Na. M. M. Mwanakijiji
Ni kweli Emanuel Nchimbi amekuwa kwenye CCM kwa muda mrefu sana. Wengi tunamjua toka akiwa Umoja wa Vijana wa CCM na kwa kweli hakuwa mtu ambaye tulimfikiria hata kwa mbali kuwa anaweza kuwa Makamu wa Rais. Ameweza kupitia sehemu mbalimbali lakini naweza kusema kuwa hakuwa mwanasiasa mwenye mikakaiti mizuri. Alikuwa anafanya maamuzi ambayo kama kuna watu walikuwa wanamuunga mkono basi alikuwa amepigwa upofu (blind sided) wa kutokujua nani anamtakia mema.
Nakumbuka sakata la Lowassa, lakini kabla ya hapo mambo ya kina SAS enzi zile. Alipotangazwa kuwa Makamu wa Rais sikuwahi kudhania alikuwa ana potential ya nyadhifa kubwa hiyo. EN alikuwa ni zao la CCM; aliipenda sana CCM na bila CCM asingekuwa hapo alipo. Inawezekana hili ndiyo kosa lake kubwa ambalo anaenda kulilipia. Inawezekana zile ziara zake za karibuni kwa viongozi mbalimbali wa tofauti zilikuwa ni kuomba wampe nafasi ya kuzungumza SSH. Njia ya mawasiliano ilikatwa na walipoenda kufungua bwawa la umeme mpasuko huo ulikuwa wazi. Alipewa nafasi ya kuimba pambio la sifa hakuimba. Kamba alijitundika mwenyewe.
Nimedokeza kwenye mada nyingine kuwa licha ya kuvuliwa uanachama wanaenda kumshitaki mahakamani; hawataacha astaafu aendelee "kula mema ya nchi'. Kama alidhani ana marafiki hao marafiki hawapo na hakuna mtu yeyote atakayejitokeza kumtetea.
Naamini kama nilivyodokeza juzi usalama wa Nchimbi ni kuwa aamue kweli kujitoa ufahamau. Utetezi wake ni Utanganyika wake. Kwamba kilichomgonganisha na Samia ni suala la yeye kutaka kutetea Tanganyika. Lakini siamini kama ataachwa afike huko; tusije kushangaa lile dudu la "Shinikizo la Damu" likagonga. Lakini endapo EN atafikishwa mahakamani kuna kamata kamata inayokuja kushinda ile ya Oktoba 29. Wote waliowasiliana na kumtia moyo Nchimbi wataingizwa kwenye "njama" na tusije kushanga baadhi ya watu wanaachishwa kazi (mabadiliko mbalimbali hadi jeshini".
Hapa ndipo tulipofika. Hapana; hapa ndipo tulipofikishwa.
Tukitaka tulisaidie taifa na kuwapa msaada mkubwa CCM ni kuwaondoa madarakani. Wataendelea kutusumbua hadi vitukuu vyetu.
Tundu Lissu Aachiliwe Mara Moja bila ya masharti... CCM wapambane na mambo yao.
Mzee Mwanakijiji, ajabu ni hii: Tunazungumza lugha moja lakini bado hatuelewani.
Hapana. Siyo kati yangu na wewe na wanaJF humu Jukwaani; bali ni kwa waTanzania wote wanaoona tukinyeshewa na mvua.
Kutoelewana lugha miongoni mwetu, maana yake hatujui tatizo letu linapotokea, lilipo na linakotupeleka.
Tunazungumzia CCM kutufikisha hapa, lakini hakuna anayesema huyu CCM ni nani hasa?
Tunalaumu CCM tunayotangaziwa inao wanachama makumi ya mamilioni ya waTanzania? Hawa wote ni CCM wanaokipenda chama chao hadi leo kwamba wanajivunia kuwa wanachama wa hii CCM?
Unauliza aliye/aliyekuwa nyuma ya Nchimbi; kwamba miongoni wa mamilioni ya hawa wanachama sasa wanamgwaya Nchimbi kutokana tu na yeye kuhoji anayoyaona yakiendelea ndani ya taifa lao; na sasa takribani wote wanamwona mpotofu; mamilioni ya wanaCCM, achilia mbali hawa waTanzania/waTanganyika wengine?
Naona nitauliza maswali mengi; lakini najuwa siwezi kupata jibu, kwa sababu pamoja na kwamba tunaelewana lugha, haya maswali hayajibiki, kama hayo yako unayouliza. Na sababu kuu ni hiyo moja: Hatutaki kujuwa ni nani hasa KIUKWELIKWELI anayetusababishia matatizo yote haya.
Siku ambayo tutaamua kumfahamu, sina shaka yoyote lugha yetu itanyooka, na pengine juhudi za kumkabili zitaanzia hapo.
Nimalizie kwa swali tena kwa atakayetaka kujibu kwa uhakika:
Emmanuel Nchimbi sasa hivi yupo wapi. Hana hata ndugu wanaoweza kujuwa alipo na kuwahakikishia waTanzania kuwa yupo salama?
Ahaaaa! ni lazima nikatae majibu ya kijinga ya "System iko hivi; Mfumo upo hivi". Tanzania haishikiliwi na vitu hivyo.