nne, Yesu mkatoliki alianzisha sakramenti ya upadre lkn be Yesu mlurheri hakufanya hivyo.

3. Kwa hiyo, Yesu Mkatoliki ni tofauti na Yesu asiye Mkatoliki. Period.

Kukataa hoja hii ni kutangaza kuwa umeshindwa kuelewa the principle of individuation, na ukakwama kuitumia katika senario ya sasa hivi.

Hata sielewi kwenye metaphysics of the one and many, universals and particulars, na topiki kama hizi walisoma nini na kuelewa nini.

Watu wengi waliopata F ya hesabu au walisoma ungwini wanapata shida kuelewa kanuni hii.

Nakuonyeni:

Enzi za kuwaburuza Waafrika zimepita! Jipangeni kuukabili ukweli.

Kumbukeni:

Uhuru wa Watanzania kufikiri na kusema tunachofikiri hauna mipaka ya kidini, kijiografia, kitaifa, wala vinginevyo.

Tuko macho dhidi ya ukoloni wa kimawazo!
 
Lini Mbowe alikuambia haya unayosema?
Kuomba ni HAKI aliyo nayo muumini wa Mungu fulani.
Kama siamini kwamba kuna ng'ombe siwezi kuomba "maziwa" ya ng'ombe.
Mbowe anaamini kuwa Mungu wa Wakatoliki hayupo na ndio maana sio Mkatoliki. Kwa hiyo hawezi na hapaswi kuomba wala kuombewa "maziwa" kutoka kwa Mungu huyu.
Mbowe anaamini kwamba Mungu wa Walutheri yupo na ndio maana ni Mlutheri. Kwa hiyo anaweza kuomba na kuombewa "maziwa" kutoka kwa Mungu huyu pekee.
 
Kwa hiyo kuua mtu kwa kutumia radi ni kitendo cha haki?
Inaaminika ukiiudhi miungu huwa inaleta majanga na maafa hadi toba itakapoombwa ikiambatana na sadaka au kafara.
 
Wanaomini miungu hulipiza kisasi au huwapa watu karma zao.
Katika ulimwengu wa essentialism haki na majukumu vinaanzia na kukomea katika hulka ya binadamu ambayo sio plastiki kihivyo.

Kwa hivyo, kuongelea haki na majukumu katika mtazamo wa constructivism ni jambo ambalo limekataliwa na wanazuoni mamboleo wote.
 
Inaaminika ukiiudhi miungu huwa inaleta majanga na maafa hadi toba itakapoombwa ikiambatana na sadaka au kafara.
Hiyo ni teolojia ya sadistic God, who by definition is an evil and unjust God
 
miungu imeanza kuabudiwa zamani sana kabla hata ya hao wanazuoni mamboleo hawajawahi kuwepo na wanazuoni mamboleo wako wa aina nyingi sana, inategemea yupi unachagua na unapenda kumuamini.
Katika ulimwengu wa essentialism haki na majukumu vinaanzia na kukomea katika hulka ya binadamu ambayo sio plastiki kihivyo.

Kwa hivyo, kuongelea haki na majukumu katika mtazamo wa constructivism ni jambo ambalo limekataliwa na wanazuoni mamboleo wote.
 
miungu imeanza kuabudiwa zamani sana kabla hata ya hao wanazuoni mamboleo hawajawahi kuwepo na wanazuoni mamboleo wako wa aina nyingi sana, inategemea yupi unachagua na unapenda kumuamini.
Hoja yangu ni fupi kuhusu jambo hili. Divine attributes zinazojadiliwa na wanazuoni ni zile ambazo zinatajwa na waumini (subjective conceptions of God). Na hizo ndizo tunaweza kujadili.

Hivyo, kusema kwamba Mungu alikuwepo kabla ya wanazuoni au vinginevyo, sio jibu kwa kitendawili kilicho mbele yetu.

Yaani, katika ngazi ya udadavuzi kama wanazuoni, tunachohitaji ni seti ya sifa za kimungu ambazo hazikanyagani.

Ni kwa jinsi hii tunatofautisha miungu ya kweli na miungu inayochongwa na viongozi wa kidini ambao ni matapeli wa kiteolojia.
 
Kuwaadhibu waovu ni u-sadistic?
Ndiyo. Kuna adhabu ambazo sio sadistic. Maumivu ni sehemu ya uovu wa kifizikia na kisaikolojia. Kuchagua uovu wa kifizikia na kisaikolojia kama njia ya kukamilisha lengo jema kimaadili ni kujiweka katika kundi la wattu wanaotendaji maovu ya kimaadili.
 
Back
Top Bottom