DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
- Thread starter
- #101
Kusema eti wachezaji wajitokeze wakosoe ni kuwatwika mzigo usio wao na pia bado mtabisha. Mwameja alienda Azam TV na medali yake ya CAF ila mpaka leo mnaita bonanza la Abiola, hapo sijaongelea Rais Samia kuwaambia huku timu nzima ikiwa mbele yake kuwa nyie siyo wa kwanza kucheza fainali ya shirikisho ila mnaendelea na huo ubishi.Nadhani kama kungekuwa na uongo katika ili kuna wachezaji waliopo hadi leo wangekuwa mstari wa mbele kukosoa, watu wa pili ni mashabiki wa mpira waliopo hai hadi sasa na wa mwisho ni bodi ya ligi pamoja na TFF wakilimalizia kwa kupinga takwimu za Yanga kama zina uongo.
Hizo source zina nukuliwa pia haziwezi kutumika kama marejeo ya moja kwa moja kwasababu kuna zingine zina mapungufu kwasababu zinaweza kuingizwa taarifa ambazo sio sahihi na zingine pia zinaonesha wazi kukosa taarifa zilizokamilika.
Mfano source aliyoteta mleta uzi kuna mahali zimeandika unknown hii ina maanisha kuwa taarifa au ukusanyaji wa taarifa haukuwa katika ukamilifu wa asilimia 100.
Pia ukiingia kwenye website ya hio source kuna N.B wameweka kuhusu muundo wa ligi kuwa ligi ya muungano kwanzia mwaka 1982 hadi mwaka 2003 ambapo wameweka wazi kuwa top teams kutoka mainland (Tanganyika) walikuwa wakicheza vs top teams kutoka Zanzibar.
Hapa maanake kulikuwa na ligi kuu Tanzania bara ( Tanganyika)
Ligi kuu Zanzibar kisha ligi ya muungano.
Walichoandika hapo kwanzia 1982 hadi 2003 ni mabingwa wa kombe la muungano na sio wa Tanzania bara (Tanganyika)View attachment 3288808
Mnataka mashabiki waliokuwepo wajitokeze waseme. Mimi hapa ni mmoja wapo na 1995 nilikuwepo, mbona mnanibishia?
Mnachotakuwa kufanya ni nyie mnaotuambia mmechukua ubingwa mara 30, mtuorodheshee hiyo miaka na muwe na chanzo cha taarifa zenu. Kuna mwenzio kaweka source ya Wikipedia ambayo inataja miaka 6 ambayo inajulikana Yanga haikuchukua ubingwa ila nayo imeorodheshwa.
Nina uhakika hata akijitokeza kiongozi wa TFF akatoa taarifa kuhusiana na hili suala zinazopingana na nyie mtamshambulia kuwa ametumwa na Simba.