Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Naendelea kunukuu...

Hoja kuu ya wale ambao wanasema kuwa katika masuala ya haki za kifamilia tunapaswa kufuata mfumo wa Kimagharibi, ni kuwa muda umebadilika na mahitaji ya karne hii yanatutaka tufanye hivyo. Tunaonelea kuwa ni vizuri tuyaweke maoni yetu wazi juu ya nukta hii, kwa sababu bila kufanya hivyo, mjadala juu ya nukta yoyote hautakuwa kamili, ingawa kwa sababu ya uchache wa nafasi haiwezekani kulijadili suala hili kwa mitazamo yake yote, kifalsafa, kisheria, kijamii na kimaadili. Itatosheleza hapa kujadili nukta mbili tu. Nukta ya kwanza ni kwamba kuafikiana kwayo na kukubaliana na mabadiliko ya wakati sio suala rahisi sana kama baadhi ya watu wasiojua wanavyofikiri. Mabadiliko yanayoletwa na wakati, wakati fulani huwa ni ya kurudisha maendeleo nyuma. Tunapaswa kwenda na mabadiliko ya wakati ya kimaendeleo na tunapaswa kuyapiga vita mabadiliko yanayoletwa na wakati ambayo ni ya kiharibifu. Ili kutofautisha aina hizi mbili za mabadiliko na kujua asili yake, tunapaswa kujua chanzo cha maendeleo (ugunduzi au mabadiliko) haya mapya na yameelekezwa katika mwelekeo gani. Tunapaswa kuangalia ni tabia gani za kibinadamu zimeyaleta (njema au mbaya) na ni matabaka gani ya watu yanatetea mambo haya mapya? Tunapaswa kuangalia je yameletwa na tabia tukufu za mwanadamu au matamanio duni yanayofanana na wanyama, na kama yamekuja kama matokeo ya uchunguzi usio wa kibinafsi wa wanazuoni na wasomi, au yameletwa na matamanio duni ya wanaotumikia nafsi zao na tabia za kifisadi za jamii. (Mwisho wa kunukuu).

Tunaondoka na nukta mbili sasa.

Anza kuwafanyia mabinti zako vile unapenda. Ukimalizana anza ku kampeini mawazo yako kwa wanaume wenzako wenye mabinti.
 
Unajidhalilisha mkuu.

الأصل في أشياء مباح.

Asili katika mambo ni kuwa yanafaa.

Yale yasiyokuwa ya kiibada yanafaa kuyafanya ikiwa hakuna katazo la wazi,kutokuwepo kwa katazo la jambo ambalo sio la kiibada basi hiyo ni ruhusa.

Nadhani huu msingi unaufahamu vizuri sana.

Kusomea udaktari na urubani kwa wanawake hizi fani ni katika mambo ya mubaahu,sio ya kiibada hivyo haya anayekataza ndio atoe dalili kwa sababu asili yake ni halali.

Unayo dalili ya kumkataza mwanamke kusomea hizo fani ambazo ni mubaaha ?
Wewe ndiyo unajidhalilisha kusoma ni ibada au siyo ibada ? Inabidi ukasome tena misingi ya kiusuli na kaida zake. Kaida hii ya kiusuli, ukiisema hivi bila kuichambua unawaachia watu ufahamu mbaya, na kuwapoteza watu. Katika kaida hii chini yake kuna vipengele, vipengele ambavyo ndani yake vina kaida nyingine ya maslahi na mafasidi, katika asili chenye kuleta madhara ni haramu. Wewe leo hii ukila chakula, lakini kikawa kina dhuru kwa muda huo chakula hicho ni haramu kwako, na ukiendelea kukila na huku unajua kinakudhuru unapata madhambi. Sasa hili la kusoma kwa kukusaidia, haliaangaliwi kijuu juu,bali lina pimwa katika uzani wa faida na hasara na kuangaliwa lipi bora zaidi kisha linatangulizwa. Rejea Majmui al Fatawa cha Shaykhul Islam Ibn Taymiyyah.

