Nikipiga simu leo katika mtandao fulani ikiwa haipatikani au mfano wake, huwa unasikia sauti ya nani ? Jinsia ya kike au ya kiume. ? Ulishawahi kujiuliza kwanini hili limekuwa sana ? Au walio fanya hivyi wajinga hawana akili ?
Sehemu nyingi za starehe, kuna yale mambo yenu ya ofa kwa wanawake, huwa wanaita "Ladies Free" ?
Mnatumika kwenye matangazo ya biashara. Suala la ulimbwende (Umiss) kuna tija gani zaidi ya kudhalilishwa na hampigi kelele, sasa mbona mnajitia upofu hali mmepwa macho ? Mwalimu wenu aliwaona nyinyi wajinga tangu siku ya kwanza, ndiyo maana anawafanya mnavyotaka na mnaona sawa, ila tukiwaambia mrudi kwenye asili mna rauka rauka.
Nani miongoni mwa wakubwa wenu aliwahi kutoka kifua mbele na kukemea mwanamke kujiuza kama bidhai, zaidi ya watu wa Dini ?
Mwanamke hakuwahi kuwa dhalili kama kipindi hiki, mwenye akili anaona na anazingatia.
Mwanamke mtu bora sana kiasili na nafasi yake ni kubwa mno, ila siyo wanawake nyinyi ambao hamjui kipi kina wadhuru na kipi kinawanufaisha.
Ahsante.