EN ni 'insider'' anaijua CCM na alijua nini kinafuata. Alikuwa na habari zote! alikataa makusudi ili kusetiri uso wake siku zijazo!
EN hakutegemea Marafiki, alijifunza kutoka kwa Lowassa, Membe, Ndugai etc. Mahakamani kwa kesi gani? Uhaini!
Hili litakuwa kosa wakilifanya! EN ata spill out the beans. EN ni insider
Naam!
Nasikia eti EN aliitwa kwenye maadili hakwenda labda anakumbuka Horace Kolimba alipotoka kuhojiwa kwa kauli ya CCM imepoteza uelekeo kilichofuata ilikuwa sala ya Wafu
Mkuu 'Nguruvi', nimekuona kule kwingine, nikasita kuweka maoni yangu mepesi kwa hoja ulizoweka. Nikaamua nivute wakati kwanza.
Sasa naona hoja zilezile zimefika huku.
Pamoja na kwamba sina jibu, lakini nimeamua niache yanayoniijia akilini kwa kifupi.
Ninakubaliana nawe, kama kuna mtu anayeifahamu kwa ndani kabisa CCM, huyu ndiye hasa; hata Lowassa asingemfikia.
Tatizo langu hapa: Anaijuwa CCM ipi hasa; maana pamoja na mambo kadhaa mabaya yaliyowahi kufanyika huko miaka ya nyuma, haya yanayofanyika sasa hata hiyo CCM yenyewe ya wakati ule ingestuka. Nchimbi bado anaijuwa CCM ipi hasa? Hii iliyowashughulikia akina Lowassa, Ndugai, Membe na wengine; na bado akaamini kwamba yeye itamtendea tofauti na hao?
Kinachonishangaza zaidi mimi ni kuhusu uzoefu wooote aliokuwa nao Nchimbi wa ndani kabisa ya chama, halafu ashindwe kujuwa chama kilivyobadilika!
Na yeye ajiachie tu wakati hata damu ya Polepole bado haijakauka!
Narudia swali lile lile kwa anayejuwa kwa uhakika: Emmanuel Nchimbi wakati huu yupo wapi. Hakuna hata ndugu/rafiki mmoja anayejuwa alipo akawaeleza waTanzania?
Au hata yeye mwenyewe kama yupo huru, aseme alipo sasa hivi na hali yake ilivyo, akitaka kueleza.
Mwisho, inanibidi nirudie tena niliyosema hapo juu kuhusu haya maneno ya "SYSTEM/MFUMO".
Tunasumbuliwa na kundi la waharifu, hakuna cha system wala mfumo wowote.