Kisha uniambie ni ipi nafasi ya nia katika matendo ?

Kwahiyo bado nasubiri ushahidi.
 
Mimi ni mwanamke wa kiislamu na kamwe siwezi kuunga hoja za huyu jamaa. Tatizo lenu mnatumia imani kumkandamiza mwanamke. Mwanamke kufanya kazi au biashara ni kosa? Mbona bi khadija R.A alikua mfanyabiashara mkubwa kipindi chake? Na yeye alikua anatumia mwili wake kama kivutio katika biashara zake? Kama sio what's the exception? Ulikuepo ? Je mtume S.a.w baada ya kumuoa bi Khadija alimuamuru aache kazi zake na kukaa ndani? Au alijiunga nae na kuendeleza biashara pamoja. Acheni kutumia dini kwa manufaa yenu binafsi.
Umekuwa bidhaa tyr
 
Kuna watu wanatumia jukwaa kubwa ka JF Ila bado wako gizani Sana, just think kuwa mwanaume ni kila kitu kumbe si kweli na bado wanafikiria kazi za kuzalilisha ni wanawake kwenda ofisini, wakati tangu zamani wanawake hufanya kazi kuanzia za shamba, kuvuna na kulisha familia huku wanaume wakisubiri yavunwe.
Bibie unaposema tangu zamani, ni zama za mababu zako au zamani ipi ?

Pili, bibie kwani unapokula wewe kwa kutumia mkono wa kushoto, ni kwamba mkono wa kulia huwezi kutumia kula au ni nidhamu na adabu ya kula inakutaka hivyo ? Sasa tunaposema mwanamke akae nyumbani kwa ajili ya kulea famili, hatumaanishi ya kuwa mwanamke hawezi kufanya hayo bali akifanha hayo madhara yake yanakuwa makubwa na kuiharibu jamii pakubwa mno, kwani kiasili mwanamke kwake ni nyumbani.

Tatu, sisi siyo kila kitu kwa ujumla wake kwani sisi kuna mengi nyinyi mnayafanya sisi hatuwezi kuyafanya, ila katika suala la kutafuta hela na kujichanganya na kwenda mbali, hili ni jukumu letu sisi, na nyinyi ni wajibu tuwaletee, leo hii mimk familia yangu ikilala njaa, hataulizwa mke wangu, nitaulizwa mimi.

Nne, ukisoma Historia kuna zama zilikuwa mwanamke ndiyo mwenye kuamua mambo, mwanamke alikuwa ana zini na wanaume kadhaa, kisha anamchagua mwenye sifa kuwazidi wenzake anampa mtoto aliye mzaa na kusema huyu mtoto ni wako. Haya yote Historia imeandika.

Tano, mwanamke kulisha familia hili si jambo lake, na ikitokea hivyo ujue si kawaida. Kwahiyo ni makosa kujengea hoja juu ya jambo ambalo ni la kimakosa.
 
In short wamama ndio wamebeba Mambo mengi kiuchumi, nimekuwa naona wanawake wanaamka saa kumi kujitaftia hela za kulea huku mchango wa wanaume sio kivile.
Kuamka kwao na kutafuta ujue ni jambo la kidharura na kuonyesha kuna sehemu haiko sawa, na usawa ni wao kuletewa na kutumia.

Sasa usilazimishe kosa likawa sio kosa, kwani kufanya hivyo ni makosa zaidi.
 
Lazima tu kubali wanawake wanajitoa mno kupita maelezo, Sasa mtu akija hapa kuponda huwa simwelewi kabisa
Kujitoa kwenu ni kimakosa na kuna maafa na kwani mmefanywa vipofu mkiona madhara msiyaseme.
 
Baada ya ng'ombe flani waliokabdhiwa majukumu ya kututunza kushindwa na kuamua kua marioo inabd tuingie maofsini
Kwahiyo wao wakikosea na nyinyi mkosee.

Huku kwetu huwa tunaishi na kauli hii "Nia njema haihalalishi njia".
 
