Twin_Kids
Mahakamani unaweza kupelekwa na kesi ikawa against your favor.
Ukienda BRAC au NMB kukopa unaweka dhamana kitu. Online hauweki kitu, in theory tunatarajia hitaji lako la next loan ndilo litakupush ulipe (in practice ni mchanganyiko na sitaandika)
a) Ili nijue riba ya kampuni natakiwa kujua principal amount aliyopokea mleta uzi na alichotakiwa kurudisha. Riba imo ndani ya maelekezo ya BOT.
b) Mkopo ni wa online. Kuonana, kunaua logic ya msingi ya mkopo wa online.
c) Unatumiwa SMS/ Unapigiwa na namba tofauti kwakua mteja una stages. Kuna stage 0 (Kabla haujaoverdue), stage 1 (baada ya kuoverdue kwa siku 1 mpaka 3 au 7), stage 2 (umeoverdue kuanzia siku 4 n.k) so ni lazima utapigiwa na namba tofauti kwakua hizo stages zote zina staff tofauti.
2) Upo sahihi. Kuna namna za kuongea na mteja na emergency contacts. Hizi contacts ambazo wamepata access sijui sheria inasemaje. Hizi siwezi kuzisemea, kama unahisi unaweza kushinda mahakamani jaribu kumshirikisha mwanasheria.
3) Taasisi zinajulikana. Nilielezea ni kwanini mnafeel hazijulikani but zinajulikana. So kutojulikana usiutumie kama msingi, as I said earlier ni ngumu online platform na mteja kukutana kudiscuss malipo, ikiwa mteja anaona kuna umuhimu huo ni bora akapokea simu na kujielezea.
Of course kampuni nyingi hua zinaweza kumfanyia exemption mteja mfano badala ya 35K akalipa 25K. Kwa ulichoandika hapa naona haujui Fintech inafanyaje kazi kwa % kubwa.
Hela za kugawa kama njugu? Hili swali ni la kitoto mno sioni kama ni level yangu ya uelewa kulijibu. Kama mitandao ya simu itakua inakata pesa kutakua hakuna haja ya uwepo wa debt collectors.