Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Kusema nimesoma secular tena waona najifaragua mkuu?
Sahihi kabisa unajifaragua, na ukajenga kwayo kwa uchachefu wako wa maarifa.
Sasa kama kusoma secular sio haramu basi jua pia na huo udaktari sio haramu ati kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanapingana na itikadi ya uislamu.
Hakuna aliyesema kusoma secular ni haramu, bali wanazuoni wetu wamefika mbali wakasema kama kuna sehemu kuna haja ya mtu kuwa na taaluma ya utabibu au uhandisi au mfano wake katika elimu za mazingira, na watu wa eneo wasisome elimu hiyo, watu hao hupata madhambi.

Gogoro linakuja katika mazingira ya upatikanaji wa hizo elimu na mfumo wake, sababu katika viwili hivyo kuna mafsada makubwa kuliko manufaa. Sasa elewa maneno ili usiwe unarudia kuandika vitu ambavyo havina msingi.
 
Mimi nazungumzia asili na nimekupa mifano lukuki kuthibitisha hilo.

Mifano yako uliyoitoa ni mifano ya kiada za watu kutokana na ujinga na imani zao potofu.
 
Asili na mila havipishani mzee.
Asili ni kitu kimoja na mila kadhalika, bali kwa ziada hata kwenye mila na desturi matamshi haya watu wengi huona yako sawa, ila mbele ya wanazuoni wa lugha wameyatofautisha maneno hayo (yaani ada, desturi na mila).

Asili ni kile ambacho juu yake hujengwa mengine.
 
Kwani unaposema asili ya mwanamke ni kukaa ndani haumaanishi kuwa hiyo ndio mila na desturi ya watanzania au waislamu ?
Hii ni sheria, na inaingia katika asili kwa ubainifu wa sheria.
Sasa nikikuambia kuwa asili ni kuwa anaezaa ndio anyonyeshe unakataa nini kuwa sio asili alafu unataka kuitia kwenye kawaida peke yake bila kujua kuwa hii ni asili pia ?
Asili niliyo ipinga ni ile niliyo kuquote katika ada ya Waarabu, suala la mwanamke hili sijakuquote sababu hii inakubalika na inajulikana kuwa ni asili.
 
Asili ya waafrika huko arabuni mfano akila bilali n.k walikuwa ni watumwa,kuwa mtumwa sio asili nzuri na sio jambo zuri lakini ndio asili ya watu weusi wengi huko kwa watu weupe.
Utumwa siyo asili mzee, usichanganye mambo. Hizo ada za watu kwa watu wengine.
 
Ada na dedturi ni vitu viwili tofautu, na tofauti zake wanazuoni wa lugha wanaziingiza katika wingi.
 
Mimi mswahili, tangu nakua mpaka leo hii, kutoka Kimara mpaka Kibaha, hii ni safari, kadhalika mpaka Mkuranga ni safari.
 
Safi. Nipe faida sasa wapi aya imesema wapi wanawake wasitoke hovyo hovyo, na uniambie dharura unaijuaje ?
 
Ukimruhusu mkeo kwenda shuleni unaangalia nini na nini au kwako huangalii usalama wake ?
 
afi. Nipe faida sasa wapi aya imesema wapi wanawake wasitoke hovyo hovyo, na uniambie dharura unaijuaje ?
Yaani mimi ndo nimekuuliza wewe kuhusu dharura unaijuaje alafu unanigeuzia swali mimi nikuambie ?

Wewe ndo umedai mambo ya dharura na ukaeleza kuwa sifa yake kuu ni kutengua kata,,zo

Mimi ndio nimekuuliza kuhusu dharura alafu wewe sasa unanigeuzia kibao wakati wewe ndo ulitakiwa kutoa majibu kuhusu dharura.
 
Mtume hakuainisha kuwa safari ni kilomota ngapi wala ngapi.

Hivyo vipimo labda uviweke wewe hapa kama ambavyo unataka kufanya.
Hili liko wazi ndiyo maana safari hukadiriwa kwa mujibi wa ada ya watu.
 
Ukimruhusu mkeo kwenda shuleni unaangalia nini na nini au kwako huangalii usalama wake ?
Naangalia anachoenda kufanya kama cha halali au haramu.kama cha halali namruhusu.

