Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Napenda kukaa siti ya mwisho kwenye kona kabisa(benchi la ufundi),. Af dereva atembeze kiatu kwelkwel.
Sipendi kukaa na mtu mjuaji wa mambo.

Be like "oya unapaona hapa, yale ndo majabali ambapo wajerumani waliyatumia kama maficho ya dhahabu walizotuibia mwaka 1927. Wakati huo ..........." Wanakera sana.
 
Wanaokaa dirishan halaf hawapendi kufungua dirisha muda wote anafunga kioo sipendii
Kukaa na wazee,na wenye watoto sipendii

Hahaha...

Au mtu anakaa dirishani halafu kila mara anaanza kukuuliza hapa ni wapi?

Mimi huwa nawajibi simple tu, tembea na Atlasi
 

Mpe namba ya kamanda fulani kikosi maalumu, zile namba zao huwa public...

Tafuta ya mmama mmoja hivi mpe...
 
Tupande ndege muache umaskini huo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Kwenye ndege utakaa mwenyewe kama ni business class...lakini kule siti zetu za kajamba nani ni kama basi tu...

Tena bora kwenye basi unakaa na mzigua au mmasaai unaweza kummudu, imagine umekaa na vichina vile vinajamba jamba hovyo we utajulia wapi jina la ushuzi kwa kichina...

Imagine unanyanyuka toka Dar/Nairobi/Addis, Dubai kwenda Peking, NYC etc non stop flight, lazima utakaa na mtu au watu muda mrefu tu...
 
[emoji23]
Hasa sisi wembamba ndio unakuta tunabanwa hadi basi.
Dawa ni kuinuka na kukaa upya..nikiinuka nikikaa nakaa seat yangu yote
Kwahiyo kama niliyekaa naye amekaa na sehemu yangu yaani namkalia Sehemu iliyozidi.

Hahaha
 
Nani mwenye experience na Yale mabus yenye seat za kukaa watu wawili kushoto na watatu kulia na amepata Seat ya katikati kwenye upande wa Seat tatu na iwe safari ya zaidi ya masaa nane...
 
Hahaah wanakuonyesha machimbo ya mjerumani
 
Nani mwenye experience na Yale mabus yenye seat za kukaa watu wawili kushoto na watatu kulia na amepata Seat ya katikati kwenye upande wa Seat tatu na iwe safari ya zaidi ya masaa nane...
Hapo bila shaka ni tabu sana.
 
Hapo anataka kuwaonyeshea wasafiri wengine kua na yeye ana family na wanainjoi
 
Napenda kuchimba dawa kichakani, aisee huwa namiss kweli hako ka moment….

Sipendi kukaa na abiria mchafu mchafu, aisee safari inakuwa ngumu hasa safari za masafa marefu…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…