Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Kichuguu FRANC THE GREAT Drifter
 
Hivi mkuu maswali yangu huyaoni? Au unaona sistahili kujibiwa. Maana naona unakazana kuuliza ila kujibu hutaki.
Kabla sijajibu maswali yako ya ziada kwanza jibu maswali yangu kisha tuendelee. Au kama huyaoni, nijulishe nitayapanga kwa namba kama unavyofanya
 
Mada ya uchumi na propaganda za kivita wapi na wapi.

Watu wengine bana yaani mtu na akili zako timamu Russia imepoteza kuliko Ukraine.

Wacha wajuvi watufundishe kuhusu uchumi, haya ya sijui kashindwa tutakuja kuyajua mwisho wa vita.
 
Mkuu data zipi zinaonyesha Russia kapoteza vifaa vingi na wanajeshi wengi kuliko Ukrein?.

Mkuu The Boy Wonder suali lake lamsingi ni je wakiinforce hivyo vikawazo bila huruma Kwa Moscow wao uchumi wao utabaki salama?.
cc Max II Jr kp kipanya44
Ukraine war, already with up to 354,000 casualties, likely to last past 2023 - U.S. documents

Data za Reuters na Al Jazeera zinathibitisha Hilo kwamba Russi imepoteza sio tu askari wengi zaidi Bali pia Tanks na drones zilizodunguliwa. If that wasn't the case wangeshateka kyiv zamani Sana.

2. Mkuu kwenye vita whether ushinde au ushindwe madhara ya kiuchumi hayaeupikiki. Tanzania hapa tulimpiga Idd Amina ila tulipoteza nguvu ya kiuchumi. So uchumi utayumba kwa kiasi chake kwa multiplier effects ila madhara ya kijeshi in case of Nuclear holocaust yanazidi faida za kuimaliza Russia!!
 
Mada ya uchumi na propaganda za kivita wapi na wapi.

Watu wengine bana yaani mtu na akili zako timamu Russia imepoteza kuliko Ukraine.

Wacha wajuvi watufundishe kuhusu uchumi, haya ya sijui kashindwa tutakuja kuyajua mwisho wa vita.
Ukraine war, already with up to 354,000 casualties, likely to last past 2023 - U.S. documents

Reuters and Al Jazeera have reported that

Kingine kama Russia hajapoteza askari wengi si angeshakua ameshinda vita?

Kama issue ni uchumi tumeshaeleza huko juu kwamba Russia Ina sustain vita sababu nchi zinakiuka masharti ya vikwazo ila kama zingeheshimu vikwazo Russia Hana ubavu wa kusurvive hata miezi 6 maana ana GDP mdogo mnoo
 
nchi gani ikipigwa vikwazo ita-survive?
US?
China?
EU?

kifupi, vikwazo alivyopigwa Russia ingepigwa EU leo tusingekua na eu,
Issue sio vikwazo issue ni ku enforce vikwazo Sasa Russia kawekewa vikwazo ila Bado anafanya Yale Yale aliyowekewa zuio. Ila mfano Venezuela ikiwekewa vikwazo unakuta nchi zinaufyata kufanya biashara naye ndio maana inaathirika.

Sanctions without enforcement are futile and obsolete.

So swali lako lingekuwa " nchi Gani ikiwekewa vikwazo na ikalazimishwa kutii ita survive"

EU inaweza survive
China inaweza survive
But Russia cannot survive if isolated completely due to weak economy
 
Hata NATO ikaamua kumpa full support ya zana za kijeshi Russia, sidhani kama itachukua wiki Russia kutapika maeneo aliyoteka.

NATO imeona mbali uwezekano wa matumizi ya Nuclear ktk hii vita, hii wanafanya waende step kwa step hapo Ukraine.

Tukumbuke walipotenga bajeti ya miaka mitano kuisaidia Ukraine, watu waliwaona NATO kama wehu, waliona ukubwa wa Jeshi la Russia dhidi ya Ukraine basi vita isingechukua hata miezi mitatu.
 
Na endapo Russia kungekuwa na uhuru wa vyombo vya habari, tungesikia mengi juu ya uchumi wa Russia.
 
Anayeisaidia Russia kupata nfuu za kiuchumi ni Uchina tu,pamoja na vikwazo ulivyosema China imeendelea kuwa karibu na Russia kibiashara na kiuchumi I'll kuipa nafuu za vikwazo.
India pia inanunua mafuta mengi sana toka Russia.
 
Ungeanza kunijibu maswali yangu mwanzo kabisa na kitaalamu kama anavyofanya bwana zitto junior ningetoa majawabu ya kila swali ulilouliza. Ila bahati mbaya hujafanya hivyo zaidi ya kuzunguka mbuyu na kuchanganya mambo. Nadhani mimi na wewe tuishie hapa, niendelea kufanya mjadala na Zitto Jr ambaye ni mchumi aliyesomea.
 
Anayeisaidia Russia kupata nfuu za kiuchumi ni Uchina tu,pamoja na vikwazo ulivyosema China imeendelea kuwa karibu na Russia kibiashara na kiuchumi I'll kuipa nafuu za vikwazo.
India pia inanunua mafuta mengi sana toka Russia.
Mbona Ulaya na Marekani wananunua bado rasilimali muhimu kutoka Urusi na kuendelea kuwekeza nchini humo, kama ambavyo Uchina na India wanafanya. AU haya ninyi wataalamu wetu hamyaoni jamani, ???

