Hakuna masuala ya kurogwa kwanza!
Halafu kingine wanawake ni rahisi kuolewa sana kwa tamaduni za kiafrika hususani hapa Tanzania ,ukiona mwanamke haolewa basi 80% yeye ndo chanzo .
Kwa sababu ni ukweli kwamba wanawake wengi wanaanza kutongozwa mapema mno tena na idadi kubwa wa wanaume ,kati ya hao wapo wahuni wanaotakq kuwachezea na wapo watu wa kweli ...kwa nn kuna watu kweli ndo maana kuna wanawake wanaolewa mapema hata umri wa miaka 18 na wapenzi wao wa kwanza .
Mwanamke kutokuolewa anataka mwenyewe kwa sabab nyingine 👉 Ana-maintain standard ili kupata anayemtaka japo anapigiwa miruzi sana ila hapa ana kuwa na akili zake kwa anayemtaka ,kama ana akili za kitoto atachelewa sana kupata handsome ..
Mwanamke ana nguvu ya kushawishi hata kwa acting sema wengi akili za utoto ,anaweza kutulia akawa na heshima ,uvaaji mzuri na tabia zinazopendeza.
Mwanamke ni rahisi kuolewa kwa kufanya vitu kadhaa tu basi ili kumvutia mwanamke kweny ishu za ndoa wala hamna mambo ya kichawi ila wanaume ndo balaa lazima uwe na uwezo wq kuhudumu familia yaani "fedha" ,ajabu ya kaisha unaweza kusota mpaka unazeeka haupati hata kazi ya maana kula yako tu mtihani.