Tabata, Dar: Anayedaiwa kutaka kuiba bodaboda na kujeruhi ateswa kwa kukanyagwa na gari

Tabata, Dar: Anayedaiwa kutaka kuiba bodaboda na kujeruhi ateswa kwa kukanyagwa na gari

Rule of law. Utawala wa sheria.

Shida ni kwamba akikamatwa akapelekwa kunakostahili anahonga anarudi tena kufanya yaleyale.

Utakuta umenunua pikipiki kwa mkopo una marejesho yanakusubiri halafu pikipiki imeporwa huko
 
Tulikofikia si pazuri nafahamu hawa wezi hawana utu wanaweza kuua hata ndugu sa babu ya kitu kama pikipiki.
Je huyo aliyekuwa anasikika kwenye video amezaliwa na mwanamke au kajizaa? Ana mama, shangazi au dada huyo?

Tufike mahali tujitafakari tunapotoa maneno ya matusi. Je huyo aliyetoa matusi mbona hajasema Mb.... ya baba yake?
Sitetei mwizi nasikitishwa na maneno ya mtoa video.
 
Kaka usihangaike hata kuiangalia hiyo video na usiitafute utaumia sn.Me nimeiangalia jana sipo sawa mpaka leo.Jamaa anakanyagwa na gari akiwa mzima mzima.Anapiga kelelee sn za kilio cha uchungu cha kifo.Hata niibiwe vip sina ujasiri na unyama wa kufanya vile kwa binadamu mwenzangu.
Utakua last born nn [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo ndio demokrasia ambayo jamaa wanataka,

Yaani mtu afanye tu anavyojisikia.

Hakuna utawala wa Sheria.
 
Kama hayajakukuta lazima uone huruma, aise hapo nyuma niliapa sintakuja kupiga mwizi ila siku waliiba yangu, kisha wakaja wakampiga risasi mdogo wa rafiki yangu.. Niliapa siku ya kukamata nitashiriki, hapo ni vile sikuwepo nahisi nami ningekuwa mmoja wa kufanya vile..

Wezi wa pikipiki ni waduwanzi mnoo, wanamtoa mtu uhai kwa machuma ambayo thamani yake haizidi MILIONI.
 
Huwezi ukaelewa ila uvunjaji wa Sheria umeongezeka Kwa kipindi kifupi mno,
Hata enzi za yule uvunjaji wa sheria ulikuwepo
Uhalifu ulikuwepo labda kama wengine mlikuwa Hammond

Ova
 
Back
Top Bottom