Wanasema "hauna haki ya kuongea kama kwanza haujafanya utafiti wa hilo unaloongelea".
Taasisi ya R.S.S.S.F. (Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation) ni taasisi kubwa duniani ambayo imekuwa inafanya kazi ya kutafiti na kuhifadhi takwimu za soka duniani kwa miaka mingi. Hii si taasisi ya vichochoroni na ina wawakilishi dunia nzima wanaosaidia kukusanya na kuchakata hizi takwimu.
Katika tovuti ya R.S.S.S.F wameripoti kuwa Yanga imewahi kuchukua ubingwa mara 25 tu. Katika rekodi zao, Simba imechukua ubingwa mara 22.
Katika miaka ya hivi karibuni, Yanga imesambaza propaganda kuwa ni bingwa mara 30 hadi katika vile vitenge vyao wakaweka nyota 3 na wakadanganya wenzao kuwa nyota 3 zinamaananisha ubingwa waliobeba mara 30.
Nadhani kulikalia hili kimya ni moja ya favour aliyowafanyia Rais wa TFF Wallace Karia halafu leo wanamtusi na kumuona hafai.
Nimeambatanisha hapa chini list ya mabingwa kuanzia 1921 hadi 2024 kutoka tovuti ya R.S.S.S.F.
View attachment 3288050
Ukipinga pinga kwa takwimu rasmi kutoka chombo kinachoaminika.