Taarifa ya 2022 ya ufanisi wa bandari duniani: Djbouti 26, Berbera 144, DSM 312 na Mombasa 326

Hivi hiyo link uliyotoa kwenye Uzi ndio yakusema Rais awape DP World Bandari?
Maelezo yanajieleza vizuri kuwa Dar es Salaam Port imeshika nafsi ya 312 wakati Mombasa Port 326 maana yake bado tumewaacha wakenya kiufanisi na hakuna mahali wametaja DP World kama ulivyoitaja kwenye Uzi wako.
Usipotoshe ukweli unless hujaelewa ulichowasilisha.
 
Hatuwezi kuzuiwa na wajinga wa CHADEMA kufanya mambo makubwa kwa maslahi ya watu wengi
Katibu mwenezi wako ameshakiri mkataba haupo sawa,
Tutajie hayo mambo makubwa yanayoletwa na DP World
 
Je port ya kwanza hadi ya tano zipo chini ya operator gani?




Mngetangaza tenda mkashindanisha kampuni si ajabu mngepata isiyokuwa na mambo ya bogus treaty.

Hizo top four ndiyo vidume wa hii sector na kwa jinsi Dar port ilipo kijiografia,msingemkosa hata mmoja.
 
Nimekuwekea link usome, uelewe, na utaona hata kama DSM imwkuwa ya 312 bado Mombasa iko na volume kubwa na kwa marekebisho yanaenda kufanyika hatutawafikia.
mfano
Mombasa in gati 19 (makasha 4, mafuta 2, mizigo 12) ukilinganisha na DSM 12 (4,2,10).
Mombasa inahudumia 35,000,000 mt kwa mwaka ukilinganisha na DSM 14,000,000 mt za mizigo.
Ninakuomba tena usome na uchambue utaona
 
Serikali ya CCM inafanya inachopaswa kufanya- kama kuna shida waisubiri kwenye uchaguzi 2025
Wakati huo bandari itakuwa imeshaenda,si bora wanavyoropoka sasa hivi ili tuone pa kurekebisha? Mnatuchanganya sana sisi wananchi,hao unaowaita chadema waliupinga mkataba kutokana na kuona kuwa kuna vifungu kadhaa haviko sawa,na wakaviainisha,sisi wananchi tukakaa mkao wa kula tusikie mkiwajibu kuhusu utata wa vifungu hivyo,badala ya kusikia mkiwajibu kwa hoja tunawaona mnarusha tu vijembe,kejeli na vitisho,vitu ambavyo hatukuvitegemea,tulidhani majibu ya hoja zao yasingejaa hata karatasi moja ya A4,badala yake tunaona mkifanya mikutano nchi nzima bila kujibu hoja zao,bado tunasubiri,ila mkiamua kufanya lolote kwa kuwa tu nyie ndiyo wenye dola basi hewallah,hatuna cha kuwafanya.
 
CCM na serikali yake walishasema hakuna mktaba kuna maelewano; kaja yule Mh. Mwambukusi kwenye baa anasema kuna mkataba; mahakanani anasema hakuna mkataba mpaka mh. jaji akalazimika kusema kuwa anacgeza vizuri mahakamani na kwenye siasa.
Mkuu hapa hatuchezi siasa wala kesi mahakamni - hapa tujadili uhalisia- hatuli siasa mkuu
 
DPW nafikiri walishatimiliwa Djibouti .... Kesi iko mahakani. Kwa sasa kuna mchina.

Anyway, kuwapa DP world litakuwa ni kosa la kiufundi. Hii ni kwa sababu DPW wanachotafuta ni control ya Bandari zote za ukanda wa Africa ili wao ndiyo wawe Kidume peke yao na kutufanya sisi tutegemee Bandari yao maisha yetu wote. Hiyo ndiyo maana ukomo wa mkataba haujawekwa. Kwa vile DPW wapo Djibouti na pia Beira haitakuwa rahisi waipendelee Bandari yetu na kuziacha hizo nyingine.

Naamini kuna makampuni ambayo yako more efficient kuliko DPW hivyo kama tungetangaza tender yangeweza kumpiku DPW ....!!

In my opinion, hatuna haja ya kutumia kampuni za nje. Tayari somo tulishalipata kutoka kwa TICTS ..... tunajifariji kutegemea kuwa kutakuwamatokeo tofauti sana DPW wakija. Kama ni wizi bado TRA watakuwepo kupokea ushuru. Unless, DPW wapokee mapato. Tatizo letu kubwa la kukosa efficiency ninasababishwa na ukosefu wa wataalamu hapo bandarini. Kama serikali itaaamua kuwekeza kwenye expertise hilo tatizo litaondoka. DPW wenyewe hao Waarabu wa UAE hawafanyi hizo kazi .... wameajili watu. Kwa nini na sisi tusiajili wataalamu na kuwalipa watufanyie kazi yetu....!!?
 
Uko sahihi na maneno yako yanaungwa mkono na link niliyoweka, soma tu utaona
Perhaps the only differentiators Mombasa can capitalise on to better its proposition and beat Dar squarely lie in two realms:

Infrastructure at the port and its hinterland and efficiency of human capital deployed at the port and on the corridor it serves.
 
Utahira wa kina juma lokole, Zembwela, kitenge na majizi ya CCM pelekeni majengo ya CCM mkawekeze milele sio bandari zetu.
 
Mkuu ni kweli waliwatoa on resource nationalization madness which always has a price tag. Kufanikiwa kwao largely kunatokana na development alizofanya DP World
 
Utahira wa kina juma lokole, Zembwela, kitenge na majizi ya CCM pelekeni majengo ya CCM mkawekeze milele sio bandari zetu.
Mkuu famila yako inawapenda na kauangalia ujinga wao- mtu anayeangalia wajinga na kufurahi definitely atakuwa mjinga zaidi- pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…