Taaluma isiyo na maadili sio taaluma. Hongera AG kwa kulisimamia hili lakini kwanini usimfutilie mbali Uwakili wa Tundu Lissu badala ya Mwabukusi?

Tundu Lissu keshakuwa mwanasiasa kwaio wanajua kumtolea uwakili sio dili maana inawezekana anapractise "rarely". Wanadhani Mwabukusi anakula kupitia uwakili kwaio wanataka kukata umeme.. Sasa wanaompenda Mwabukusi wampe kazi ya kisiasa basi watakuwa wamemfunga AG goli saba za mshindo
mwabukusi apewe uenyekiti wa chadema, mbowe chama kimemshinda
 
Kama unajua unajua tu; uzuri wa taaluma uko hivi, wanakufutia huku unasajiliwa huko duniani, muhimu kichwa kiwe smart na si makaratasi.
 
Maadili ndiyo kila kitu kwenye kila kazi na kila taaluma. Maadili hayo yanajumuisha jinsi unavyoongea, unavyovaa na hata unavyotembea na yanapaswa yazingatiwe hata kama mtu yuko nje ya kazi. Maadili ndiyo utambulisho wa taaluma.

Na kila taaluma ina maadili yake special. Mhudumu wa baa utamtambua kwa ongea yake, vaa yake, ukaaji wake na tembea yake. Vivyo hivyo kwa nesi, daktari, engineer, mhasibu, wakili wa mahakama kuu na kadhalika.

Ni kweli kabisa watu kama Fatuma Karume na Tundu Lissu kila mwenye akili aliwaona wazi hawaendani kabisa na maadili ya taaluma zao za kuwa mawakili wa mahakama kuu. Kwa usahihi kabisa Fatuma alifyekwa kutoka kwenye taaluma hiyo.

Inashangaza huyu Tundu Lissu bado anaendelea kupeta hadi leo. Amediriki hadi kukaidi summon ya DCI. Anaendelea kuwadhihaki na kuwatukana viongozi wakuu kwa kiwango kikubwa sana kuliko walicho onesha akina Mwabukusi, Madeleke na Nashara ambao wako kwenye kashikashi ya kufyekwa. Kwa nini AG amekuwa anaogopa kumshughulikia Tundu Lissu? Au alisha shughulikiwa kitambo sisi hatuna taarifa?
AAG atuambie kwann Saini yake haipo kwenye mkataba Ule wa kimangungo.
 
Inawezekana uko sahihi. Wanaanza na wadogo wadogo kabla ya kubwa lao. Sasa hivi wanasubiri wakati wa kukaribia uchaguzi mkuu ndipo washughulike naye kama ambavyo serikali ya Amerika inavyofanya sasa kwa Trump.

Itasaidia kulinda heshima ya taaluma (profession) ya wanasheria. Fikiria kama wanasheria wote nchini kwetu wakiwa na tabia kama ya Tundu Lisu nchi itakalika kweli? Si tutakuwa kama Kenya, vurugu kila siku na watu kupoteza uhai?

Lengo siyo kumkatia umeme unaompa riziki yake ya maisha. Lengo ni kuisafisha hii taaluma ya uwakili wa mahakama kuu yetu ambayo anaichafua na wengine wameanza kuiga uchafuzi huo. Apishe huku na aendelee kwenye hiyo taaluma ya siasa aliyoichagua, anayoipenda, anayoimudu na inayomwingizia kipato cha mamillioni ya dola kwa mwaka.

Ni kweli hawa nao wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo. Kosa lao si la kukiuka maadili ya profession ya uanasheria. Kosa lao linaweza likawa ni incompetence (weledi mdogo), negligence au corruption. Makosa hayo hayashughulikiwi na Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Mahakama Kuu. In fact makosa hayo ni makubwa zaidi kuliko haya yanayofanywa na Tundu Lisu na Mwabukusi.

Walio ridhia mkataba ni wabunge ambao ndiyo wawakilishi wetu rasmi bungeni tuliowachagua wenyewe. Bunge lina maadili yake na kamati yake ya maadili ya wabunge. Kuridhia mkataba wabunge hawajakiuka maadili yao kama wabunge, tunachoweza kuwashughulikia ni kwenye sanduku la kura la mwaka 2025. Sasa hivi hatuwezi kuwafanya cho chote, labda kuwabembeleza wakafute hayo maridhio waliyoyafanya.

