Hizo ngonjera wanawachezea nyie wanajua hamfuatilii mambo ya nchi....wamesahau kama hizo njia za kusafirisha umeme ni component iliyopo kwenye mradi tangu day 1 ya mkataba. TAFUTA HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI BAJETI YA MWAKA 2021............... Hii ni sehemu ya kipande cha hotuba hiyo.....
MIRADI YA KUZALISHA UMEME
Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere – MW 2,115
24. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi wa kimkakati na wa kielelezo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere 19 Hydro Power Project (JNHPP) utakaozalisha MW 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji. Gharama za mradi huu ni Shilingi trilioni 6.55 zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.
25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha uchimbaji na ujenzi wa handaki la kuchepusha maji ya Mto Rufiji (diversion tunnel), kuendelea na ujenzi wa bwawa (main dam and spillways), ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels), ujenzi wa kituo cha kuzalishia umeme (Power House) na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (Switch yard). Hadi kufikia mwezi Mei, 2021, jumla ya Shilingi trilioni 2.495 zimelipwa kwa mkandarasi sawa na asilimia 100 ya fedha iliyotakiwa kulipwa kulingana na hatua ya utekelezaji wa mradi iliyofikiwa.
26. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla utekelezaji wa mradi katika maeneo muhimu matano (critical path) hadi kufikia mwezi Mei, 2021 umefikia wastani wa asilimia 52. Hadi sasa jumla ya wafanyakazi 7,243 wameajiriwa. Kati ya wafanyakazi hao; 6,452 ni Watanzania sawa na asilimia 89.1 na kutoka nje ya nchi ni 791 sawa na asilimia 10.9.
27. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2021/22, Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi ambapo kazi zitakazofanyika 20 ni pamoja na kuendelea na kukamilisha: ujenzi wa bwawa (main dam and spillways); ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels); ujenzi wa kituo cha kuzalishia umeme (Power House); na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (Switch yard). Jumla ya Shilingi trilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa katika mwaka 2021/22 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Juni, 2019 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022.
28. Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa mradi huu pamoja na miradi mingine kutafanya nchi yetu kuwa na jumla ya takriban MW 5,000 kufikia mwaka 2025. Katika kipindi hicho mahitaji yetu ya juu ya umeme yanatarajiwa kufikia MW 2,677 hivyo kuwa na ziada ya takriban MW 2,323 na kuweza kuuza umeme nje ya nchi na kuongeza mapato ya Shirika. Aidha, Serikali itaweza kutekeleza azma yake ya kupunguza bei za umeme kwa wananchi.