Inawezekana uko sahihi. Wanaanza na wadogo wadogo kabla ya kubwa lao. Sasa hivi wanasubiri wakati wa kukaribia uchaguzi mkuu ndipo washughulike naye kama ambavyo serikali ya Amerika inavyofanya sasa kwa Trump.
Itasaidia kulinda heshima ya taaluma (profession) ya wanasheria. Fikiria kama wanasheria wote nchini kwetu wakiwa na tabia kama ya Tundu Lisu nchi itakalika kweli? Si tutakuwa kama Kenya, vurugu kila siku na watu kupoteza uhai?
Lengo siyo kumkatia umeme unaompa riziki yake ya maisha. Lengo ni kuisafisha hii taaluma ya uwakili wa mahakama kuu yetu ambayo anaichafua na wengine wameanza kuiga uchafuzi huo. Apishe huku na aendelee kwenye hiyo taaluma ya siasa aliyoichagua, anayoipenda, anayoimudu na inayomwingizia kipato cha mamillioni ya dola kwa mwaka.
Ni kweli hawa nao wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo. Kosa lao si la kukiuka maadili ya profession ya uanasheria. Kosa lao linaweza likawa ni incompetence (weledi mdogo), negligence au corruption. Makosa hayo hayashughulikiwi na Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Mahakama Kuu. In fact makosa hayo ni makubwa zaidi kuliko haya yanayofanywa na Tundu Lisu na Mwabukusi.
Walio ridhia mkataba ni wabunge ambao ndiyo wawakilishi wetu rasmi bungeni tuliowachagua wenyewe. Bunge lina maadili yake na kamati yake ya maadili ya wabunge. Kuridhia mkataba wabunge hawajakiuka maadili yao kama wabunge, tunachoweza kuwashughulikia ni kwenye sanduku la kura la mwaka 2025. Sasa hivi hatuwezi kuwafanya cho chote, labda kuwabembeleza wakafute hayo maridhio waliyoyafanya.
Sasa huoni hizo vurugu, machafuko na vifo vya mara kwa mara zinazotokea huko Kenya? Kila kitu duniani kina mipaka yake. Demokrasia ina mipaka yake na kila nchi ina aina yake ya demokrasia inayozingatia maadili na utamaduni wa nchi. Anal sex na mambo mengine ya LGBTQQIP2 kwa USA na ulaya ya magharibi ni demokrasia. Kwetu na nchi kama Russia na China mambo hayo hayakubaliki hata kidogo.
Wewe kijana kuwa na heshima kwa wazee. Hawa ndiyo wamekuzaa, wamekulea, wamekusomesha na kukufikisha hapa ulipo. Elimu uliyoipata imetoka kwa hawa wazee. Inaelekea sasa wewe mtoto umevurugwa na hao wazungu. Hayo maadili na tamaduni za hao wazungu unaona kwamba ni za kisasa. Huo u homosexuality, transgender na midudu mingine mnayofanya mnaona ndiyo kisasa. Ni lazima sisi wazee wenu tuwarudishe kwenye mstari.
Nimeeleza kuwa kila fani (profession) ina maadili yake. Maadili ya profession ya udaktari ni tofauti na yale ya profession ya uanasheria na hivyo hivyo kwa profession zingine.
Nimeeleza pia kuwa kila kazi ina maadili (behavior) yake specific. Chagudoa maadili yake ni pamoja na kuvaa nusu uchi na kunengua kiuno anapotembea. Jambazi naye ana behavior yake, pia mwanasiasa na kadhalika.
Kila nchi pia huwa ina maadili na utamaduni wake wa kipekee. Maadili na utamaduni wa Tanzania ni tofauti na Kenya, Rwanda, USA, UK na kadhalika. Sijui kama bado hujanielewa.