Taarifa kutoka TRA kuhusu kubadilisha umiliki wa chombo cha moto

Sasa mkuu unashindwa kulipa parking fee ya sh.500?
 
Mukoko Tunombe Oops!! Business Digenda Shoti, Iweee
 
Sasa mkuu unashindwa kulipa parking fee ya sh.500?
Shida sio kulipa shida ni kuandikiwa bila kujijua una deni sababu inaji compound on daily basis😅 sasa laiti nisingejua siningejikuta niko kwenye deni ambalo sijui hata parking ya lini nilipigwa hivyo
 
Unaweza kuandikiwa parking fee hata kama uko kwenye foleni tu.
 
Tanzania Nchi ngumu sana sijui wamesomea wapi na tafiti zao za hovyo wenzetu wanarahisisha kuhamisha umiliki wa vyombo vya moto sisi tupo busy kukomaliana na hivi vitu chakavu..
 
Wrong start!
Kazi ya TRA ni kukusanya kodi sio kukagua gari. Wala sio kubuni kodi au TOZO mpya bila kupitishwa na Bunge.

Hiyo kazi ya ukaguzi kama gari ni la wizi ifanywe na polisi.
Maana yake polisi (walio na data au taarifa za magari yaliyoibiwa) ndiyo watoe clearance report kwamba gari husika sio la wizi.

Mnapotaka kila taasisi moja ifanye kazi zisizo zake mnasababisha mianya ya rushwa, uonevu, usumbufu na unnecessary red tape.

Kwamfano niko kijijini nimepatwa shida ya dharura nisimuuzie mali yangu rafiki yangu, ndugu, au jirani yake mpaka TRA wahusike! M/Kiti wa serikali ya mtaa au Wakili/Hakim hawatoshi?

TRA itafika mahali watataka wawepo kila unaponunua baiskeli, bodaboda, bajaji, nyumba, cement, matofali, mabati nk. Eti kwasababu huenda hicho kitu ni cha wizi!
 
Bado kuna shida waliowekwa hawajui jinsi ya kuongeza mapato.Nasikitika na nchi yangu. Sidhani kama aliqualify kwenye hii taaluma au ndio zile paper zinazovuja huko ajira portal.

Hapo kutakuwa haina haja ya wanasheria. Kazi ya kukagua gari na kuwepo kwa wanauhuziana linamalizwa na vehicles inspectors pamoja na wanasheria sio TRA.
Natabiri utenguzi katika TRA.

Loo nchi yangu tunafeli kwenye selection
 
Binafsi naona utaratibu ni mzuri, sababu una faida NYINGI kuliko hasara. Tatizo ni namna ya utekelezaji tu..system zao zitakuwa fair enough? Na kama kupata details za mwenye kadi itakuwa ngumu means zoezi litakuwa gumu..lakini Kwa mnunuzi details ZAKE ni rahis , na kwakweli inapendeza ukinunua UPATE kadi Yako , penye shida ni mkataba wa mwanasheria Tena mwenye kutoa EFD receipt, ...unajua Kwa MDA mrefu baadhi ya watu wali ignore ubadirishaji wa umiliki..watu wakishapeana kadi halisi basi !!! Sasa mnyololo wa kuuziana sometimes UNAWEZA Kuta ni mrefu ..YAANI tokea Kwa muuzaji wa kwanza mpaka wa mwisho ..UNAWEZA Kuta wewe ni mmiliki wa 5 huko, aliyekuuzia nae hakubadiri, nae hakubadiri pia....basi kumpata yule wa AWALI ni shida...wangesema LABDA utaratibu uanze Sasa (japo Sio rahisi kujua kama ni lini ) ..ila dhana nzima ya kubadiri umiliki ni mhimu na ni vema Sana hata kama gari ni ya 1.5ml[emoji3]
 
Sioni kama hawa TRA wanakubaliana na TEHAMA SYSTEM au impact of saving time! Ninawasiwasi hata databases huwa haziko updated to reflect! Manunuzi mengi dunia ya sasa ni online systems na ndio sytem inayoingiza hela za hapo kwa hapo yaani chap chap! Kwa maamuzi mliyofanya sanasana mnatengenezavmianya ya rushwa, msongamano kwenye vituo vyenu vya TRA na watu kuambukizana corona tu na jinsi mlivyo slow 🐌 mara excuses za mtandao uko down oooh mara mtandao haujarudi! Kwa hili naweza kusema mmekurupuka na hamja crack vichwa vyenu!
Tumieni fingerprint system za vitambulisho vya NIDA au PASSPORT , kusanyeni hayo madeni au hizo kodi kupitia plate number za magari kwa kutumia scanners za police huko barabarani watu walipe kwa control number ! Muuzaji na mnunuzi wajaze online form za ubadilishaji jina kila mtu alipe kodi yake! Mnunuzi aje tu na recepts zote kuchukua card yake ya gari na kazi yenu itakuwa ku double check na ku hakiki mtu anaondoka na kadi yake!
Ni mtazamo wangu tu
 
Hakuna haja ya kubadilisha, ukishamuuzia asepe nalo tu......wakimkamata unawambia nilimpa kama zawadi, inaisha hiyo? halafu kama gari ilishaalipiwa kodi zote wakati inaingizwa nchini, kodi nyingine mnazotafuta kwenye gari chakavu ni zipi hasa, yaani akili za bongolala ni shida sana.....
 
kipindi cha Front Page
Vipindi vingi kwenye station zetu za radio na TV vina majina ya kigeni na hasa kiingereza.
Je sababu ni nini wakati mazungumzo yanakuwa ya kiswahili mwanzo hadi mwisho?
Je huko Ulaya na Marekani wenzetu wamevipa vitindi vya station zao majina ya Kiswahili?
Je kuwa na majina ya kiingereza kwa vipindi vya TV na redio kuna tija gani katika ustawi wetu?
Je ina maana Kiswahili hakina majina yanayofaa kwa vipindi hivyo?
 
Japo maisha siyo kutesa kila siku ila pesa ndiyo kila kitu...

Cha umuhimu gari iwe kwenye system kihalai, uwe na mkataba mengine wanapitisha tu...
 
Mmiliki awepo na mnunuzi awepo ,Ina maana mmiliki akinipa copy ya kitambulisho chake haitoshi ?
 
hahahhahah mkuu umenichekesha hapo kwa wahindi gari anakupa ila kadi hakupi mpaka mkabadilishe....waoga sana wa masekeseke wanawajua wabongo akili zao.
 
Hakuna hata haja ya kupelekana polisi wala nini,hii kesi inaishia hapo hapo kwa maana jina la kwenye kadi lazima liendane na taarifa za mlipaji wa Bima ya hiko chombo cha moto.

Omba tu isifike huko mzee.
 
Na wewe unapotumia neno TV je hakuna neno la kiswahili linalotumika kwa kitu jicho ?
Bila shaka ni Luninga, sasa kwa nini hukutumia we .com ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…