Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Naendelea kunukuu...

Hoja kuu ya wale ambao wanasema kuwa katika masuala ya haki za kifamilia tunapaswa kufuata mfumo wa Kimagharibi, ni kuwa muda umebadilika na mahitaji ya karne hii yanatutaka tufanye hivyo. Tunaonelea kuwa ni vizuri tuyaweke maoni yetu wazi juu ya nukta hii, kwa sababu bila kufanya hivyo, mjadala juu ya nukta yoyote hautakuwa kamili, ingawa kwa sababu ya uchache wa nafasi haiwezekani kulijadili suala hili kwa mitazamo yake yote, kifalsafa, kisheria, kijamii na kimaadili. Itatosheleza hapa kujadili nukta mbili tu. Nukta ya kwanza ni kwamba kuafikiana kwayo na kukubaliana na mabadiliko ya wakati sio suala rahisi sana kama baadhi ya watu wasiojua wanavyofikiri. Mabadiliko yanayoletwa na wakati, wakati fulani huwa ni ya kurudisha maendeleo nyuma. Tunapaswa kwenda na mabadiliko ya wakati ya kimaendeleo na tunapaswa kuyapiga vita mabadiliko yanayoletwa na wakati ambayo ni ya kiharibifu. Ili kutofautisha aina hizi mbili za mabadiliko na kujua asili yake, tunapaswa kujua chanzo cha maendeleo (ugunduzi au mabadiliko) haya mapya na yameelekezwa katika mwelekeo gani. Tunapaswa kuangalia ni tabia gani za kibinadamu zimeyaleta (njema au mbaya) na ni matabaka gani ya watu yanatetea mambo haya mapya? Tunapaswa kuangalia je yameletwa na tabia tukufu za mwanadamu au matamanio duni yanayofanana na wanyama, na kama yamekuja kama matokeo ya uchunguzi usio wa kibinafsi wa wanazuoni na wasomi, au yameletwa na matamanio duni ya wanaotumikia nafsi zao na tabia za kifisadi za jamii. (Mwisho wa kunukuu).

Tunaondoka na nukta mbili sasa.
 
Tatizo mtizamo!,,

upendo wa mama ni muhimu sana na njia za kuonyesha upendo huo si moja tu.,
Mama ukijipanga unaweza jishughulisha na kuhudumia watoto vizuri
Siyo kwa njia hii mnayopita bibie, usibishane ukweli.
 
Unamaanisha hamna wanawake wanaopata kitu katika kutafuta😅😅?..
Uko sayari nyingine nini mkuu?
Punguza hasira kidogo unaweza ona ukweli
Nionyeshe ukweli bibie.
 
Kama nakuona hapo na vidole vitatu hewani ukinisunta hahahaha

Kama ulivyosema wino umekauka na kalamu zimenyanyuliwa ndivyo wanawake tumeshaamka.

Bado wale wa kuolewa wanne mume mmoja ipo siku wataamka tu
Nacheka sana, naandika kuhusu haki na wenye haki uwajue.

Naona ukweli ninao usema unadhihiri, hamna hoja, nasema hata mjikusanye makumi kwa mamia, hamtaweza kuonyesha "umgando" wa hiki ninachokiandika. Wingi una ni jinsia ya kike.

Umegusia kuhusu vidole juu na kusutana, najua kuhusu kujeruhi kwa elimu na insafu na hili ndiyo nalinya hapa.Maana hata nikikuomba ushahidi wa hilo la vidole juu huna ithibati zaidi ya kuendelea kuwasilisha hisia zako. Sasa usiandike mambo ili kurahisha nafsi yako, bali andika kuhusu ukweli na haki kwa ajilu ya maslahi na kuwazindua watu.

Ukiwa na hoja nistue, ama kuhusu hisia hata kuku anazo.

Utanikuta hapa hapa,tukijaaliwa.
 
Nimeshindwa kweli sasa hapa unataka hoja gani. Mimi mwanamke msomi nimeenda shule nimegradute nimeajiriwa natengeza pesa napendeza mambo yananinyookea nikae nabishana na mtu anataka niwe housewife kazi kubwa ni kuzaa na kuitikia wito wa mume kila atakaponihitaji na nikikataa malaika watanilaani mpaka kunakucha.Huo mda wa kupanga na kupangua hoja natoa wapi?
Sawa.
 