Mimi ni mwanamke wa kiislamu na kamwe siwezi kuunga hoja za huyu jamaa. Tatizo lenu mnatumia imani kumkandamiza mwanamke. Mwanamke kufanya kazi au biashara ni kosa? Mbona bi khadija R.A alikua mfanyabiashara mkubwa kipindi chake? Na yeye alikua anatumia mwili wake kama kivutio katika biashara zake? Kama sio what's the exception? Ulikuepo ? Je mtume S.a.w baada ya kumuoa bi Khadija alimuamuru aache kazi zake na kukaa ndani? Au alijiunga nae na kuendeleza biashara pamoja. Acheni kutumia dini kwa manufaa yenu binafsi.
Nimesumbuana Sana na ndugu yangu Jurjani...huyo ni wale PSYCHOPATH wanaomkandamiza mwanamke Kama ishara ya kuonesha masculinity Yao.....

Tatizo Ukimwambia ukweli ANAKUFURISHA na kusema ATAMCHAPA MTU MAKOFI.....

They are insecured moronic men...
 
wewe ni muislamu poa,uislamu unataka muislamu aufuate na sio vinginevyo....ungekuwa muislamu kweli ungemuunga mkono jamaa,anachozungumzia hapa ni stara ya mwanamke katika maisha yake ya kila siku,mwanamke siyo lazima kuvaa niqab,uso wake si vibaya kuonekana......haya makundi ya kutetea haki za wanawake wangepigania kwanza stara kwa mwanamke na kutumiwa kama chombo au kivutio katika biashara ingekuwa poa.
😂😂😂😂 Looh
 
Nimesumbuana Sana na ndugu yangu Jurjani...huyo ni wale PSYCHOPATH wanaomkandamiza mwanamke Kama ishara ya kuonesha masculinity Yao.....

Tatizo Ukimwambia ukweli ANAKUFURISHA na kusema ATAMCHAPA MTU MAKOFI.....

They are insecured moronic men...
Unaweza kuonyesha wapi katika andiko langu au nilichokiandika kina mkandamiza mwanamke ?

Pili, ukandimizi ni kumyima mtu haki yake aidha kwa kutumia mabavu au masimango, sasa niambie katika hili nililo liandika wapi amekandamizwa mwanamke au ishara ? Zaidi ya kuwazindua nyinyi na wajinga wenzenu.
 
Watu design ya Hawa wanakuaga wameshindwa ht kutunza familia ...bas anatafuta chaka
Nimecheka sana, kwanini una bahatisha bibie, na kuleta dhana ? Hii ni ishara ya kushindwa kujenga hoja na kuitetea hoja yako.

Sasa nashindwaje kutunza familia wakati nahimiza juu ya kuzitunza familia zetu, kwani hili ndiyo jukumu letu sisi na nyinyi tuwetee majumbani,mtumie na mtulele watoto wetu.

Huu ni uwanja wa kuhudhurisha hoja kama nyinyi mnasema ukweli. Kushindwa kutunza familia labda itokee kwa jambo ambalo liko nje ya uwezi wangu, ila sababu najua majukumu yangu, na ninajua familia yangu isipokula wala kuvaa wala kuishi vizuri, nitaulizwa mimi na si mke wangu, kadhalika aibu itakuja kwangu. Kwahiyo tunapambana na ndiyo maana wake zetu wametulia majumbani na wanaishi poa. Akili zao zimetulia, amani imetawala.

Unaposhindwa kuleta hoja bibie, wewe endelea na hicho ulichokichagua, ila ukweli lazima tuwape na hatuangalii nani atalaumu na nani atachukizwa.

Ahsante.
 
Wanaume, Tumelikana jukumu tulilopewa Enzi zile za Adam na Hawa....Nyerere Alisema Wakati wa Chama kimoja," Wakikosa Wanayoyataka ndani ya Chama watayatafuta nje ya Chama"Nimeingizia Tu!
 
