Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Na hii ndio taarifa yake

Habari ya asubuhi wana familia.

Sisi tunaumwa, nilipata ajali mbaya tarehe 5 October na ilionekana nimepata fracture kwenye mguu, siku tatu mbela ikaonekana nimepata clavicle dissociate (mfupa wa bega ulipishana.

Na nilimuona bingwa wa mifupa tukapata matibabu (arm sling na figger of 8).

Niliendelea kupata nafuu hadi tarehe 24 ghafla nilianza kupata maumivu mapya upande wa kulia kama kichomi kikali, tulipata rufaa na sasa tupo muhimbili Sewahaji 17 room 12.

Nimetobolewa pafu baada ya kugundilika lili pata kuvia dam na uzembe ulifanyika kwa kutokugundua tatizo hilo na nikakaa na shida hiyo kwa wiki 3.

Kwakifupi hatuendelei vizuri sana lakini nashkuru Mungu naendelea kutoa damu kwenye pafu na sasa nikama inatoa usaha.

Leo kuna vipimo tutafanya pamoja na kukaa na wataalam, kama ikiwa bora zaidi tunaweza sogea kwa nchi yenye wataalamu zaidi ili tupate kupona.

Naomba mtuweke kwenye maombi n Mungu atawabariki sana.

NB: Kwenye ajali hiyo mbaya iliyohusisha madereva wawili pamoja na Ushimen! Dereva wa kwanza ambaye ndie alisababisha ajali hiyo mbaya alikufa pale pale.. Dereva wa pili aliyekuwa na Ushimen alifariki siku tatu baadae

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuepusha ndugu yetu na kifo.. Tumuombee nafuu ya mapema
Jamaa simpendi kichizi.
 
Nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunipigania na hatimaye nimefika hapa nilipo, kwani haikuwa kazi rahisi na wala si kwa ujanja wangu wala uwezo wangu mimi kama binadam ambae hajakamilika.
Pili napenda kutoa shukrani zangu kwa JamiiForums na members wote waliokuja kuniona nikiwa nimelazwa (ingawa najua wengi walipata taarifa kwa kuchelewa.
Nasema asante kwa members wooote mlio nijulia hali hapa jamvini, na hakika nimeuona upendo wenu ulivyo mkubwa. Na....Mungu awabariki sana!!!!
 
Amen kaka ugua pole namin utazid kuimarika.
 
Tangu ulipo fungua uzi kwamba haunipendi nilitambua mkuu, wala usitumie nguvu kubwa..[emoji1787]
Lakini kwangu mimi nina amani sana kwaku najua ninatenda mengi yalio mema "lakini sijakamilika"
Kaka naambiwa na kusoma mengi umewagusa wengi humu kwa namna moja ama nyingine natamani ningelijua mapema hilo pengine ningelisaidika.kama wengine.
 
Back
Top Bottom