Sasa huoni hizo vurugu, machafuko na vifo vya mara kwa mara zinazotokea huko Kenya? Kila kitu duniani kina mipaka yake. Demokrasia ina mipaka yake na kila nchi ina aina yake ya demokrasia inayozingatia maadili na utamaduni wa nchi. Anal sex na mambo mengine ya LGBTQQIP2 kwa USA na ulaya ya magharibi ni demokrasia. Kwetu na nchi kama Russia na China mambo hayo hayakubaliki hata kidogo.

Wewe kijana kuwa na heshima kwa wazee. Hawa ndiyo wamekuzaa, wamekulea, wamekusomesha na kukufikisha hapa ulipo. Elimu uliyoipata imetoka kwa hawa wazee. Inaelekea sasa wewe mtoto umevurugwa na hao wazungu. Hayo maadili na tamaduni za hao wazungu unaona kwamba ni za kisasa. Huo u homosexuality, transgender na midudu mingine mnayofanya mnaona ndiyo kisasa. Ni lazima sisi wazee wenu tuwarudishe kwenye mstari.

Nimeeleza kuwa kila fani (profession) ina maadili yake. Maadili ya profession ya udaktari ni tofauti na yale ya profession ya uanasheria na hivyo hivyo kwa profession zingine.

Nimeeleza pia kuwa kila kazi ina maadili (behavior) yake specific. Chagudoa maadili yake ni pamoja na kuvaa nusu uchi na kunengua kiuno anapotembea. Jambazi naye ana behavior yake, pia mwanasiasa na kadhalika.

Kila nchi pia huwa ina maadili na utamaduni wake wa kipekee. Maadili na utamaduni wa Tanzania ni tofauti na Kenya, Rwanda, USA, UK na kadhalika. Sijui kama bado hujanielewa.
Tulia ww muumini wa nidhamu ya woga na unafiki. Sisi tunaangalia tija na sio muonekano wa mtu.
 
Maadili ndiyo kila kitu kwenye kila kazi na kila taaluma. Maadili hayo yanajumuisha jinsi unavyoongea, unavyovaa na hata unavyotembea na yanapaswa yazingatiwe hata kama mtu yuko nje ya kazi. Maadili ndiyo utambulisho wa taaluma.

Na kila taaluma ina maadili yake special. Mhudumu wa baa utamtambua kwa ongea yake, vaa yake, ukaaji wake na tembea yake. Vivyo hivyo kwa nesi, daktari, engineer, mhasibu, wakili wa mahakama kuu na kadhalika.

Ni kweli kabisa watu kama Fatuma Karume na Tundu Lissu kila mwenye akili aliwaona wazi hawaendani kabisa na maadili ya taaluma zao za kuwa mawakili wa mahakama kuu. Kwa usahihi kabisa Fatuma alifyekwa kutoka kwenye taaluma hiyo.

Inashangaza huyu Tundu Lissu bado anaendelea kupeta hadi leo. Amediriki hadi kukaidi summon ya DCI. Anaendelea kuwadhihaki na kuwatukana viongozi wakuu kwa kiwango kikubwa sana kuliko walicho onesha akina Mwabukusi, Madeleke na Nashara ambao wako kwenye kashikashi ya kufyekwa. Kwa nini AG amekuwa anaogopa kumshughulikia Tundu Lissu? Au alisha shughulikiwa kitambo sisi hatuna taarifa?
LISSU amewa outclass kuanzia bungeni mpaka nje ya bunge!!
 
uniqueness for all ni kufuata sheria zilizokubaliwa na jamii
Kuna watu bila vurugu na kuenenda against miongozo dunia haijizungushi vizuri kwenye mhimili wake.Utazoea tu.Ukitaka kushindana naye kwenye hizohizo sheria anakubwaga asubuhi na mapema.
 
Ni kweli, uadilifu kwenye tasnia ya sheria ni muhimu haswa ukizingatia majukumu ya mwanasheria yeyote. Mkuu wa chama cha wanasheria ni kioo cha jamii na maoni yake katika kila suala hutiliwa maanani na watu wengi. Wamombo husema, "You don't preache water and drink wine".
 
Na ukatoa mfano wa Mashinji kama Daktari kuasahau kwamba hayo "maadili" ya udaktari unayozungumzia hapo ni tofauti na hiyo kazi aliyokuwa akifanya. Hakuna uhusiano wa aina yoyote hapo.
Ndiyo maana nikaona hujui ulichokuwa unalenga tokea mwanzo wa mada.

