KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Inavyoonekana we si mwaminifu hata kwenye maisha ya kawaida,ndo maana kwenye circle yako umekosa hata wa kukupiga tafu hiyo 42 elfu.Jirekebishe kwa hilo, na dawa ya deni ni kulipa acha kulia lia.Ukute hata hizo T&C hukusoma.Nenda kafungue kesi uone kama hawajakushinda hao wapuuzi wa mtandaoni.
 
Ni vizuri awe na watu kumi tu kwenye simu ambao wana tija
 
Mwamba usiwalipe kwa walichokufanyia ni udhalilishaji,wamekuvua nguo.Fikiria watu ulikuwa unaheshimiana nao,alafu wakudhalilishe kirahisi.USIWALIPE,waambie ushawalipa kupitia udhalilishaji waliokufanyia.
Brand yangu ishaharibika
Walipe tu, na omba radhi kwa kuchelewesha
Hapana, sifanyi ivo
 
Dawa ya deni ni kulipa, mwenye tatizo ni wewe hata ukifungua kesi bado itakugharimu tu, ww ulikubali vigezo na masharti, sa tunalalamika nn? Kama ungelipa on time deni lao yote yasingetokea, haijalishi ulikuwa na dharura gani

Mimi sikupitisha dead line, hilo moja.

Mbili hakuna kigezo kwamba nisingelipa wanitangaze kuwa mimi tapeli
 
Huu ni upoyoyo! Yaani utumiwe sms kuwa fulani anadaiwa alafu umlipie pasipo kumsikiliza na yeye kama kweli anadaiwa au ni matapeli ndio wanatuma sms🤔.
 
Ni kweli washitaki kwa kuingilia privacy yako; ukiwa na mwanasheria mzuri watakulipa fidia kubwa kuliko deni hilo. Deni ni jambo lako private inayolindwa na katiba kifungu 16-1 mpaka pale mahakama itakapoamuru litangazwe. Walichotakiwa wao na kukupeleka mahakamani, siyo vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…