Takwimu za UN zinasema kwamba, Urusi na Ukraine kwa pamoja ndiyo wauzaji wakubwa wa mazao ya chakula. Wanaendelea kusema kwamba asilimia 44% ya nafaka kutoka bahari nyeusi imeenda kwa wateja ambao ni mataifa makubwa ya Ulaya na Asia (High Income Countries).

Juzi Urusi katijoa kwenye The Black Sea Grain Deal, na angalia nini kimetokea. Takwimu za masoko ya dunia zinasema baada ya Urusi kujitoa tu kwenye huo makakati hapo majuzi, bei ya nafaka imepanda kwa asilimia 3% nzima ambayo ni sawa na senti 689.25 kwa kibaba kimoja (689.25 Per Bushel). Hii inamaanisha bei ya chakula itapanda sana na kuchochea mfumuko wa bei (Food Price Inflation) kule Ulaya na sehemu nyingine duniani.

Hapa hata upandishe riba juu (Hiking Interest Rates) kiasi gani ili kupambana na mfumuko wa bei, huwezi kufanikiwa. Njia rahisi ya kudhibiti mfumuko wa bei itakuwa ni kutafuta rasilimali, na siyo zenye uhaba na kuziingiza kwenye soko. Fedha zitapoteza thamani na nguvu ya manunuzi itaisha.

Hili nimemwambia ndugu yangu zitto junior , ila yeye anaamini kwamba huu utajiri wa vitu visivyoonekana (Imaginary/ Incorporeal wealth) ndiyo njia sahihi ya kupata taswira halisi ya uchumi wa nchi. Binafsi hili linanipa ukakasi, kwasababu tokea karne za 17 tulitumia vyote, (Utajiri unaoonekana na Utajiri usioonekana) kupima taswira ya utajiri na uchumi wa nchi.

Sasa narudia maswali yangu, tena;

Mosi, imekuwaje taifa ambalo ni asilimia 4% ya Uchumi wa dunia isababishe mfumuko mkubwa wa bei ya chakula kwenye soko la dunia hadi kuathiri nchi tajiri za G7 ambazo zinamiliki asilimia 37.7% ya uchumi wa dunia, ???

Pili, Je dunia na wachumi walikuwa sahihi kuacha kuangalia utajiri wa nchi kwa kurunzi ya Finance Economy peke yake bila kuzingatia Commodity Economy, ???
 
Itakua vp km maswal yako wakishindwa kuyajibu???
 
Hapa wengi naona tunashindwa kukubaliana kwamba wewe mwenye milioni(pesa) ndani ili uile(uitumie) lazima awepo mwenye mahindi ndani. So ni lazima kwanza yawepo mahindi ndo mwenye pesa anaweza kuishi na ndo kinachotokea kwa West vs Russia
 
naona unaongea usichokijua, acha nikuache nitamaliza nguvu zangu!
 
Hapa wengi naona tunashindwa kukubaliana kwamba wewe mwenye milioni(pesa) ndani ili uile(uitumie) lazima awepo mwenye mahindi ndani. So ni lazima kwanza yawepo mahindi ndo mwenye pesa anaweza kuishi na ndo kinachotokea kwa West vs Russia
kwa lugha rahisi hapo, tajiri ni mwenye mahindi (maana akipandisha bei au akigoma kuuza wewe mwenye milioni utahangaika sana kupata mbadala, au pengine ukipata itakua bei juu mno,

ndipo ile nadharia kwamba ulaya magharibi ni maskini (pengine kuliko afrika) inapoingia,..... leo tukisema kila mtu aishi kwa kutegemea alichonacho, basi wale wenzetu wanaweza kufa sana,

na hii ndiyo inayombeba Urusi, ana bidhaa ambazo ulaya wanazihitaji ili waendelee kuishi na uchumi wao usitetereke pakubwa,......
 
Mosi, imekuwaje taifa ambalo ni asilimia 4% ya Uchumi wa dunia isababishe mfumuko mkubwa wa bei ya chakula kwenye soko la dunia hadi kuathiri nchi tajiri za G7 ambazo zinamiliki asilimia 37.7% ya uchumi wa dunia, ???
Narudia Tena mkuu, uchumi sio zero sum game ndio maana ukipunguza ajira uchumi haukui ila pia ukiongeza ajira ghafla uchumi unaporomoka. Uchumi is all about kung'ata na kupuliza ndio maana broad money supply (Demand deposits+ Forex + Currency in circulation) huwa inapdandishwa na baada ya muda Fulani inapunguzwa (kwa kuuza au kununua hati fungani) ila ukisema uongeze Hela tu uchumi unakufa ila pia ukipunguza pesa kwa mzunguko uchumi unakufa.

Having said that unakosea pale ambapo unaonyesha kwamba uwepo wa vita ya Ukraine na Russia ndio hiyo inayopelekea inflation kupanda USA Au EU? Ulifanya hivyo lazima uweke control variables (We ni msomi unanielewa hapa) mfano macroeconomic variables kama floating interest rates (Moving average), unemployment rate, COVID 19 repurcussions, kuanguka kwa benki za USA, housing crisis, scarcity ya dollar kwenye soko la kimataifa, Sasa ukifanya test yoyote iwe Panel data au hata Pooled OLS lazima tu utaona jinsi Gani hizo factor zingine zinachangia zaidi uchumi wa EU au US uanguke na sio necessarily Kwa Russia kuzuia mauzo ya grains or whatever resources wanauza kwa EU au USA.

TLDR: You can't conclusively say factor Moja ya Russo-Ukranian War ndio directly inasababisha matatizo ya kiuchumi huko western Bloc bila controlling for other macroeconomic variables ambazo zilishaleta athari za kiuchumi since 2020.

Correlation is not causation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…