KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Backup ya taarifa zake ziko kwenye system yao. Hata akifuta hiyo app wao bado wanazo
Fanya hivi nenda setting>Privacy>permission manager>apps that can control your data....ukifungua huk utazikuta app zote ulizo allow ku access simu yako then gusa moja moja utakuta kipengele cha dont allow.
 
Wachana nao
kwani wakitumia watu sms kama hiyo we unapungukiwa nini, songa mbele usirudishe pesa
Eeeh miye nashangaa mtu anakwambia eti wanadharirisha kivipi si umechukua pesa yani wakikudharirisha ndio tiketi huwalipi kabisa

Na watanzania tunakuwa watu wa ajabu sana hao ilitakiwa hao jamaa wapigwe pesa mpaka wajue kumbe wabongo hawagopi dharirishwa
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Kwa jinsi walivyo wahuni, hii ndio dawa yao.
 
Mkuu sasa huoni kuwa Mwanasheria anaweza kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha kuendesha kesi kuliko ungewalipa hiyo ths.56,000?
Tumia busara lipa pesa yao endelea na mipango yako!
 
Eeeh miye nashangaa mtu anakwambia eti wanadharirisha kivipi si umechukua pesa yani wakikudharirisha ndio tiketi huwalipi kabisa

Na watanzania tunakuwa watu wa ajabu sana hao ilitakiwa hao jamaa wapigwe pesa mpaka wajue kumbe wabongo hawagopi dharirishwa
Wanaundaga magroup ya Whatsapp na kukudharirisha. Kuna jamaa mmoja niliona ameundiwa group la WhatsApp na huko wameaddiwa ndugu na wazazi wake. Group linaitwa NAUZA MK......U ILI NIPATE PESA YA KUWALIPA PESA X. Wakaweka na Profile picture ha jamaa kabisa. Wanauzi sana hao raia.
 
Tupate wakili wa kujitolea tuwapeleke wao mahakamani kwa kosa la kutudhalilisha.
 
Wanaundaga magroup ya Whatsapp na kukudharirisha. Kuna jamaa mmoja niliona ameundiwa group la WhatsApp na huko wameaddiwa ndugu na wazazi wake. Group linaitwa NAUZA MK......U ILI NIPATE PESA YA KUWALIPA PESA X. Wakaweka na Profile picture ha jamaa kabisa. Wanauzi sana hao raia.
mamlaka za nchi yetu huwa zinakua sharp kupambana na wapinzani tu, magenge kama haya wanachukua muda mrefu kuwawajibisha
 
Twin_Kids

Mahakamani unaweza kupelekwa na kesi ikawa against your favor.

Ukienda BRAC au NMB kukopa unaweka dhamana kitu. Online hauweki kitu, in theory tunatarajia hitaji lako la next loan ndilo litakupush ulipe (in practice ni mchanganyiko na sitaandika)

a) Ili nijue riba ya kampuni natakiwa kujua principal amount aliyopokea mleta uzi na alichotakiwa kurudisha. Riba imo ndani ya maelekezo ya BOT.

b) Mkopo ni wa online. Kuonana, kunaua logic ya msingi ya mkopo wa online.

c) Unatumiwa SMS/ Unapigiwa na namba tofauti kwakua mteja una stages. Kuna stage 0 (Kabla haujaoverdue), stage 1 (baada ya kuoverdue kwa siku 1 mpaka 3 au 7), stage 2 (umeoverdue kuanzia siku 4 n.k) so ni lazima utapigiwa na namba tofauti kwakua hizo stages zote zina staff tofauti.

2) Upo sahihi. Kuna namna za kuongea na mteja na emergency contacts. Hizi contacts ambazo wamepata access sijui sheria inasemaje. Hizi siwezi kuzisemea, kama unahisi unaweza kushinda mahakamani jaribu kumshirikisha mwanasheria.

3) Taasisi zinajulikana. Nilielezea ni kwanini mnafeel hazijulikani but zinajulikana. So kutojulikana usiutumie kama msingi, as I said earlier ni ngumu online platform na mteja kukutana kudiscuss malipo, ikiwa mteja anaona kuna umuhimu huo ni bora akapokea simu na kujielezea.

Of course kampuni nyingi hua zinaweza kumfanyia exemption mteja mfano badala ya 35K akalipa 25K. Kwa ulichoandika hapa naona haujui Fintech inafanyaje kazi kwa % kubwa.

Hela za kugawa kama njugu? Hili swali ni la kitoto mno sioni kama ni level yangu ya uelewa kulijibu. Kama mitandao ya simu itakua inakata pesa kutakua hakuna haja ya uwepo wa debt collectors.
........ c) Unatumiwa SMS/ Unapigiwa na namba tofauti kwakua mteja una stages. Kuna stage 0 (Kabla haujaoverdue), stage 1 (baada ya kuoverdue kwa siku 1 mpaka 3 au 7), stage 2 (umeoverdue kuanzia siku 4 n.k) so ni lazima utapigiwa na namba tofauti kwakua hizo stages zote zina staff tofauti......
 
Dawa ya deni ni kulipa, acha maneno mengi lipa pesa za watu. Kitendo cha wewe kukopa 42,000/= kinaonesha wewe ni mtu wa aina gani. Kukopa 42,000/= kwenye taasisi wakati una contacts 200 kwenye simu yako ni jambo moja, lakini kuja hapa na kulalamika kwamba umedhalilishwa na kwamba eti unatafuta mwanasheria, hilo ni jambo lingine.
 
Hii adha alikutana nayo PS wa ofisini kwetu, tulimshauri atafute mwanasheria akaogopa akaishia kulalamika. ila yeye case yake ni tofauti kidogo, walimdhalilisha akiwa ameshafanya malipo tayari na wao ndio walichelewa kuconfirm malipo.
Mimi nilikopa app inaitwa Jipimiekash tarehe 26, kufika tarehe 28 ananipigia muhudumu wao kunilazimisha nilipe wakati due date ni tarehe 1 nilimind sana licha ya kumueleza anajibu "hiyo tarehe 1 ni ya kampuni,mimi nataka ulipe leo kabla ya jioni"
 
Hiki ndo nilichowafanyia PESA X mbwa wale, nimepita na 80000 yao, na kunishika hawawezi, shenzi kabisa yani mtu ukikaa tu siku tatu bila kuwalipa wanaaza usumbufu wa kingese.

Mpaka waje kudevelop hizo applications zao tutakuwa tumewaliza sana.
details boss
 
haahaha
 
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita.

View attachment 2910966View attachment 2910967

Pia soma malalamiko mengine: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika

Majibu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yazionya Taasisi za mikopo zinazodhalilisha watu ikiwemo kutuma ujumbe kwa ndugu
Pole sana,hao jamaa ni wahuni
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Aisee
 
Back
Top Bottom