Swamidwa Habidadi Mkulima Mwenye Ndoto Kubwa Kutoka Burkina Faso

Swamidwa Habidadi Mkulima Mwenye Ndoto Kubwa Kutoka Burkina Faso

Mweke hapa tumwone mkuu.
20240827_112613.jpg


20240827_112646.jpg


20240827_112716.jpg

Huyo hapo mkuu
 
Huyo ni mbongo acheni kumuuza mara m south mara Burkina faso,,,Yan hayo ma parody ya south na Burkina Faso yamejua kutuibia mtu wetu,,na wabongo nao wanafata mkumbo tu Burkina Faso ,south Africa wanaongea Kiswahili toka lini ?
Wenu nyie ni Gigi,umber ruty na masha love.kiongozi
 
Mbo
Swamidwa Habidadi ni kutoka Burkina Faso ambaye ni mkulima mwenye mafanikio makubwa. Alianza kilimo akiwa na umri mdogo wa miaka 16 baada ya wazazi wake kufariki dunia, na kwa sasa amejitolea kikamilifu katika shughuli za kilimo kuliko masomo yake.

Aligawa shamba alilorithi kutoka kwa wazazi wake, ambalo lina ukubwa wa hekta 6, na kupanda mazao mbalimbali kama mchele, mahindi, maharage, soya, na matunda. Sehemu nyingine ya shamba lake imetengwa kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viwandani. Shamba hili ndiyo tegemeo lake kuu la kipato.

Mwaka huu, Swamidwa amevuna mavuno makubwa ya mazao; magunia 10,000 ya mahindi, magunia 8,000 ya mchele, na magunia 5,000 ya karanga. Pia, ana mifugo mingi ikiwa ni pamoja na ng'ombe zaidi ya 900 na mbuzi 500. Ameajiri jumla ya wafanyakazi 40, ambao ni wanaume 20 na wanawake 20, na ana trekta kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kilimo.

Swamidwa pia ni mfanyabiashara aliye na magari kadhaa ya kifahari, yakiwemo BMW 4, Mercedes Benz wagon 2, na Range Rover 3. Anamiliki gari la Vx Hilux na pia amewanunulia wafanyakazi wake pikipiki 40 kwa ajili ya kurahisisha usafiri wao. Amejenga hoteli kubwa tatu katika eneo lake.

Mbali na mafanikio yake ya kilimo, Swamidwa ni mtoaji mkubwa wa misaada kwa jamii yake. Ameleta umeme na maji safi katika eneo analoishi, na kwa ujumla ni mtu muhimu na tegemeo kubwa kwa jamii inayomzunguka. Yeye ni mfano wa mtu mwenye mafanikio makubwa kupitia kilimo na kujitolea kusaidia wengine.

View attachment 3080182

View attachment 3080183

View attachment 3080184View attachment 3080185
View attachment 3080186
View attachment 3080187

View attachment 3080188

View attachment 3080189

View attachment 3080190

View attachment 3080191
na hii picha inatrend sana bongo kama kule Twitter kuna account inatumia ni ya mbongo?
 
Acheni kamba jamani sisi ni watu wazima

Hata kama una nia ya kumpamba mtu mbona njia zipo nyingi, yaani ekali 6 uvune magunia elf10 ya mahindi!! aisee labda kilimo cha karatasi
 
Kwamba kwenye hekta 6 humohumo kavuna gunia 10,000 za mahindi, gunia 8,000 za mchele, gunia 5,000 za karanga.
Na kwenye hekta 6 hizohizo bado kuna nafasi ya kilimo cha mazao ya viwandani. Na bado ana mifugo.

Unatuchukuliaje mzee
Hahahaha jamaa anatudanganya live. Hivi anajua alichoandika huyu?
 
Back
Top Bottom