Pili ashikamane na utaratibu wa sheria pale anapokuwa anazungumza asiwe mwenye kulegeza sauti anapokuwa yupo na watu wengine.

Allah asema.

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

[ AL-AH'ZAB - 32 ]
Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema.

Bila shaka hapa waliambiwa wasilegeze sauti pale wanapokuwa mazingira ambayo sio ya majumbani kwao ama hata majumbani kwao ikiwa watasemeshana na wale wasiokuwa mahrim zao wasifanye hivyo.

Asipeane mikono na watu ajnabi na anatambua hilo.
Atoke akiwa katika stara ya sheria.

Hayo ni katika mambo ya msingi naangalia mimi.

kwako huangalii usalama wake ?
Usalama wa nini ?
 
Hili liko wazi ndiyo maana safari hukadiriwa kwa mujibi wa ada ya watu.
Ndo mana nakuambia kuwa safari ile ya mahrim ni ile safari ya KUSAFIRI na sio safari ya kwenda tu kama kutoka mbagala kwenda kawe.

Hii kutoka mbagala kwenda kawe huwezi kusema ni safari ya mwanamke kutoka na mahrim wake kwa sababu kwa ada ya watu wengi wa daressalam hii sio safari ya kusafiri ni safari ya kwenda tu umbali wa kawaida.

Unapotaka kujaalia kuwa kila safari ni ya kusafiri hili litadhihirisha tena kuwa namna gani dalili unaziweka pahala ambako sio pake.

Safari inafahamika ni ile ya kwamba ukienda watu wa mji huo wanahesabu kuwa umesafiri haswa.

Sasa mwanamke kutoka ndani kwenda kwenye mahitaji yake haihitaji mahrim kwa sababu hiyo sio safari ya kusafiri ,jambo hili unatakiwa ulitoe katika masharti,sio sawa ndugu unafanya ugumu mambo ambayo sheria haikuyazungumza.
 
Mimi mswahili, tangu nakua mpaka leo hii, kutoka Kimara mpaka Kibaha, hii ni safari, kadhalika mpaka Mkuranga ni safari.
Hiyo ni ada yako usilazimishe watu kuona hivyo.

Wapo watu hawaoni kuwa hiyo ni safari ya kusafiri bali hiyo ni safari ya kawaida tu ambayo kisheria sio ile ya kusafiri.

Lakini pia kama wewe unaona ni safari ya kusafiri basi haulazimishwi kuwa usione ni safari ya kusafiri,utafanya wewe kwa uoni wako yale ambayo yanaambatana na usafiri.

Ila usilazimishe mpaka sisi wengine ambao hatuoni kuwa hiyo ni safari ati tuone kuwa ni safari ile ya kusafiri.

Ukilazimisha hivi utakuwa unazidi kuchochea kuni ile tabia yako ya kutaka watu wote wafuate mtazamo wako jambo ambalo sio sahihi.

Safari ya mwanamke kutoka na mahrim ni ile ambayo mwanamke hutoka akihisabika kuwa amesafiri,yaani safari hiyo hadi mwanaume akitoka awe anahisabika kuwa amesafiri.
 
Ada na dedturi ni vitu viwili tofautu, na tofauti zake wanazuoni wa lugha wanaziingiza katika wingi.
Pinga kwa hoja na mifano ambayo nimetoa kuonesha tofauti hizo.sio unapinga kwa kusema wanachuoni wamesema wanachuoni wamesema hivi na vile,hiyo kwangu katika hili sio hoja

Nimekupa mifano na wewe toa mifano kupinga hiyo yangu kuwa nilichosema sio sahihi,huku ndiko kujadili kuzuri,sio kwa hivi unavyomwenda.

Nimekuonesha mifano ya ada ama mila na desturi na mifano yake wewe pinga kwa mifano ambayo itaenda kinyume,sio kutumia neno wanawachuoni kunyamazisha yale ambayo nimeyasema.

Usijadili mambo wakati umevaa miwani ya mtu lazima utayumba tu,kama unajadili unatakiwa uvae miwani yako kwanza alafu ndio ujadili.
 
