Bwana Armata nimeuliza maswali rahisi sana ambaya hata mtoto anayesoma shahada ya uchumi, sheria au siasa angeweza kuyajibu. Nilihitaji uchambuzi wa kiuchumi uliojaa takwimu, mahesabu na kanuni za kiuchumi. Bahati mbaya mno nimeona maelezo na maoni yako binafsi. Haina shida twende taratibu hivyohivyo.
Nashangaa mno kuona kwamba msomi kama wewe kutofahamu kwamba The Oil Embargo ni moja ya sababu kubwa iliyosababisha kutengeneza mfumo mpya wa uchumi wa dunia Bretton Woods II na kusababisha American-Asia Corporate Inversion mambo makuu yanayoigharimu Marekani mpaka leo.
Kama vitu rahisi hivi vimekupita wewe mchambuzi wa mambo ya siasa basi kuna tatizo kubwa pahala. Ila tuendelee taratibu hivihivi naamini tutaelewana huko mbele.
Bwana Armata nimeuliza swali rahisi sana. Nini kimepelekea mataifa ya G7 kupandisha riba za mabenki juu (Hiking Interest Rates). Unaweza pia hata kunitajia sababu za kwanini Urusi naye alipandisha riba za mabenki juu. Ntakushukuru kama utanipa majibu.
Umejibu vyema kabisa, lakini hapa napata maswali mengine matatu;
Swali la kwanza, hao Ulaya wanavyotafuta mbadala wa nishati ya Urusi watapambanaje na tatizo la mdororo wa uchumi ambalo limewakumbuka au hili tatizo litaondoka ndani ya usiku mmoja ?
Ifahamike takwimu za International Energy Agency (IEA) zinasema itachukua miaka isiyopungua kumi kwa Ulaya kuweza kupata mbadala wa nishati ya bei rahisi kama ya Urusi.
Swali la pili, gharama za uzalishaji zikipanda juu kwasababu ya ghaarama za nishati mbadala unadhani viwanda vitaendelea kufanya uzalishaji katika kiwango ambacho kilikuwepo kabla ya mwaka 2022, ???
Kumbuka kanuni za uchumi wa kibepari zinasema hivi, ili uweze kupata faida kwenye uzalishaji ni lazima uwe na nishati ya bei ndogo na malighafi za bei ndogo. Wanavyotafuta mbadala wa nishati ya Urusi wataendelea kuwa na nguvu kubwa ya uzalishaji ???
Swali la tatu, wanavyotumia gharama kubwa kutafuta mbadala wa nishati ya Urusi, bara la Ulaya watakabilianaje na tatizo la mfumuko wa bei (Energy Inflation), ???
Mwisho kabisa, ndiyo Urusi imeingia kwenye mdororo wa uchumi kwasababu ya vikwazo vikubwa kutoka mataifa ya G7 ambayo ndiyo yenye uchumi mkubwa duniani. Ila ambacho kinanishangaza ni kwanini mataifa yanayomiliki asilimia 30.7% ya uchumi wa dunia nayo yawe kwenye kundi moja na Urusi taifa ambalo ni asilimia 4% ya uchumi wa dunia. Huoni hapa kuna walakini ???
Bwana Armata majawabu yako yanazidi kunishangaza mno. Urusi siyo taifa lenye uchumi wa mitaji (Capital Market Driven Economy) kama Marekani. Marekani ndiyo taifa tajiri duniani kwasababu asilimia 34% ya soko la mitaji (Capital Markets) duniani linashikiliwa kwa fedha za kimarekani (Denominated in US Dollars). Hivyo Marekani ndiyo makao makuu ya masoko ya mitaji duniani.
Mabenki ya Urusi yakiwa mufilisi haileti madhara kwa dunia hata kidogo, lakini mabenki ya Marekani yakiwa mufilisi dunia nzima itaona madhara kwasababu yeye peke yake ndiyo mwenye soko kubwa la mitaji duniani ambalo karibia benki kuu (Central Banks) zote zinanunua bidhaa na huduma.
Deni la Marekani linamilikiwa (US Treasury Bills are held by foreign states) na mataifa ya nje kama Uchina kama mbinu ya kuyawezesha mataifa hayo yapate fedha za kimarekani kwa wingi kama mbinu ya uwekezaji, lakini pia kupunguza thamani ya fedha zao , jambo ambalo kiuchumi ni muhimu mno kwenye kufanikisha biashara ya kimataifa (China uses this economic technique of devaluating her local currency against the dollar in-order to boost exports)
Nilitegemea haya unayafahamu hivyo usingeleta mfano wa mabenki ya Urusi. lakini kwasababu hukuyafahamu basi nimekupa takwimu na sababu za kiuchumi kwanini umufilisi wa mabenki ya Urusi na Marekani uko tofauti. Mtu yoyote aliyesoma uchumi na kufahamu vizuri siasa za dunia hawezi kufanya huu ulinganifu.
Turudi kwenye swali letu la msingi: Nini kimepelekea mabenki 1000 ya Marekani yanayouza mitaji duniani kote kuwa mufilisi (Insolvent), ???
Uko sawa kabisa, Urusi hauzi nishati ya bure, lakini ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza nishati ya bei nafuu kwa nchi za Ulaya, Uchina na India. Uchumi wa viwanda wa Ujerumani una thamani ya dola za Kimarekani Trilioni 1, lakini unaendeshwa na nishati kutoka Urusi yenye thamani ya dola za kimarekani Bilioni 60 tu. Huo mbadala watakoupata hapa ni upi ndugu yangu ?