Na usijifanye kwamba hujui kuwa katika kila 'Profession', pamoja na kuwa na hayo maadili; hao ni watu tu, kuna matapeli, majizi na takataka za kila aina katika profession hizo.
Wewe naona bado hujaelewa umuhimu na maana ya professional ethics and professional ethical codes of conducts.

Ni kwamba ukiwa mwanachama wa kundi lo lote kuna kanuni na taratibu fulani ambazo ni lazima uzifuate. Ukizikiuka unafutwa kwenye hilo kundi au unakuwa suspended kwa kipindi fulani. Kwa mfano hata humu Jf mwenendo wako (behavior) ukikiuka kanuni na taratibu za Jf utalamba ban ya kuonekana humu. Hata kwenye makundi ya WhatsApp wenzako wakikuona ni nuisance, administrators wa group watakuondoa kwenye group lao. Hii haimaanishi kwamba umefanya kosa la jinai wala haikuondolei uhuru wako wa kufanya mambo mengine.

Vivyo hivyo kila professional body yake inayosajili professions wake na kusimamia (administrate) mienendo, maadili na tabia (professional ethics) za wanachama wake. Mawakili wa Mahakama Kuu ni watumishi wa mahakama kuu. Mienendo na maadili yao yanasimamiwa na Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Mahakama Kuu na ndiyo huko AG kapeleka suala la Mwabukusi. Tunachosema Tundu Lisu naye apelekwe huko kwenye kamati ya mawakili wenzake wa mahakama kuu kwani ukiukaji wake wa maadili ya uwakili.

Baraza la Madaktari wa Tanganyika (MCT) ndiyo linasimamia maadili ya madaktari wote wa Tanzania bara. Daktari yo yote anayeyakiuka maadili ya udaktari, usajili wake hufutwa au kuwa suspended kwa kipindi fulani. Dr Mashinji aliendelea kuishi kwenye maadili yake ya udaktari hata alipokuwa huko chadema na sasa yuko ccm. Hivyo bado jina lake lipo kwenye daftari la Msajili wa madaktari wa Tanganyika.

Kama bado hujaelewa, sina namna nyingine ya kukuelimisha. Professional ethical codes of conducts are mandatory to every member of that profession.
 
Big brain gani anabwabwaja maneno ya ovyo yasiyo na staha.
Tundu Antipas Mughwai Lissu ni ubongo mkubwa huyo fenesi hata wakijaa bombardier hawamuwezi Lissu ukumbuke ukimfanyia kibaya Lissu kinakurudia mara tatu yake kama huamini nenda CHATTLE kwenye Ile nyumba ya milele kamuulize kubwa la maadui kilichomtokea
 
Wewe naona bado hujaelewa umuhimu na maana ya professional ethics and professional ethical codes of conducts.

Ni kwamba ukiwa mwanachama wa kundi lo lote kuna kanuni na taratibu fulani ambazo ni lazima uzifuate. Ukizikiuka unafutwa kwenye hilo kundi au unakuwa suspended kwa kipindi fulani. Kwa mfano hata humu Jf mwenendo wako (behavior) ukikiuka kanuni na taratibu za Jf utalamba ban ya kuonekana humu. Hata kwenye makundi ya WhatsApp wenzako wakikuona ni nuisance, administrators wa group watakuondoa kwenye group lao. Hii haimaanishi kwamba umefanya kosa la jinai wala haikuondolei uhuru wako wa kufanya mambo mengine.

Vivyo hivyo kila professional body yake inayosajili professions wake na kusimamia (administrate) mienendo, maadili na tabia (professional ethics) za wanachama wake. Mawakili wa Mahakama Kuu ni watumishi wa mahakama kuu. Mienendo na maadili yao yanasimamiwa na Kamati ya Maadili ya Mawakili wa Mahakama Kuu na ndiyo huko AG kapeleka suala la Mwabukusi. Tunachosema Tundu Lisu naye apelekwe huko kwenye kamati ya mawakili wenzake wa mahakama kuu kwani ukiukaji wake wa maadili ya uwakili.

Baraza la Madaktari wa Tanganyika (MCT) ndiyo linasimamia maadili ya madaktari wote wa Tanzania bara. Daktari yo yote anayeyakiuka maadili ya udaktari, usajili wake hufutwa au kuwa suspended kwa kipindi fulani. Dr Mashinji aliendelea kuishi kwenye maadili yake ya udaktari hata alipokuwa huko chadema na sasa yuko ccm. Hivyo bado jina lake lipo kwenye daftari la Msajili wa madaktari wa Tanganyika.