Unaweza kuonyesha wapi katika andiko langu au nilichokiandika kina mkandamiza mwanamke ?

Pili, ukandimizi ni kumyima mtu haki yake aidha kwa kutumia mabavu au masimango, sasa niambie katika hili nililo liandika wapi amekandamizwa mwanamke au ishara ? Zaidi ya kuwazindua nyinyi na wajinga wenzenu.

Ndo Mana Nikakuambia Wewe Ni Miongoni Mwa Wakandamizaji Wanawake....

Bwana Traditionalist Skiza Yaa Akhui...Umeona Ulivyo Kuwa Mchache Wa Fadhili Kwa Wanawake ?!!
Ona Hapo Juu..."Kutumia mabavu au masimango"..Umegotea hapo tu Kooo.

Umesahau uliposema kuwa Ni ibn Uthaymeen tu ndio mwenye kuijua hedhi ya kina mama?!!!

Mwanamke ana Ubongo Mwanamke Ana Akili Yaani Elimu Ya Kuujua Mwili wake Amepewa Ashaykhul Muadhama Ashaykhul Kiraam Muhammad Ibn Uthaymeen ?!!😁😁😁 Hapa tu Ni pigo jengine la DHARAU kwao...Ni hatua Nyingine ya kuwadharau......

Ulipinga Mwanamke Kusoma Elimu Faradhil Kifayaa...nakukumbusha,ulinizodoa kuwa Wasiwe Aeronautic Engineers,Space Engineers,Surgeons na Pilots...kwani Inawafaa WANAUME TU...huku Ni kuwadharau....Ni Majuzi tu,UAE mdada Kichwa Balaa amerusha chombo anga za mbali...muislam na mwarabu Yule haya MKUFURISHE na umchape makofi uyapendayo.....Wanawake JIRANI Zake Wa Pale Damaam,Khobar,Jeddah na Najd wanapigania haki zao KUENDESHA MAGARI...😂😂😂 Isn't it INSANITY?!!!!

Innal Batwila Kana Zahuka...
 
Thamani ya kitu inaonekana kikipotea

Labda wanaume tulishindwa kutambua mchango wa wanawake kipindi kile na ndo mana tupo hapa

Kiukweli thamani ya wanawake tumeijua saivi baada ya wanawake wengi kupoteza thamani

Watoto wetu watateseka sana kukosa maleZi bora
 
Nimecheka sana, kwanini una bahatisha bibie, na kuleta dhana ? Hii ni ishara ya kushindwa kujenga hoja na kuitetea hoja yako.

Sasa nashindwaje kutunza familia wakati nahimiza juu ya kuzitunza familia zetu, kwani hili ndiyo jukumu letu sisi na nyinyi tuwetee majumbani,mtumie na mtulele watoto wetu.

Huu ni uwanja wa kuhudhurisha hoja kama nyinyi mnasema ukweli. Kushindwa kutunza familia labda itokee kwa jambo ambalo liko nje ya uwezi wangu, ila sababu najua majukumu yangu, na ninajua familia yangu isipokula wala kuvaa wala kuishi vizuri, nitaulizwa mimi na si mke wangu, kadhalika aibu itakuja kwangu. Kwahiyo tunapambana na ndiyo maana wake zetu wametulia majumbani na wanaishi poa. Akili zao zimetulia, amani imetawala.

Unaposhindwa kuleta hoja bibie, wewe endelea na hicho ulichokichagua, ila ukweli lazima tuwape na hatuangalii nani atalaumu na nani atachukizwa.

Ahsante.
😂😂😂
 
Unaweza kuonyesha wapi katika andiko langu au nilichokiandika kina mkandamiza mwanamke ?

Pili, ukandimizi ni kumyima mtu haki yake aidha kwa kutumia mabavu au masimango, sasa niambie katika hili nililo liandika wapi amekandamizwa mwanamke au ishara ? Zaidi ya kuwazindua nyinyi na wajinga wenzenu.
😲😲😲
 
Back
Top Bottom