Taarifa ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule za kanisa katoliki Tanzania


Hizo shule ni biashara ya nani, waumini mnashirikishwa katika ujenzi. Shida ada zao wakatoliki wengi hawazimudu gharama za ada, kanisa lizingatie Hali za waumini wao. Ikiwezekana kuwe napunguzo Kwa waamini wakikatoliki
 
Hongera kanisa katoliki. Taasisi, serikali na wengine waige mfano huu

Waige nini sasa
hapo watoto wanachujwa sana; Shule zao zinataka wale ceam tu...
Sasa shule zote zikichuja, wale wa maksi za kawaida ambao ndio wengi watasoma wapi?
 
Basi mkuu hizo shule zimejengwa kwa misaada ya watu wa Marekani.
 
Hospitali za umma zimejengwa kwa kodi za wananchi,SGR imejengwa kwa kodi za wananchi,ATCL ipo pale kwa fedha za walipakodi ambao ni sisi,vipi umewahipeleka hoja kama hiyo sehemu tajwa?
After all ada za shule za wakatoliki ni ndogo sana,ujilinganisha na akipatacho mtoto pale.Jenga hoja nyingine.
 
Tofautisha vitu vya umma na vitu vya kikundi cha watu wenye malengo yao. Umma hauna quid pro quo. Dini ni sawa na kikundi kama saccos, ni muunganiko wa watu flani wenye malengo ama mtazamo ama imani flani inayofanana, hivyo chochote kinachofanywa na watu hao lazima kiwe kwa maslahi ha hao watu kwanza. Sasa inawezekanaje uchangishe hao watu ujenge miundombinu halafu hiyo miundombinu isiwafadishe hao wajenzi ama watoa fedha(investors) badala yake uweke vingezo vya vingumu ambavyo investors hawawezi kumudu kutumia hiyo miundombinu? Huo ni utapeli ama wizi, kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Hao watoto wanapata nini ambacho watoto wengine hawapati kinachozidi thamani ya fedha zao walizolipa ada?

Hoja hapa sio watoto kupata faida kubwa, hao watoto ni wa wale original investors ama ni wa watu wengine?

Hii hoja sio rahisi wewe kuielewa ukija kwa mtazamo wa kidini. Dini hupumbaza sana, ni ulevi mkubwa kuliko cocaine.
 
Hawajui hiyo survival for fittest, wako occupied na DELUSION za after life i.e Every muslim will be given a kingdom as their property and a palace as their house with angels as their servants🙁 , why suffer on planet earth😛
 
Kuna Marian Boys mbili, hii na ile ya Bagamoyo?
Ni hiyo hiyo. Msichofahamu wadau wengi ni kimoja tu! Bagamoyo kwenye mgawanyo wa Majimbo ya Katoliki, iko Jimbo la Morogoro! Na Katoliki hawana Jimbo la Pwani! Isipokuwa Jimbo kuu la Dar es salaam, Jimbo la Morogoro (na hiyo Bagamoyo ikiwemo), nk.
 
Waige nini sasa
hapo watoto wanachujwa sana; Shule zao zinataka wale ceam tu...
Sasa shule zote zikichuja, wale wa maksi za kawaida ambao ndio wengi watasoma wapi?
Wanatakiwa wakasomee elimu ya ufundi stadi, kucheza mpira, kuimba, nk.

Mbona jambo hili hata Mwanafalsafa mashuhuri kabisa wa Kigiriki (Plato) alishawahi kuwagawa hawa viumbe katika makundi matatu! (1. Golden Boys, 2. Silver Boys, 3. Iron Boys!!). Tena ni miaka hiyo ya BCE!!! Kwa hiyo hakuna namna nyingine Sheikh.
 
Semeni shule za kanisa Katoliki kwanini mnafichaficha, by the way lengo la ujumbe huu ni nini?
Taarifa kwa umma but pia lengo lingine, kanisa linajaribu kuwaonesha wateja wao kwamba hawakukosea kuchagua kupeleka watoto wao kwao. Ninacho wapendea Wakatoliki, wanaendesha mambo yao kitaasisi, kisomi kabisa. Yaani wana hadi idara ya elimu, na hi ndio imetoa taarifa yao kwa umma, kama serikali yaani. Hawa jamaa wamejipanga, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, daa
 
Nasemaje mi mwanasheria sinaaa.........lakini kwani hata raia namba moja naye si aliruka ruka tu mpaka kufika kwenye d.a.k.i.t.a.r.i.............miaa au nasema uwongo jamani
 
Semeni shule za kanisa Katoliki kwanini mnafichaficha, by the way lengo la ujumbe huu ni nini?
Ni taarifa tu kwa wadau wa eliminate,wazazi, walezi, wanafunzi wenyewe waliomaliza elimu hapo na hata ikawa ni tangazo la biashara kwa wanaotaka kujiunga na hizo shule.
 

Hata hivyo mtoto kupata nafasi shule za Katoliki ni hadi awe na pass za juu sana, Kama mtoto anapass za kawaida asitegemee kupata nafasi huko. Hata sijui kwa nini wanajivunia kufaulisha wakati wamechukua wanafunzi magenius ambao wanauwezo wa kufaulu vizuri kwa msaada wa kawaida tu wa mwalimu....
 
Ni hiyo hiyo. Msichofahamu wadau wengi ni kimoja tu! Bagamoyo kwenye mgawanyo wa Majimbo ya Katoliki, iko Jimbo la Morogoro! Na Katoliki hawana Jimbo la Pwani! Isipokuwa Jimbo kuu la Dar es salaam, Jimbo la Morogoro (na hiyo Bagamoyo ikiwemo), nk.
Kuna jimbo la Mafinga?
 
Punguzeni ada maana hizo shule zimejengwa Kwa sadaka za waumini cha ajabu wao wanashindwa kuwasomesha watoto wao hizo shule
 
Semeni shule za kanisa Katoliki kwanini mnafichaficha, by the way lengo la ujumbe huu ni nini?
Lengo ni kuonyesha kuwa ''usione vinaelea, vimeundwa''. Kuna watu huwa wanapiga kelele sana kuwa nchi inaongozwa na mfumo kristo kwa sababu kila sehemu unakuta wakristo bila kujua kuwa taasisi zao zinafanya kazi nzuri ya kusomesha wanafunzi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…