Taarifa hizi za Mradi wa JNHPP zimefichwa kumlinda nani?

Miradi mingi ya Ujenzi huongezewa muda especially miradi mingi iliyofanyika between 2017-2022.Mwaka 2019-2020 kulikua na Covid 19 ambayo imeathiri perfomance ya sekta za ujenzi dunia nzima. Mwaka 2020-2021 Tanzania mvua zilinyesha karibu miezi 7 mpaka 8 non stop.Kitu ambacho kiliathiri ujenzi wa hilo bwawa na hata SGR pia iliathirika.

Ukiachana na hizo factor, miradi mingi ya ujenzi hua haikamiliki on time, always hua kunakua na extension ya muda either mwaka au miaka miwili kutokana na jinsi mkandarasi alivyotetea uchelewaji wa kazi. Mara nyingi Kipindi cha mwanzo cha mradi (Mobilization period) ndio huwa changamoto kutokana na kwamba wakandarasi wengi huwa wageni, they have to cope na mazingira.

Si ajabu kwa mradi mkubwa kama huu wa bwawa kupewa extension ya muda. SGR lot 1 ilitakiwa kukamilika 2019 au 2020 lakini mpaka sasa timu bado zinakamilisha kazi ndogo ndogo zilizobakia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…