KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni kweli washitaki kwa kuingilia privacy yako; ukiwa na mwanasheria mzuri watakulipa fidia kubwa kuliko deni hilo. Deni ni jambo lako private inayolindwa na katiba kifungu 16-1 mpaka pale mahakama itakapoamuru litangazwe. Walichotakiwa wao na kukupeleka mahakamani, siyo vinginevyo.
Mbona kama umetupiga kama Mkuu...

16.-(1) Chama kinachounda Serikali na Chama chenye haki ya
kuchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, vitateua
Wanadhimu wa vyama hivyo Bungeni ambao watajulikana kwa
jina la Mnadhimu wa Serikali na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni.
 
Hiki ndo nilichowafanyia PESA X mbwa wale, nimepita na 80000 yao, na kunishika hawawezi, shenzi kabisa yani mtu ukikaa tu siku tatu bila kuwalipa wanaaza usumbufu wa kingese.

Mpaka waje kudevelop hizo applications zao tutakuwa tumewaliza sana.
Acha wizi lipa pesa za watu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Hii nzuri ila umeenda harakaharaka sana rejea tena kutupa huo utaalamu tafadhali
 
Mbona kama umetupiga kama Mkuu...

16.-(1) Chama kinachounda Serikali na Chama chenye haki ya
kuchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, vitateua
Wanadhimu wa vyama hivyo Bungeni ambao watajulikana kwa
jina la Mnadhimu wa Serikali na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni.
Sijui wewe unasoma Katiba gani yenye kifungu hicho ulichonukuu; nadhani unasoma kanuni za bunge; Katiba yenyewe inasema hivi
1708701439140.png
 
Wachana nao
kwani wakitumia watu sms kama hiyo we unapungukiwa nini, songa mbele usirudishe pesa
Tatizo lipo mkuu.
Kumbuka katika hao 200 Kuna michepuko 7 ya Vladmir Putin, Kuna mchumba wake na Wana kwaya wenzake bila kusahau wapangaji wenzake.
Sasa michepuko ikigundua kwamba jamaa sh 56 tuzinamtoa jasho wakati bar anakunywa bia za kutosha, si fedheha hiyo.
 
Siku nyingine kopa BRANCH hawana huo ujinga wa kuona contacts zako, isitoshe usiporudisha mkopo on time wanakupigia magoti wakiimba urudishe 50 percent only.
Binafsi wananida hela ya kueleweka karibia M na wameniambia nisimwambie mtu.
Very professional these guys.
 
Mara hii nimeamini maneno ya mleta mada,hii text nilitumiwa wiki iliyopita inaonekana kuna jamaa ana namba yangu amewakopa,surprisingly nimejikuta kumbe na mimi kitendo cha mtu mwenye # yangu kukopa mtandaoni basi moja kwa moja nakuwa nimemdhamini hata kama simjui.
Screenshot_2024-03-14-21-53-28-270_com.android.mms-edit.jpg

(truecaller imenipa jina la mmiliki wa hiyo # ila sijamfahamu hasa ila ktk kumbukumbu zangu zinaonyesha nilizungumza nae mwaka jana zaidi ya mara nne,
Screenshot_2024-03-14-22-27-58-466_com.truecaller.jpg
kwa wanaomfahamu watamuona kama mtu wa ajabu sana,hakika huu ni udhalilishaji)
 
Mara hii nimeamini maneno ya mleta mada,hii text nilitumiwa wiki iliyopita inaonekana kuna jamaa ana namba yangu amewakopa,surprisingly nimejikuta kumbe na mimi kitendo cha mtu mwenye # yangu kukopa mtandaoni basi moja kwa moja nakuwa nimemdhamini hata kama simjui.View attachment 2934580

(truecaller imenipa jina la mmiliki wa hiyo # ila sijamfahamu hasa ila kwa wanaomfahamu watamuona kama mtu wa ajabu sana,hakika huu ni udhalilishaji)
Wewe picha yako itakua mtandaoni soon 🤣🤣🤣
 
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita.

View attachment 2910966View attachment 2910967
Ndugu stefano iyanga lipa pesa ya watu aisee
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
App nyingi za finance huwa zina detect kama simu ipo rooted na huwa hazifanyi kazi kwenye rooted phones
 
Masharti yao mepesi sana. Uwe na laini iwe angalau active zaidi ya mwaka mmoja, jina ulilosajiriwa kwenye laini liwe sawa na NIDA utakayopeleka. Hafu uwape na access ya contacts. Basi
 
Wachana nao
kwani wakitumia watu sms kama hiyo we unapungukiwa nini, songa mbele usirudishe pesa
kuna nyingine Pesa X wana maneno ya shombo hadi niliwasave wote namba zao 11 kwenye access nilifinya kuna app moja ilikuwa hacked ilikuwa inaruhusu kupata sms na namba lakin inawapa empt kwahyo hawakupata access yoyote sikuwalipa niliwazulumu
 
Back
Top Bottom