Kama bado hujaelewa, sina namna nyingine ya kukuelimisha. Professional ethical codes of conducts are mandatory to every member of that profession.
Kwa hiyo aliyesaini utopolo kwenye ule mkataba hashughulikiwi na hizo kanuni lakini yule anaepinga huo utopolo uliofanyika ndo anatakiwa kushughulikwa kwamba Hana maadili! Mi nadhani waarabu hawakuishia kuhonga Hela pekee huenda watu wamekula hadi dullar open head maana akili za kawaida haziwezi kukubaliana na huu muamala
 
Kama raia huru usiyependa dola kuchezewa si ujitolee kwenda Mahakamani ili kufungua madai awajibishwe!
Masuala ya ukiukaji wa professional ethics hayashughulikiwi mahakamani. Mahakama hushughulika na kesi za jinai na madai tu na zile za kikatiba. (criminal and civil cases). Ukiukwaji wa professional ethical codes of conducts hushughulikiwa na professional ethical bodies; kwa mawakili wa mahakama kuu kama alivyo Tundu Lisu ni Kamati ya Mawakili wa Mahakama Kuu.
Kama unajua unajua tu; uzuri wa taaluma uko hivi, wanakufutia huku unasajiliwa huko duniani, muhimu kichwa kiwe smart na si makaratasi.
Mhhhh yaani Tundu Lisu akasajiliwe kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Uingereza au ya Amerika? Kwanza riziki yake wala haitokani na huo uwakili wa mahakama, unatokana na siasa huko chadema.

AAG atuambie kwann Saini yake haipo kwenye mkataba Ule wa kimangungo.
Mikataba haisainiwi na AG. Yeye ni mshauri tu wa serikali na si lazima ushauri wake ufuatwe. Na huwezi ukashauri kama hujaombwa kushauri.

LISSU amewa outclass kuanzia bungeni mpaka nje ya bunge!!
Amewa outclass labda kwa utundu na wazazi wake hawakukosea kumpa hilo jina la tundu! Lakini utundu siyo deal na mara nyingi huwa na madhara. Alikaribia kupoteza maisha yake kwa sababu ya huo utundu wake lakini hawezi kuuacha kwani amezaliwa nao. Inabidi wamvumilie lakini kwenye hili group la mawakili wa mahakama aondolewe.

Kuna watu bila vurugu na kuenenda against miongozo dunia haijizungushi vizuri kwenye mhimili wake.Utazoea tu.Ukitaka kushindana naye kwenye hizohizo sheria anakubwaga asubuhi na mapema.
Watu wanaopenda vurugu watatupwa wakaishi Syria au Afghanistan. Isitoshe hapa tunaongelea maadili ya uwakili, hayana uhusiano na sheria za nchi. Tungalikuwa tunaongelea uchochezi ndipo mambo ya sheria yangehusika.
 
Masuala ya ukiukaji wa professional ethics hayashughulikiwi mahakamani. Mahakama hushughulika na kesi za jinai na madai tu na zile za kikatiba. (criminal and civil cases). Ukiukwaji wa professional ethical codes of conducts hushughulikiwa na professional ethical bodies; kwa mawakili wa mahakama kuu kama alivyo Tundu Lisu ni Kamati ya Mawakili wa Mahakama Kuu.
Kwako wewe kuchezewa dola unaona ni ethical issue?

Mwananchi wa kawaida akiichezea dola utampeleka kwenye ethical body ipi?
 
Kwa hiyo aliyesaini utopolo kwenye ule mkataba hashughulikiwi na hizo kanuni lakini yule anaepinga huo utopolo uliofanyika ndo anatakiwa kushughulikwa kwamba Hana maadili! Mi nadhani waarabu hawakuishia kuhonga Hela pekee huenda watu wamekula hadi dullar open head maana akili za kawaida haziwezi kukubaliana na huu muamala
Kuupinga huo mkataba siyo kosa na wengi wanaupinga. Kosa ni kuwatukana viongozi wakuu wa nchi na kuwaita matope ili hali yeye ni mtumishi wa serikali: mawakili wa mahakama kuu ni watumishi wa serikali. Kwa matusi hayo anapaswa kuondolewa kwenye utumishi wa serikali ili awe huru kutukana kama akina mbowe ingawaje huko nako kuna sheria ya vyama vya siasa chini ya Mtungi.
 
