Nitaeleza chache ya hizo ambazo sikuridhika nazo kama mifano.
Wakati maeneo mengine ya nchi hakuna miundo mbinu inayotuunganisha na nchi jirani;
Nimekuuliza ni eneo gani tulitazame! tusiongelee jumla tuwe specific kama Mombasa-Tanga
Hii 'Master plan' ya EAC ni nani hasa anaibuni, maana inaonyesha wazi kuwa hiyo barabara ni mpango ulio buniwa kufurahisha baadhi ya watu tu! Ushirika wetu huu wa Afrika Mashariki, ushindwe kujuwa ni wapi palipo na uhitaji zaidi wa miundo mbinu kufanikisha ushirika itazame tu mradi ambao ni 'redundant' kama huu?
Mradi umeandikiwa ''proposal' kisha ukafanyiwa analysis na ndipo pesa zikatoka kwa wahisani
Si suala la EAC pekee. Sijui kama umefika na kuona faida za barabara kati ya Namanga-Holili
hata ukichukulia Kenya yenyewe na Uganda, ambao wana mpaka mrefu kati yao. Sehemu za kuingiliana kuu ni mbili.
Uhitaji wa miundo mbinu kati yao ni mkubwa sana, hasa ukichukulia kwamba biashara kati ya nchi hizo ni kubwa zaidi kati yao, kushinda ilivyo huku kwetu!
Biashara kati ya Uganda na Kenya ni ndogo kuliko Kenya-Tanzania. Ni ukweli nitakuletea takwimu
Uganda-Kenya wana mradi wa EAC unaojulikana kama North corridor, unaufahamu!
"Trade partner" ambaye siku zote yeye anafaidika zaidi na soko kwetu kuliko tunavyo faidika na soko kwake? Tunauza mali zetu nyingi zaidi nchi zingine kuliko tunavyouza Kenya, miaka yote. Na partner huyu haishi ulalamishi na kuweka vikwazo juu ya bidhaa zetu, huku yeye akitaka kufaidika zaidi na soko letu! Yeye anapenda sana kuchukuwa malighafi hapa, kama ngozi, pamba, mahindi alizeti, n.k., ili sisi tukanunue biskuti kwake
Biashara imegeuka, Tanzania ina export zaidi Kenya kuliko ilivyokuwa.
Kasome gazeti la EA, Kenya wame opt kuelekea DRC.
Soko la Kenya ni la kwetu lakini ujinga unatuanguasha.Sisi tulitakiwa tuwe '' food basket' ya Kenya kwasababu ya arable land. Tuna madini kama Kioo ambayo tulitakiwa tuwe na viwanda kuongeza thamani! hatuna! Tunanunua biskuti kwasababu sisi ni 'stupid'
Kwa nini tushikiliwe na 'trade partner' wa namna hii huku tukipoteza nguvu zetu za kuendeleza hawa 'partner' wengine wengi wanao tuzunguka?
Kwani ni partner gani tuliyemuacha? Ni lazima katika uchumi tuwe ''strategic' .
Burundi na Rwanda zina population ya 30 Milion. Kenya ina 50M na uchumi mkubwa kuliko Burundi au Malawi.
Msumbiji hawafanyi biashara kubwa na sisi wame 'base' zaidi SADC kama mkakati wao.
Malawi hakuna shida ya kufikika. DRC Kuna SGR tena inaingia Burundi na Rwanda.
Tatizo liko wapi?
Tuweke juhudi; tutumie hicho kidogo kilichopo kuendeleza u-'partner' wetu na hawa ambao tumewasahau siku nyingi.
Partner wapi hao? Mbona huwataji tuwajadili!
Mombasa na Tanga tayari zimeunganishwa. Kuna barabara nzuri tu toka siku nyingi.
Tunachosema hapa ni Tanga-Bagamoyo! ambako kuna 'interest' zetu si Tanga-Mombasa.
Na Tanga- Bagamoyo ndipo hoja yangu ilipo, kwamba, hatuna sababu ya kusafiri kwa ''square' yaani Tanga-Segera-Chalinze-Dar! ni upotevu wa rasilimali na muda. Masaa 2 yanatosha Tanga-Bagamoyo
Fursa ya Burundi kutumia bandari ya Mombasa kwa kupitia kwenye barabara zetu, lakini tusione fursa ya Burundi kutumia bandari zetu za Tanga na Dar es Salaam?
Well, Burundi wanatumia kwasababu sisi ni 'stupid''. Bandarizilipaswa kuwapa incentive, kila siku tunabadili mameneja. Tumeshindwa kuendesha shirika la Reli, usiwalaumu tujilaumu
Hili swala la utalii, kwani watalii hawawezi kuja Tanzania bila kwenda Kenya? Ukiniuliza mimi nitakwambia kwamba Tanzania ndiyo inayo tumika kuinufaisha Kenya katika swala hilo, na ndiyo maana wanalilia sana hiyo 'visa' ya pamoja; na ndiyo maana Mlima Kilimanjaro ulikuwa Kenya zaidi ya Tanzania, hali kadhalika Serengeti ipo kuiinua Maasai Mara!
Hapana! kuna kutegemeana. Nenda Kenyatta Inter Airport utaona jinsi ndege zinavyotoka mataifa duniani zikileta Watalii. Again, ni ujinga wetu tulikuwa na akina PIA, AEROFLOTA, SAS, Luftansa, France, BA , Ethipoia, Egypt, n.k. Jiulize kwanini ziliacha kuja kwa muda mrefu zikaendelea Nairobi.
