LOOOoooh!
Mzee Mwanakijiji, hili swali mbona umeliacha linaelea lenyewe hivi?
Mimi nitaongeza kwamba, kila sehemu ya nchi yetu inafaa kuunganishwa kwenye SGR, lakini natambua uwezekano huo haupo kwa sasa.
Tanga (mkoa/mji) iunganishwe kutoka/kwenda wapi, kwa mfano?
Ungetaka nijibu swali hili, ninge kwambia Toka Bandari ya Tanga hadi Musoma
Nikiwa bado sijui madhumuni ya hoja yako, umenikumbusha jambo ambalo hadi leo sielewi lilianzia wapi.
Huu mradi wa barabara itokayo Malindi, Kilifi , Kenya, inaambaa ambaa kando kando ya bahari hadi Tanga na kushuka kwenda hadi Bagamoyo. Hii barabara tayari ilisha anza kujengwa na mkopo toka AfDB ulisha kubaliwa.
Hii barabara ni nani hasa aliitaka sana?