Swali kwa Wanawake wa kileo: Nini kilichowatoa majumbani na kuanza kuingia mitaani na maofisini kutafuta hela?

Hapa ndipo nawashangaa ina maana wanaume hamuoni siku hizi mnakimbilia kwa wingi kuitwa ma aunt. Ama kweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Hawa mashoga waliojaa mijini ni vyombo vya starehe pia na vivutio.

Kila jinsia ipambane na hali yake
wanawake ni wengi sana wanaotembezwa uchi,kuliko hao ma aunt.....ukiona baya unatakiwa kulisemea sio kutetea maovu wewe...hata kama sio jinsia yako.
 
Hapa ndipo nawashangaa ina maana wanaume hamuoni siku hizi mnakimbilia kwa wingi kuitwa ma aunt. Ama kweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Hawa mashoga waliojaa mijini ni vyombo vya starehe pia na vivutio.

Kila jinsia ipambane na hali yake
😀😀😀😀 Sawasawa kabisa....

Nimefanya kautafiti kasiko rasmi nimegundua kuwa humu mitaani hasa jijini dar..kuanzia uswazi Mpaka pande za Kichangachui Masaki,kumejaa boys na young men wenzetu wenye vitabia vya MCHELEMCHELE....

Nimemkumbuka mama mmmoja mtu mzima Raia wa US alipata kusema kuwa SIKU HIZI BAADHI YA MEN wanavaa visuruali vya njano na Pink....Mimi nikaenda mbali KIFIKRA kuwa unaweza kumkuta mwanamume timamu kabisa,lakini akawa na ROHO YA NJANO na PINK kufikia kuwazodoa wanawake Kama afanyavyo ndugu Jurjani.....
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la wanawake kutafuta rizki,kusoma,kuolewa,kumiliki mali ni haki ya msingi kama binaadamu,tatizo linakuja pale wanapotumiwa na kudhalilishwa pasipo watetezi wao kupaza sauti na kukemea unyama unaofanywa wa kumtumia mwanamke kama kivutio cha anasa mbalimbali..........huku akiachwa bila stara,utu na heshma yake.
 
Sawa.Je Katika harakati hizo HAKUNA wasiodhalilishwa usemavyo?!! Na kwa upande wa wanaume,hakuna wanaodhalilishwa na kujidhalilisha mikononi mwa baadhi ya wanawake na baadhi ya wanaume wenzao?!!!
 
Nilitamani nisome tu bila kuchangia ila hapa pamenipa swali.

"Kuwa chini ya mtu au kuwa chini ya mwanaume" inamaanisha nini?
 
Ss mtoto akiwa shule nyumbani unakaa nyumbani unalea nini?
Kuna shida kwani Mama kwenda kazini na mtoto kwenda shule ?

Malezi ni pamoja na kumvisha nguo asubuhi na kumlisha ndio...ama asubuhi huwa mnafanyaje?

malezi ni ya wazazi wote wawili na ni ya muda wote ila haikuzuiii kujishughulisha..ama akina baba huwa hamlei watoto wenu?.
 
D
Duuh msumari mkali kwetu wanaume.....

Really Alpha Males are not the followers of what Jurjani advocating here....
 
Mawazo mgando gani?
huoni kama mnamezeshwa sumu kwenye mambo ya kipuuzi,kuliko mambo yanayowadhalilisha utu wenu,asilimia kubwa ya wanawake wanatumika kama kivutio cha mambo mbalimbali bila kujua kama wanadhalilishwa.


Mfano?
 
Nilitamani nisome tu bila kuchangia ila hapa pamenipa swali.

"Kuwa chini ya mtu au kuwa chini ya mwanaume" inamaanisha nini?
Ina maanisha kusimamiwa kwa hali zote.
 
Kati ya Uzi ambao umesimama huuu kwakweli wanawake wengi hawajitambui wamefanywa bidhaa bila kujijua wanawake wengi wanatumika kama bidhaa kuhakikisha maendeleo yanapatikana lkn lengo ni kuiharibu dunia!
 
Nikipiga simu leo katika mtandao fulani ikiwa haipatikani au mfano wake, huwa unasikia sauti ya nani ? Jinsia ya kike au ya kiume. ? Ulishawahi kujiuliza kwanini hili limekuwa sana ? Au walio fanya hivyi wajinga hawana akili ?

Sehemu nyingi za starehe, kuna yale mambo yenu ya ofa kwa wanawake, huwa wanaita "Ladies Free" ?

Mnatumika kwenye matangazo ya biashara. Suala la ulimbwende (Umiss) kuna tija gani zaidi ya kudhalilishwa na hampigi kelele, sasa mbona mnajitia upofu hali mmepwa macho ? Mwalimu wenu aliwaona nyinyi wajinga tangu siku ya kwanza, ndiyo maana anawafanya mnavyotaka na mnaona sawa, ila tukiwaambia mrudi kwenye asili mna rauka rauka.

Nani miongoni mwa wakubwa wenu aliwahi kutoka kifua mbele na kukemea mwanamke kujiuza kama bidhai, zaidi ya watu wa Dini ?

Mwanamke hakuwahi kuwa dhalili kama kipindi hiki, mwenye akili anaona na anazingatia.

Mwanamke mtu bora sana kiasili na nafasi yake ni kubwa mno, ila siyo wanawake nyinyi ambao hamjui kipi kina wadhuru na kipi kinawanufaisha.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…