Tunategemea sana soko la utalii la Kenya lakini ni kwa ujinga wetu
Hilo la nchi kushindwa kuwa na miundombinu na kulazimika kutumia ya nchi zingine ili uweze kuyafikia maeneo yaliyomo nchini mwako ni aibu isiyofaa kusimulia hata kidogo.
Yes ilikuwa ni aibu na Kenya walitumia fursa
Na kumbuka, wakati hayo yanatokea, miundo mbinu kati ya nchi hizi jirani ilikuwa mizuri tayari. Nani aliyekuwa akifanya hujuma ya nchi kuwa katika hali mbovu kiasi hicho!!
Hapana, Barabara ya Dar-Mwanza ilikuwa haipitiki.
Hata KAMATA ililazimika kupitia Kenya.Niliyaona kwa macho yangu
Sasa mpango ni huo huo wa kuendelea kutushikilia tusitazame majirani zetu wengin na hata baadhi ya maeneo yetu wenyewe ndani ya nchi, lakini tuwe na barabara za ziada za kutufikisha nchi jirani?
Hayo majiji yaliyopo huko, huku kwingine hayapo? Biashara haiwezi kuwa sehemu moja tu, biashara ipo kila mahali, kazi iliyopo ni kuitafuta tu na kuistawisha kwa uwepo wa miundo mbinu mizuri. .
Kuna hoja yako 'imejificha' lakini nitakueleza. Hapa JF kuna uzi ukionyesha takwimu za BoT.
Mikoa ya kaskazini iliongoza sikumbuki vizuri nadhani kwa miezi 3 ikichangia Trilions katika pato la Taifa.
Daraja lilipovunjika pale Chalinze-Goba JK alisema '' anapeleka jeshi' kwasababu ile barabara ni ''life line of the economy'. Nina maana kwamba shughuli za uchumi ni hesababu si ku-balance kipi kiende wapi.
Trilioni zilizoingia BoT zinatakiwa zijenga Barabara ya Mtwara-Songea yenye faida sana kiuchumi.
Pesa zinazopatikana kwa shughuli za uchumi 'mikoa na nchi jirani'' zitumike kujenga barabara ya Tanga-Dodoma. Ni wendawazimu kuzunguka Tanga-Sgera- Chalinze-Morogoro-Dodoma.
Ni wendawazimu kusafiri Arusha-Kilimanjaro-Segera-Chalinze- Morogoro. Tayari kuna barabara kuanzia Korogwe- Handeni-Kilosa-Morogoro. Iwekwe lami tukikusanya pesa za 'Mikoa na jirani''
Ni wendawazimu mtu kwenda Dar-Lindi-Mtwara akitoka bara.
Ijengwe Barabara ya kupitia JNHPP kuanzia Chalinze ili kupunguza muda wa kusafiri na gharama zitokanazo
Nakubaliana na PPP kujenga barabara ya kulipia. Pesa zitakwenda kujenga miundo mbinu kunakohitajika.
Ukinishawishi Reli ya Mtwara-Songea nakubaliana nawe 100% kwasababu ina manufaa kiuchumi si kwasababu tunataka mikoa hiyo nayo iwe na reli.
Kuna uhitaji mkubwa sana kwa Tanzania kustawisha uhusiano wa kibiashara na majirani zake, Uganda, DRC, Zambia na hata Msumbiji.
Kimekosekana nini kwa majirani hawa! kwa miundo mbinu?
Kuendelea kusisitiza biashara kati ya Kenya na Tanzania, biashara ambayo matokeo yake ni hafifu sana ni kupoteza muda na fursa.
Biashara ya Tanzania-Kenya ni kubwa kuliko biashara ya jirani mwingine! huu ni ukweli wa wazi.
Unaweza kuwa na 'reservations' zingine lakini haziondoi ukweli
Nipe data ni nchi gani kati ya 8 tunazopakana nazo yenye biashara kubwa na sisi kuliko Kenya.
Katika EAC Kenya ni super power, sasa unakwenda ku trade na Burundi ili iweje
Sioni sababu hata moja ya Tanzania kutokuwa na biashara kubwa kati yake na DRC; lakini nguvu kubwa zinatumika Kenya,
DRC si kuna SGR hadi Msongati! kuna TAZARA kuna usafiri wa Ziwa Tanganyika, kuna Barabara ya Kigoma.
Unataka kipi tusichokiona wenzako!
Bahati nzuri iliyo nayo Tanzania, tofauti kabisa na Uganda; haina utegemezi wowote wa maana kwa hiyo nchi jirani. Tanzania inao uwezo wa kuendesha mambo yake yote bila ya kuitegemea Kenya. Ingekuwa vinginevyo, tunge lizwa sana, kama Uganda wasivyoisha kunyanyaswa.
Hata US inaweza kuendesha mambo yake bila kutegemea Taifa lolote lakini ukweli unabaki pale pale uchumi ni kitu 'intertwining' kwamba huwezi kuwa na uchumi wako.
Tunategeana sana na Kenya na napenda sana kwasababu Kenya wanatoa challenge! Ndio maana tunalazimika kufikiriData za BoT zinathibitisha umuhimu wa biashara na Kenya
Unaweza ''kuwa na concerns'' na Kenya na Mikoa jirani, hilo haliwezi kufuta ukweli wa takwimu za uchumi.