Kuhusu mkataba baina ya Uchina na Saudi Arabia nilitegemea ufahamu kwamba nishati inayotoka ghuba ya Uajemi kwenda Uchina husafirishwa kupita bahari hivyo ni gharama kwasababu ya muda, bima (Maritime Insurance) na upakiaji (Packaging). Gesi inayokuja kutoka Saudi Arabia kwenda Uchina ni LNG, ambayo ni gharama mno kuitengeneza. Ila pia kumbuka kampuni la bima kama LLYODS OF LONDON la Uingereza linachaji dola za kimarekani milioni 50 kwa mzigo mmoja wa majini.
Unadhani kuliko kutumia Trans-Siberian Pipeline ambayo husafirisha gesi kwa haraka bila ukomo, Uchina atajikita kabisa kwenye kutegemea mkataba wake na Saudi-Arabia ???
Bwana Armata nakushauri kama kaka, usijibu hivi tena mbele za watu. Yaani unapima soko la nchi husika kwa kuangalia manunuzi ya magari kweli. Unataka kusema leo hii Tanzania ikununua magari mengi kuliko Kenya basi soko letu ndiyo kubwa ???
Halafu kuichumi huwezi kulinganisha nguvu ya manunuzi (Purchasing Power) ya nchi mbili moja kwa moja. Inabidi uzingatie mambo kadhaa wa kadhaa, ndani ya nchi unazozifanyia uwiano. Wachumi wengi hutumia kipimo kiitwacho THE BIG MAC INDEX, kupima nguvu ya manunuzi baina ya nchi mbili (Purchasing Power Parity). Hili linafanyika kwasababu bei za vitu kwenye nchi mbalimbali zinatofautiana.
Bwana Armata wewe mwenzangu ulisomea wapi uchumi, mbona mambo unauliza mambo ambayo yanatutia wenzako ukakasi ? Tunarudi kulekule kama nilivyosema.
Marekani ana mengi ya kupoteza kuliko Urusi kwasababu yeye nchi yake ndiyo makao makuu ya soko la mtaji hapa duniani (The Epicenter of World's Capital Market). Uchumi wa Marekani unaendeshwa na udhibiti wa masoko ya hisa, riba, hati-fungani na uchapishwaji wa fedha. Urusi ana sehemu ndogo mno kwenye uchumi wa mitaji.
Riba zinapopandishwa juu bila mpangilio, wawekezaji wengi zikiwemo benki kuu za (Central Banks) duniani kote, na mashirika mengine hupoteza imani kwenye mfumo jambo ambalo linaweza kusababisha mtafaruku kwenye masoko (Market Volatility), kuanguka kwa mabenki, hata mitaji kuondoka nchini (Capital Flight) au hata mtikisiko wa uchumi wa dunia kama ilivyokuwa mwaka 2008.
Ewaah, swali langu liko hapa. Kwanini matajiri wa G7 hawajawekea vikwazo makampuni ya nishati ya nchi masikini kama Urusi, na kuamua kutumia fedha zao kupata nishati mbadala ???
Kama uchumi wa Urusi unaendeshwa kupitia gesi na mafuta, kwanini uweke vikwazo kwingineko kwenye sekta ambazo hazina madhara makubwa, lakini uache kuweka vikwazo kwenye sekta ambazo zinaipa Urusi nguvu ya kuendesha vita yake ya kivamizi na uchumi wake, ???
Aidha unachanganya watu makusudi, unakwepa swali au hufahamu kitu. Binafsi nimeuliza kuhusu soko la hati-fungani (Bond Market) na siyo soko la hisa (Stock Market). Wewe umejibu kana kwamba hivi vitu viwili ni kitu kimoja, jambo ambalo limenishangaza sana.
Ungefahamu utofauti uliopo baina ya haya masoko mawili, na jinsi yanavyofanya kazi kwenye uchumi wa dunia sidhani kama ungetoa hata mfano wa Urusi. Nimekuuliza kwanini soko la hati-fungani, ambao ndiyo uwekezaji unaoaminika zaidi kule Ulaya limeanguka ???
Hujanijibu kitaalamu, umezunguka mbuyu na kuleta siasa.
Mkuu, unafahamu nini maana ya Quantitative Easing (QE), ???
Mkuu, unazidi kuchanganya mambo. Binafsi sijazungumzia fedha ya Marekani kutumika kama EXCHANGE peke yake. Hayo umeyasema wewe. Binafsi nimeuliza kuhusu asilimia 55%-59% ya matumizi ya fedha ya Marekani as COMMODITY, STOREHOLDE OF WEALTH and A BEBT-INSTRUMENT not only as a MEANS OF EXCHANGE.
Ikumbukwe kiuchumi, mbali na kabla ya kufanya manunuzi dola ya Marekani ni bidhaa kama bidhaa nyingine ambazo Marekani inauza kwa nchi mbalimbali. Hivyo nilivyozungumzia asilimia 55% nilizungumzia hili.
Nadhani hili tuliache, kwasababu ulilijibu bila kulielewa vizuri.
NB: Binafsi naendelea kusubiri majawabu yako nijifunze zaidi mkuu....