Endelea kukaa kwenye nyumba za tembe achana na nyumba za kisasa tulizoiga kutoka magharibi,
Endelea kupanda punda achana na magari na ndege za magharibi,
Vaa ngozi za wanyama acha suti na kanzu za waarabu,
kukeketa wanawake,
Rudi kwenye utawala wa machifu achana na demokrasia.

Unataka wasiwepo walinzi wa kike ili mke awe anapapaswa na wa kiume kwenye ukaguzi?

Hutaki askari wa kike kwa ajili ya kushugulika na wanawake?

Hutaki madaktari wengi wa kike wanawake waweze kushughulikiwa mambo yao kwa fargha zaidi?

Usingependa kuwa na Kiongozi Bora kama Angel Merkel au

Usingependa kuiona dunia ikiwa na kina Marie Curie wengi zaidi,mvumbuzi wa radioactivity aliyetoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya x-ray,mionzi na tiba za cancer?

Nawaonea huruma watoto wako wa kike kwa kuwa na baba kama wewe,Namshanga na kumsikitikia mwanamke aliyukubali kuleta kiumbe duniani pamoja na wewe.
Naona umevamia bila kuelewa kiini, akili salama inamtaka mtu aige vya maana, vya kijinga unachuja kisha unaachana navyo, na hi tunalo jijadili hapa ni miongoni mwa mambo ya kijinga na yasiyo faa kuigwa, sasa jifunze kuweka kila kitu mahala pake.

Nipo....
 
Kama wakatazwe naomba ushahidi wa katazo hilo limetoka wapi ?
Naomba unipe ushahidi unao wataka wao wasome hizo elimu ? Kisha rejea swali langu na ujibu kwa mujibu wa swali langu linavyotaka.
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👊🏽

Mimi ni mwanamke wa kiislamu na kamwe siwezi kuunga hoja za huyu jamaa. Tatizo lenu mnatumia imani kumkandamiza mwanamke. Mwanamke kufanya kazi au biashara ni kosa? Mbona bi khadija R.A alikua mfanyabiashara mkubwa kipindi chake? Na yeye alikua anatumia mwili wake kama kivutio katika biashara zake? Kama sio what's the exception? Ulikuepo ? Je mtume S.a.w baada ya kumuoa bi Khadija alimuamuru aache kazi zake na kukaa ndani? Au alijiunga nae na kuendeleza biashara pamoja. Acheni kutumia dini kwa manufaa yenu binafsi.
 
Mimi ni mwanamke wa kiislamu na kamwe siwezi kuunga hoja za huyu jamaa. Tatizo lenu mnatumia imani kumkandamiza mwanamke. Mwanamke kufanya kazi au biashara ni kosa? Mbona bi khadija R.A alikua mfanyabiashara mkubwa kipindi chake?
Biashara zake alikuwa anazifanyaje baada ya kuolewa na mtume ?

Biashara zake alikuwa anazifanya yeye au alikuwa anazifanya mtume kwa kumuagiza ?
Kama huna elimu ya dini bora kuuliza na si kumzulia mama yetu Khadija.
Niambie imani ya Uislamu imetumika wapi kumkandamiza mwanamke ? Ukionyesha hilo, mimi naomba uongozi wa "jf" waifute hii ID yangu na wewe utakuwa shahidi wa hili.
Uislamu unaangalia maslahi dhidi ya ufisadi bibie.

Hujaambiwa mwanamke kufanya biashara ni kosa na ndiyo maana tulisema huko nyuma ya kuwa mwanamke anaruhusiwa kumiliki mali, ila kwa njia ambazo ni salama kwake na si kwa njia ambazo mnapita nyinyi,njia za kushindana na wanaume katika uovu.
Na yeye alikua anatumia mwili wake kama kivutio katika biashara zake?
Nionyeshe baada ya mtume kumuoa mama Khadija,mama Khadija alikuwa anafsnyaje biashara zake ?