Maadili ndiyo kila kitu kwenye kila kazi na kila taaluma. Maadili hayo yanajumuisha jinsi unavyoongea, unavyovaa na hata unavyotembea na yanapaswa yazingatiwe hata kama mtu yuko nje ya kazi. Maadili ndiyo utambulisho wa taaluma.

Na kila taaluma ina maadili yake special. Mhudumu wa baa utamtambua kwa ongea yake, vaa yake, ukaaji wake na tembea yake. Vivyo hivyo kwa nesi, daktari, engineer, mhasibu, wakili wa mahakama kuu na kadhalika.

Ni kweli kabisa watu kama Fatuma Karume na Tundu Lissu kila mwenye akili aliwaona wazi hawaendani kabisa na maadili ya taaluma zao za kuwa mawakili wa mahakama kuu. Kwa usahihi kabisa Fatuma alifyekwa kutoka kwenye taaluma hiyo.

Inashangaza huyu Tundu Lissu bado anaendelea kupeta hadi leo. Amediriki hadi kukaidi summon ya DCI. Anaendelea kuwadhihaki na kuwatukana viongozi wakuu kwa kiwango kikubwa sana kuliko walicho onesha akina Mwabukusi, Madeleke na Nashara ambao wako kwenye kashikashi ya kufyekwa. Kwa nini AG amekuwa anaogopa kumshughulikia Tundu Lissu? Au alisha shughulikiwa kitambo sisi hatuna taarifa?
ungeonekana una akili kama ungebainisha hapa matusi ya lisu kwa hao unaowaita viongozi wakuu. vinginevyo wewe ni CHAWA PRO usiye hata na akili.
sikiliza hotuba za LISU MFANO ILE YA CHATO KISHA SEMA ALITUKANA TUSI GANI?
Baki na ujinga wako usitufanye wote wajinga
 
Kwako wewe kuchezewa dola unaona ni ethical issue?

Mwananchi wa kawaida akiichezea dola utampeleka kwenye ethical body ipi?
Mwananchi wa kawaida atashughulikiwa na sheria za nchi kama amezivunja. Huyo professional atashughulikiwa kote kote kama amevunja professional ethical codes of conducts na kama pia amevunja sheria za nchi at the same time.
 
ungeonekana una akili kama ungebainisha hapa matusi ya lisu kwa hao unaowaita viongozi wakuu. vinginevyo wewe ni CHAWA PRO usiye hata na akili.
sikiliza hotuba za LISU MFANO ILE YA CHATO KISHA SEMA ALITUKANA TUSI GANI?
Baki na ujinga wako usitufanye wote wajinga
Kumwita rais wa nchi matope ni kitu gani kama si matusi? Au wewe kwako ni maneno gani ni matusi? Kwako matusi ni yale ya nguoni tu?
 
Maadili ndiyo kila kitu kwenye kila kazi na kila taaluma. Maadili hayo yanajumuisha jinsi unavyoongea, unavyovaa na hata unavyotembea na yanapaswa yazingatiwe hata kama mtu yuko nje ya kazi. Maadili ndiyo utambulisho wa taaluma.

Na kila taaluma ina maadili yake special. Mhudumu wa baa utamtambua kwa ongea yake, vaa yake, ukaaji wake na tembea yake. Vivyo hivyo kwa nesi, daktari, engineer, mhasibu, wakili wa mahakama kuu na kadhalika.

Ni kweli kabisa watu kama Fatuma Karume na Tundu Lissu kila mwenye akili aliwaona wazi hawaendani kabisa na maadili ya taaluma zao za kuwa mawakili wa mahakama kuu. Kwa usahihi kabisa Fatuma alifyekwa kutoka kwenye taaluma hiyo.

Inashangaza huyu Tundu Lissu bado anaendelea kupeta hadi leo. Amediriki hadi kukaidi summon ya DCI. Anaendelea kuwadhihaki na kuwatukana viongozi wakuu kwa kiwango kikubwa sana kuliko walicho onesha akina Mwabukusi, Madeleke na Nashara ambao wako kwenye kashikashi ya kufyekwa. Kwa nini AG amekuwa anaogopa kumshughulikia Tundu Lissu? Au alisha shughulikiwa kitambo sisi hatuna taarifa?
Huna akili ,watu namna yako ndani ya nchi hatufiki popote,pumbavu
 
Back
Top Bottom