Taarifa muhimu kuhusu Mradi wa JNHPP zimeshindwa kuwekwa wazi licha ya kutambua kuwa Mradi huu ni wa watanzania na wala sio mali binafsi ya familia ya 'Watu wazuri hawafi"
Ni sababu zipi zilizosababisha watanzania washindwe kuambiwa Mradi utakamilika lini?
Ni sababu zipi zilisosababisha kutokuwekwa wazi uongo kuhusu Madai ya Trilioni 1.5 ambazo Mkandarasi alipaswa kuilipa Serikali kwa kukiuka mkataba na kuchelewesha mradi badala ya mradi kukamilika Juni 2022 hadi sasa mradi haijulikani utakamilika lini.
Spika wa Bunge, Tulia aliyeanzisha hoja hiyo ya mkanganyiko wa taarifa kuhusu kukamilika kwa mradi bungeni Novemba, 2022 amepewa nafasi ya kuongea ameshindwa kuuliza maswali hayo kwa lengo la kumfaidisha nani?
Mpaka sasa watanzania wote wako gizani hawajui mradi utakamilika lini na lini utaanza uzalishaji. Kwanini wanaomundalia Hotuba Mh Rais wameshindwa kuweka time frame ya mradi?
Kwanini Waziri mwenye dhamana ya nishati ameshindwa kuweka time frame ya mradi kukamilika.
Maswali haya yalipaswa kujibiwa siku ya jana
Miradi mingi ya Ujenzi huongezewa muda especially miradi mingi iliyofanyika between 2017-2022.Mwaka 2019-2020 kulikua na Covid 19 ambayo imeathiri perfomance ya sekta za ujenzi dunia nzima. Mwaka 2020-2021 Tanzania mvua zilinyesha karibu miezi 7 mpaka 8 non stop.Kitu ambacho kiliathiri ujenzi wa hilo bwawa na hata SGR pia iliathirika.
Ukiachana na hizo factor, miradi mingi ya ujenzi hua haikamiliki on time, always hua kunakua na extension ya muda either mwaka au miaka miwili kutokana na jinsi mkandarasi alivyotetea uchelewaji wa kazi. Mara nyingi Kipindi cha mwanzo cha mradi (Mobilization period) ndio huwa changamoto kutokana na kwamba wakandarasi wengi huwa wageni, they have to cope na mazingira.
Si ajabu kwa mradi mkubwa kama huu wa bwawa kupewa extension ya muda. SGR lot 1 ilitakiwa kukamilika 2019 au 2020 lakini mpaka sasa timu bado zinakamilisha kazi ndogo ndogo zilizobakia.