Aya iko wazi, na udharura wa hilo unakuja kutokana na makatazo na fadhila alizo wekewa mwanamke akiwa nyumbani, kwa maana kuziacha fadhila hizo mpaka iwepo haja ya kufanya hivyo, na hiyo haja hukadiriwa kwa makadirio yake ya kukidhi vigezo. Hii ndiyo dharura.

Sasa nilikushangaa ulipo niuliza udharura kwenye aya uko wapi, hali ya kuwa aya iko wazi na hadithi inaunga mkono jambo hilo.

Alhaafidh Abubakr al Bazzar amesimulia hadithi toka kwa swahaba Anas Ibn Malik, ya kuwa kuna mwanamke alienda kwa mtume, na kumuleleza mtume ya kuwa wanaume wamepewa vitu vyenye kuwafanya wapate fadhila nyingi sana, kama vile kupigana jihadi na mfano wake, mtume akamwambia mwanamke yule ya kuwa "Mwanamke atakae tulizana nyumbani kwake miongoni mwenu basi huyo atalipwa ujira na yule mwanaume anae pigana jihadi.

Hii ni kutokana na fadhila nyingi apatazo mwanamke akitulizana nyumbani, ikapelekea ya kuwa jambo la kutoka kwake nje ni mpaka iwepo haja kubwa saa, na hii ndiyo dharura yenyewe sasa.

Kadhalika mwanamke anapata fadhila kubwa akisalia nyumbani, na ndiyo maana mtume akabainisha ya kuwa tusiwakataze Wake zetu kwenda msikitini endapo wakiomba ruhusa hiyo, hii ni kuonyesha ya kuwa Mwanamke mahala pake ni nyumbani na kutoka kwake ni dharura, yaani kwa haja na si vinginevyo.


Sasa unapokuja kupinga jambo, basi uje ushahidi toka katika aya na hadithi au japo kauli za wanazuoni juu ya hoja yako.
 
Utumwa siyo asili mzee, usichanganye mambo. Hizo ada za watu kwa watu wengine.
Nimekuambia asili ya waafrika ama watu wengi weusi huko kwa watu weupe ni utumwa.

Sijasema kuwa utumwa ni asili.angalia maneno yangu vizuri,sizungumzii utumwa kama utumwa,nazungumzia utumwa kwa watu maalumu.

Kwa maana kuwa watu weusi asili ya kuanza kuenea kwao huko kwa watu weupe ilikuwa ni utumwa.

Utumwa inaingia katika sababu za watu weusi kuwa wapo huko,kwa maana yake kuwa asili ya hao weusi walikuwa watumwa ndio maana wakapatikana huko arabuni ama uzunguni.


Hizo ada za watu kwa watu wengine.
Sasa hii kauli ndo unakubaliana na mimi kuwa jambo linaweza kuwa ada kwa wengine na kwa wengine isiwe ada pia,niliwahi kusema huko juu nakumbuka.

ada za watu kwa watu wengine.
Hii ada huwezi kuitoa katika asili.

Mfano waarabu walikuwa na ada ya kuwafanya watumwa baadhi ya watu weusi.

Utakataa vipi kuwa asili ya waarabu ilikuwa ni kuwafanya baadhi ya watu weusi watumwa ?

Kama ada ya watanzania ni kuwa mwanamke ndo anapika.
Utakataa vipi ukiambiwa kuwa asili ya watanzania mwanamke ndo huwa anapika ?

Unakataaje ndugu kati ya ada na asili ?

Ada na asili ya watanzania wa kusini ni kupeleka jando ama unyago watoto wao wakikua.

Hii ni ada lakini pia ndio asili ya hao watu.huwezi kukataa katika hili,ni maneno tofauti yanayokaribiana maana
 
Hii ada huwezi kuitoa katika asili.
Sasa siwezi vipi wakati umeshindwa kuiweka kwenye asili ?

Soma maneno yako huku ukiwa unatafakari.
Ada na asili ya watanzania wa kusini ni kupeleka jando ama unyago watoto wao wakikua.
Hivi huoni unavyilazimisha mambo mpaka unayaunga maneno mawili yasiyo kaa pamoja ili ukidhi maana yako. Hayakai hapo maneno hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…