Tangu tupate misaada hiyo imetusaidia nini? Mbona JPM katekeleza Mega projects nyingi kwa hela yetu!
Swali lako linaeleweka na kuna jibu: Inategemea. Kuna mifano mingi ya nchi zilizotumia mikopo kwa buasara na kufaidi. Mfano nchi nyingi za Ulaya ziliharibika kabisa baada ya Vita Kuu ya Pili na hapo Marekani kuanzia mwaka 1948 ilimwaga pesa USD bilioni 12.4 kupitia "Marshall Plan" na pesa hiizi zilifika hasa Uingereza (26%), ikifuatwa na Ufaransa (18%) na Ujerumani ya Magharibi (11%). Milioni 9 hivi ilifika kama Msaada" wa zawadi, mengine kama mikopo kwa masharti fulani.
Kwa jumla ilikuwa msaada muhimu kupeleka nchi hizi tena kwenye njia ya mafanikio - 1948 bado zilkuwa na njaa (Ujerumani vyakula vilipatikana hadi 1950 kwa mgawio tu, Uingereza hadi 1953, yaani kila mwananchi alipata kadi za kununulia vyakula kwa kiwango fulani).
Marekani ilifaulu kujenga athira yake ya kisiasa dhidi ya Urusi (adui kuu wakati ule), nchi zilizopkoea zilifaulu kujenga uchumi na kutengeneza upya muiundombonu na viwanda.
Kuna mifano ya kinyume, hasa pale ambako mikopo ilitumiwa ama vibaya (wizi upande wa viongozi) au bila busara.
Miradi mikubwa ya TZ hadi sasa imelipiwa kwa madeni ya kibiashara nisipokosei; "
Tanzania has secured a $1.46 billion concessional loan from the Standard Chartered Bank's Group to fund its standard gauge railway line between Morogoro and Dodoma.
Finance Minister Dr Philip Mpango said the new loan was part of an agreement reached with Standard Chartered Bank Group executive director Bill Winters in Dar es Salaam, which would go to fund the 430km line between Morogoro and Makutupora." (chanzo:
Tanzania secures $1.46b SGR loan from Stanchart) Raisi haikumaanisha kwamba pesa ya reli zilipatikana serikalini tayari, bali serikali iliweza kukopa pesa hii kwa benki kwa njia ya kawaida, bila kuomba kwanza guarantee kutoka nchi za nje, IMF au World Bank.
Inayobaki ni deni na busara ya deni itaonekana baadaye, kama reli italeta mapato ya kutosha kulipia gharama za madeni haya aana benki inategemea kila senti inarudishwa pamoja na riba iliyopatanwa.
Katika miaka ya nyuma (2001 na 2006) "nchi beberu" ziliamua kufuta madeni mengi ya Tanzania.
Tangu siku zile madeni yalipanda tena, ila tu zaidi kutoka "wabepari" kama benki za biashara (hawana masharti kisumbufu kama haki za binadamu) kuliko "mabeberu" (taasisi za kiserikali zinazosumbua mara kwa mara na madai ya aina hii.
"