Hivi hizi habari umezisoma wapi bibie ? Mbona unakuwa muongo na kumzulia mama Khadija ? Inaonekana uliposikia kwamba mama Khadija alijaaliwa mali na mfanya biashara, ukamfananisha na nyinyi wa leo ? Havilingani viwili hivi, umbali wake ni sawa na mbingu na ardhi.
Je mtume S.a.w baada ya kumuoa bi Khadija alimuamuru aache kazi zake na kukaa ndani? Au alijiunga nae na kuendeleza biashara pamoja. Acheni kutumia dini kwa manufaa yenu binafsi.
Sasa utuonyeshe wewe, baada ya mama Khadina kuolewa na mtume, alikuwa anatoka na kwenda kuparanganyikana na wanaume katika kutafuta na mfano wa hayo ?

Kipindi, mtume anapewa utume mama Khadija alikuwa anachakarika ?
Au alijiunga nae na kuendeleza biashara pamoja.
Mama Khadija alikaa nyumbani na shughuli za biashara akawa anazifanya mtume na kuzisimimamia.
 
Hawa wanaume sijui wanatuchukuliaje, Yani wanatuona sisi ka kitu kisicho thamani wanakera Sana. Na sisi hatuwezi acha kufanya kazi tujipatie kipato maana ukimtegemea mwanaume lazima ufe maskini

Huyu mwanaJF Jurjani mtizamo wake uko finyu sana.

Mimi nimeenda shule ya msingi yenye waalimu 50. Waalimu 49 walikuwa wanawake kasoro mwalimu mmoja. Sekondari hivyo hivyo waalimu wanawake walikuwa majority. Chuoni ni hivyo hivyo kina mama wengine walitupiga lecture.

Sasa hawa mama zetu wangezuiwa kutoka kwenda kufundisha shuleni sijui hali ingekuwaje na huu ni mfano mmoja wa jamii na familia kufaidika kwa mwanamke kufanya kazi nje ya makaazi yake ktk sekta ya elimu.

Bado kuna sekta kibao mama ntilie, udaktari, Uganga wa kienyeji, Uongozi wa Taasisi listi ni ndefu kina mama wame changia ktk uchumi, jamii na taifa.
 
Naomba unipe ushahidi unao wataka wao wasome hizo elimu ?
Unajidhalilisha mkuu.

الأصل في أشياء مباح.

Asili katika mambo ni kuwa yanafaa.

Yale yasiyokuwa ya kiibada yanafaa kuyafanya ikiwa hakuna katazo la wazi,kutokuwepo kwa katazo la jambo ambalo sio la kiibada basi hiyo ni ruhusa.

Nadhani huu msingi unaufahamu vizuri sana.

Kusomea udaktari na urubani kwa wanawake hizi fani ni katika mambo ya mubaahu,sio ya kiibada hivyo haya anayekataza ndio atoe dalili kwa sababu asili yake ni halali.

Unayo dalili ya kumkataza mwanamke kusomea hizo fani ambazo ni mubaaha ?
 
Huyu mwanaJF Jurjani mtizamo wake uko finyu sana.

Mimi nimeenda shule ya msingi yenye waalimu 50. Waalimu 49 walikuwa wanawake kasoro mwalimu mmoja. Sekondari hivyo hivyo waalimu wanawake walikuwa majority. Chuoni ni hivyo hivyo kina mama wengine walitupiga lecture.

Sasa hawa mama zetu wangezuiwa kutoka kwenda kufundisha shuleni sijui hali ingekuwaje na huu ni mfano mmoja wa jamii na familia kufaidika kwa mwanamke kufanya kazi nje ya makaazi yake ktk sekta ya elimu.

Bado kuna sekta kibao mama ntilie, udaktari, Uganga wa kienyeji, Uongozi wa Taasisi listi ni ndefu kina mama wame changia ktk uchumi, jamii na taifa.
Kuna watu wanatumia jukwaa kubwa ka JF Ila bado wako gizani Sana, just think kuwa mwanaume ni kila kitu kumbe si kweli na bado wanafikiria kazi za kuzalilisha ni wanawake kwenda ofisini, wakati tangu zamani wanawake hufanya kazi kuanzia za shamba, kuvuna na kulisha familia huku wanaume wakisubiri yavunwe. Na kuuzwa wachukue hela. In short wamama ndio wamebeba Mambo mengi kiuchumi, nimekuwa naona wanawake wanaamka saa kumi kujitaftia hela za kulea huku mchango wa wanaume sio kivile. Lazima tu kubali wanawake wanajitoa mno kupita maelezo, Sasa mtu akija hapa kuponda huwa simwelewi kabisa
 
Back
Top Bottom