MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wenu nyie ni Gigi,umber ruty na masha love.kiongoziHuyo ni mbongo acheni kumuuza mara m south mara Burkina faso,,,Yan hayo ma parody ya south na Burkina Faso yamejua kutuibia mtu wetu,,na wabongo nao wanafata mkumbo tu Burkina Faso ,south Africa wanaongea Kiswahili toka lini ?
na hii picha inatrend sana bongo kama kule Twitter kuna account inatumia ni ya mbongo?Swamidwa Habidadi ni kutoka Burkina Faso ambaye ni mkulima mwenye mafanikio makubwa. Alianza kilimo akiwa na umri mdogo wa miaka 16 baada ya wazazi wake kufariki dunia, na kwa sasa amejitolea kikamilifu katika shughuli za kilimo kuliko masomo yake.
Aligawa shamba alilorithi kutoka kwa wazazi wake, ambalo lina ukubwa wa hekta 6, na kupanda mazao mbalimbali kama mchele, mahindi, maharage, soya, na matunda. Sehemu nyingine ya shamba lake imetengwa kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viwandani. Shamba hili ndiyo tegemeo lake kuu la kipato.
Mwaka huu, Swamidwa amevuna mavuno makubwa ya mazao; magunia 10,000 ya mahindi, magunia 8,000 ya mchele, na magunia 5,000 ya karanga. Pia, ana mifugo mingi ikiwa ni pamoja na ng'ombe zaidi ya 900 na mbuzi 500. Ameajiri jumla ya wafanyakazi 40, ambao ni wanaume 20 na wanawake 20, na ana trekta kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kilimo.
Swamidwa pia ni mfanyabiashara aliye na magari kadhaa ya kifahari, yakiwemo BMW 4, Mercedes Benz wagon 2, na Range Rover 3. Anamiliki gari la Vx Hilux na pia amewanunulia wafanyakazi wake pikipiki 40 kwa ajili ya kurahisisha usafiri wao. Amejenga hoteli kubwa tatu katika eneo lake.
Mbali na mafanikio yake ya kilimo, Swamidwa ni mtoaji mkubwa wa misaada kwa jamii yake. Ameleta umeme na maji safi katika eneo analoishi, na kwa ujumla ni mtu muhimu na tegemeo kubwa kwa jamii inayomzunguka. Yeye ni mfano wa mtu mwenye mafanikio makubwa kupitia kilimo na kujitolea kusaidia wengine.
View attachment 3080182
View attachment 3080183
View attachment 3080184View attachment 3080185
View attachment 3080186
View attachment 3080187
View attachment 3080188
View attachment 3080189
View attachment 3080190
View attachment 3080191
Acha uongo weweUnaijua hekta na eka!!?hekta ni kubwa mara 1000 ya Eka!
Kwao mto wa mbu, ndipo wazazi wake wanapoishi na wanamashamba ya mpungaMweke hapa tumwone mkuu.
hahahaha!Unaijua hekta na eka!!?hekta ni kubwa mara 1000 ya Eka!
Mbona mavuno makubwa sana kuliko eneo!!?hahahaha!
Hekta moja ni sawa na Eka 2.5 tu. kwa lugha rahisi hizo Hekta 6 ni sawa na Ekari 15 tu
Mbona mavuno makubwa sana kuliko eneo!!?
Watakatishaji fedha hao!
Mtwambie anaitwa nani basi kama yupo Mbarali na msije na majina ya Bupe wala Tusekilegi maana kwa shepu yake HAWEZI kuwa Mnyakyusa!!😡😡😡😡Mbona mbongo huyo yuko mbarali huko analima mpunga..
Hapa mi mwenyewe nilibaki nimeshanga!!Acheni kamba jamani sisi ni watu wazima
Hata kama una nia ya kumpamba mtu mbona njia zipo nyingi, yaani ekali 6 uvune magunia elf10 ya mahindi!! aisee labda kilimo cha karatasi
Huyu dada uliyomuweka hapo ni mtanzania,ufanye research kabla ya kupost
www.instagram.com
Maisha ya mitandaoni sio halisi kabisa!tunarushana roho TU!Ndio tumtafute atupe hiyo Elimu mkuu 😂
Hahahaha jamaa anatudanganya live. Hivi anajua alichoandika huyu?Kwamba kwenye hekta 6 humohumo kavuna gunia 10,000 za mahindi, gunia 8,000 za mchele, gunia 5,000 za karanga.
Na kwenye hekta 6 hizohizo bado kuna nafasi ya kilimo cha mazao ya viwandani. Na bado ana mifugo.
Unatuchukuliaje mzee