Silent Sinner
Member
- Oct 28, 2012
- 13
- 0
"when the wind blows, the grass bends." Master Confucius
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unaamini katika uumbaji?
Talking about the heart and feelings.
Kwakuwa natumia simu nashindwa ku-paste link moja kwa moja ila nenda ka-search "follow your heart finally science agrees with us"
halafu angalia kuna greg braden na bruce lipton wametajwa mwisho kabisa, nenda kawaangalie you tube.
Mi namfahamu Greg siku nyingi tu.
Siamini katika kuamini. Unaelewa significance ya kauli hii?
Siamini katika kuamini chochote.
Naweza kugoogle sasa hivi rankings za page zikawa zimebadilika nikaona kitu tofauti.
Weka link. Taja journal. Hata The Flat Earth Society wana website.
kama wewe uamini katika kuamini,unaamini katika nini?
kama wewe uamini katika kuamini,unaamini katika nini?
Kama wewe hupendi rangi unapenda rangi gani?
Soma post #25
Hapa https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/358932-swali-la-kizushi-kwa-kiranga-2.html#post5100683
Ngoja nikurahisishie hilo neno kuamini halipo kwenye kamusi yake
okay ata kama sipendi rangi lakini haiondoi ukweli kwamba rangi zipo..sasa ata wewe ata kama uamini katika kuamini lakini unakubali imani ipo na kutokubali kuamini ndio imani yako.wewe ni muumini wa kutokuamini..Mungu ajalibiwi Kiranga,akiamua umpe imani kamili kiranga chote kitakuisha.
Hata kama Santa Claus hayupo, na wewe huamini kwamba Santa Claus yupo, lakini unakubali kwamba imani ya kwamba Santa Claus yupo ipo, na wewe kutoamini Santa Claus ndo kuamini kwako.
Umesoma post number 25? Umeielewa?
post yako nambari 25 nimeisoma..ila imejaa contradictions..ni kama hapa unavyosema huamini imani ila unakubali imani ipo,lakini bado unarudi kusema imani yako ni kutoamini..
Sasa ebu nikuulize kitu, ni kitu gani/nini kinacho control ulimwengu??
Post umeisoma ila hujaielewa.
In a nutshell nimesema sitaki kuamini, nataka kujua.Lakini kuamini hakuepukiki kwa sababu hata ukikanyaga hatua moja unakanyaga kwa imani (imani kwamba macho yako hayakudanganyi na unapokanyaga pako firm) kwa hiyo mtu atakayekwambia haamini chochote bila ku qualify hiyo statement ama hana uelewa mpana ama muongo tu.
Ukweli kwamba imani haiepukiki haumaanishi tutumie imani hata pale inapoepukika.
Kuna dini fulani ya wahindi mostly, inaitwa Jainism. Jainism ni dini ya non-violence. Wao hawaamini hata kuua sisimizi. Na ukimkuta a devout Jainist anataka kutembea huko vijijini India unaweza kutaka kucheka kama huwaelewi, maana kama njia ina siafu na hamna pengine pa kupita wako radhi kwenda polepole wakiwafagia siafu /sisimizi taratibu ili mradi wasiwakanyage tu.
Hawaamini katika kuua kiumbe chochote.
Je hilo lina maana hawaui kiumbe chochote? Hasha. Hawawezi kufagia kila kiumbe. Wanaua sisimizi wengine bila kupenda.
Lakini wanafanya jitihada zote kuhakikisha kwamba hawaui pale inapowezekana wasiue.
Same thing applies with me and belief. Ninapoamka asubuhi nakanyaga sakafu kwa imani, ni a ridiculously low level of belief because this process has been tested over and over again experimentally. But there is no way of telling kwamba kesho the laws of physics wont change, or an earthquake will hit my house just as I am stepping down from my bed, or my floor will otherwise collapse. So for this reason I have to go by faith that the floor will hold.
But there are things that I do not have to go by faith. Things that could be verified and weighed within reason.
Ukiuliza "ni kitu gani/ nini kinacho control ulimwengu" unafanya assumption kwamba ulimwengu uko controlled.
Kwa nini unafikiri ulimwengu uko under control? Unaposema kitu gani kinacho control ulimwengu unaongelea control gani specifically?
Kama ulimwengu uko under control, kwa nini inakubidi ufagie ili uchafu usizidi? Kwa nini inakubidi ujaze mafuta kwenye gari ili liweze kwenda? Kwa nini inakubidi kula ili usife kwa njaa? Kwa nini unazeeka? Kwa nini unakufa?
Is this the control you are talking about?
ulimwengu uko controlled na Mungu muumba wa vyote..yeye ndio ana control kila kitu..ana control jua na mvua..usiku na mchana..mwanga na giza..leo na kesho..wanaadamu wote(ata nyinyi wapagani mnaomchukia)..viumbe vyote..mbingu na ardhi..
'Umeuliza kwa nini nafikiri ulimwengu uko controlled'..sababu ipo wazi hakuna makosa makosa yanayofanyika,kila kitu kipo kwenye mpangilio..kuanzia uumbaji hadi mzunguko wa dunia..na inapotokea tatizo ni mipango yake Muumba..jua alikuchi saa mbili usiku wala binadamu hazaliwi na mapembe..nani yuko nyuma ya yote aya???ni Mungu ambaye anakupenda ata wewe ndio maana anakuyumbisha kwenye iman ili siku utaporudisha iman kamili hautayumba tena kamwe na utatangaza sifa na zake na utukufu..amekujalia akili ya kutambua mema na mabaya,akili ya kutambua huu ni uchafu haufai kukaa karibu na makazi ya watu..akili ya kutengeneza usafiri wa kurahisisha safari na kutafuta mafuta ya kuendeshea huo usafiri..akili ya kutafuta chakula..na pindi utapokamilisha utukufu wake atakuchukua na kuwapa nafasi wengine waendeleze utukufu.
Ndio maana ata hao wanasayansi wamekosa majibu ya chanzo cha ulimwengu japo wameangaika sana..ata vitu kama 'giza' vimewashinda kuprove uwepo wake
Kiranga nakumbuka
uliwahi kusema hapa jf kwamba umeoa.
Je, mliona aina gani ya ndoa?, mke wako anaamini dini gani?
Unaweza acha kujibu If it's too personal.
Hakuna makosa makosa yanayofanyika?
Kwa nini tetemeko la ardhi limetokea Haiti na kuua watoto wasio na hatia?
Kwa nini watu wengine wanazaliwa viziwi, wengine vipofu, wengine viziwi na vipofu?
Mungu mwenye uwezo wote na upendo wote atawezaje kuachia mabaya yatokee duniani wakati yeye ndiye ana control yote?
Ana uwezo wa kuondoa mabaya yote haya lakini hajali tu?
Au anajali lakini hana uwezo?
Hawezi kuwa anajali na ana uwezo akaacha yaendelee.