Kimantiki na mifano ipo nchi nyingi, shirika lolote la Kiserikali likiwa kubwa sana ni lazima litawanywe uendeshaji wake ili lisiwe kama serikali ndani ya serikali.
Tanesco kwa viwango na jiografia ya Tanzania ni shirika kubwa sana kuweza kuendeshwa kutokea makao makuu moja na DG mmoja. Ni vyepesi sana kutumika kufanya hujuma, japo iwe ya mkitengo kimoja tu, itaathiri shirika zima.
Suluhisho pekee ni kulikata viande vipande vitoke vikam[uni vingi vinavyojitegemea na uhusiano wao utakuwa wa kibiashara tu. Hakuna zaidi.
Niliwahi kupendekeza hili miaka mingi sana nyuma.
Tanesco ufanyike utaratibu wa kulivunja vunja. Nje ya hapo tutasewka na umeme maisha. Hata tuzalishe umeme zaidi ya tunaouhitaji, bado gtugtakuwa na kukosa umeme na hakuna wa kumwajibisha kwa haraka. Tutabadili mawaziri, tutabadili ma DG, tutafanya kila namna, ni mzigo mkubwa kuliko wabebaji.