Taarifa Rasmi kwa Umma: Yanga ni bingwa mara 25, Simba mara 22

Kusema eti wachezaji wajitokeze wakosoe ni kuwatwika mzigo usio wao na pia bado mtabisha. Mwameja alienda Azam TV na medali yake ya CAF ila mpaka leo mnaita bonanza la Abiola, hapo sijaongelea Rais Samia kuwaambia huku timu nzima ikiwa mbele yake kuwa nyie siyo wa kwanza kucheza fainali ya shirikisho ila mnaendelea na huo ubishi.

Mnataka mashabiki waliokuwepo wajitokeze waseme. Mimi hapa ni mmoja wapo na 1995 nilikuwepo, mbona mnanibishia?

Mnachotakuwa kufanya ni nyie mnaotuambia mmechukua ubingwa mara 30, mtuorodheshee hiyo miaka na muwe na chanzo cha taarifa zenu. Kuna mwenzio kaweka source ya Wikipedia ambayo inataja miaka 6 ambayo inajulikana Yanga haikuchukua ubingwa ila nayo imeorodheshwa.

Nina uhakika hata akijitokeza kiongozi wa TFF akatoa taarifa kuhusiana na hili suala zinazopingana na nyie mtamshambulia kuwa ametumwa na Simba.
 
Tuanze na wewe shabiki uliokuwepo kipindi hiko hadi leo, je unakubaliana na hiyo source uliyoweka kuwa muundo wa ligi ulikuwa unachukua top teams toka ligi ya Tanganyika na top teams toka Zanzibar kisha zinakutana katika muungano, kwanzia mwaka 1982 hadi 2003? Swali langu linahitaji majibu ya 'ndio'au 'hapana' kama hukubaliani nalo na sio easy au maelezo kibao.

Tukilimaliza hili ndio tuje kwenye hiyo hoja ya CAF Cup Simba iliyovaa medali.
 
Mjadala nimeanzisha mimi na nimesema inabidi upingwe kwa takwimu kinzani na siyo porojo.

Kama source ya hizo mara 30 zenu ni Wikipedia, nimeorodhesha miaka 6 ambayo imeorodheshwa kama Yanga imechukua ubingwa ambayo siyo sahihi. Ukitaka source nyingine inayoniunga mkono kuhusu hilo naweza kukupa. Na wewe nipe source zako za kuaminika au na wewe source yako ni Wikipedia ambayo hata mimi naweza kuingia sasa hivi nikaedit?
 
Narudia tena.. tulianza kuhesabu pamoja tangu na tangu na kwamba miaka yote tulikubaliana kwa kila mmoja makombe alokusanya,, swali je huo udanganyifu umeanza baada ya yanga kuhesabu la 30 au la? Mana toka nmeanza ufahamu kwa kufuatilia mpira wamiguu nliona waandishi na watangazaji wakihesabu makombe kwa timu zote tena wanaainisha ni kombe la ngapi mpaka kufikia Leo
NB: NADHAN HATA MANGUNGU ANAJUA NDO MANA YUPO KIMYA
 
Hatupo zama za kurithishana historia kwa midomo, tumeshatoka huko. Ndiyo maana ili kupata historia yenye uhakika zaidi, wenye akili wakakaa chini wakachukua historia hizo na kuziweka katika maandishi na ndiyo tunapata kanzidata kama hii ya R.S.S.S.F. Sasa nyie mnaopinga, leteni kanzidata na takwimu zinayopingana na hiyo ili tufanye uwiano siyo mambo ya kusema tulikuwa tunaambiana na kuhesabu pamoja!
 
Hizo not known 5 ni za Yanga Mkuu.
 
Ndio hilo SAYVILLE na hata mimi nimegusia, kuna haja wakaja front kulizungumzia hili kabla huko mbele watu hawajapaza sauti ikaleta tafrani.

Hiko chanzo chako kinatambuliwa na TFF?


Hizi takwimu umeokota wapi😀😃
Kwa wale wanaopendelea kutumia Wikipedia kama source yao, hii hapa page ya Wikipedia ya Yanga inasema Yanga ni bingwa mara 25.

 
Wewe si umeleta source tunaijadili source uliyoleta? Tunaanza na source uliyoleta ila bahati nzuri wewe mwenyewe umekiri kuwa ulikuwepo kipindi hiko, sasa tuanze na kile source ilichokiandika kwenye N.B kwamba ligi kuu ilibadilika muundo kwanzia mwaka 1982 hadi 2003 kwa kuchukua top teams kutoka ligi ya Tanganyika na ligi ya Zanzibar kisha kukutana katika ligi ya muungano. Ili mjadala uende vyema nataka ukiri je unakubaliana source yako kuhusu jambo hilo ama lah?
 
Mimi sipo kwenye Wikipedia, nataka tujadiliane kupitia hiyo hiyo source yako uliyoleta wewe tuanzie hapo kwenye N.B
Acha porojo, leta source yako ya kuaminika inayopingana na hiyo source yangu.

Mpaka nimeleta hapa ina maana nakubaliana na kilichomo katika source hiyo kuhusiana na idadi ya ubingwa wa Yanga. Inachotakiwa ni wewe kuipinga hiyo source siyo kwa porojo bali kwa kuambatanisha source inayokinzana na hiyo!
 
Acha porojo, leta source yako ya kuaminika inayopingana na hiyo source yangu.

Mpaka nimeleta hapa ina maana nakubaliana na kilichomo katika source hiyo
Sawa kama unakubaliana nayo, naomba njoo na list ya mabingwa wa Tanganyika kwanzia mwaka 1982 hadi mwaka 2003 kwasababu hiyo source yako kwanzia mwaka 1982 hadi 2003 imeweka mabingwa wa kombe la muungano ndio maana Malindi na KMKM wapo kwenye hiyo list.

Kwavile source imekiri kuwa kulikuwa na ligi ya Tanganyika na Zanzibar kisha wanakutana kwenye muungano, hivyo lete takwimu ya mabingwa upande wa Tanganyika 1982-2003
 
Kwa hilo nakubali niliteleza, dhamira yangu ni kusema Uefa cup ambayo huo msimu wa 2009/10 ndio yalibadilishwa jina kuwa Europa sio winners cup ambayo ni discontinuated tangu 1999.
Uefa cup na winners cup zilikua scrapped,likaja shindano jipya europa, arsenal alicheza na galatasaray kama kumbukumbu ziko sawa huyo europa 2000 au 2001 final akapoteza
 
Tukubaliane kwanza, kumerge ni kufuta au kuunganisha?
CAF hawakusema wame-merge winners cup na caf cup,ndiyo maana hawahesabu kombe la winners cup la ahly 1993 na caf cup la stella 1993 kuwa ni kombe la shirikisho
 
CAF hawakusema wame-merge winners cup na caf cup,ndiyo maana hawahesabu kombe la winners cup la ahly 1993 na caf cup la stella 1993 kuwa ni kombe la shirikisho
Kwa hiyo unakana vielelezo ulivyoambatanisha wewe mwenyewe vinavyosema CAFCC imetokana na merger ya mashindano hayo mawili?
 
Mbumbumbu huyo hanaga hoja zaidi ya ubishana tu, chanzo anachotumia sijui kama kakipitia kikamilifu kuona kama kulikuwa na ligi ya muungano na ligi ya Tanzania bara ndani ya msimu mmoja. Na Yanga huwa wanasema ni mabingwa mara 30 wa ligi ya Tanzania bara.

View attachment 3288983View attachment 3288984
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…