Salam Wanajamvi, natumai wote mko poa kabisa!
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye mada. Mungu wetu Bwana wa Viumbe vyote ametuumba Jinsi mbili za ME na KE. Kuwa Me au Ke haina maana kuwa uko superior au less superior to the opposite sex, bali sote tunategemeana katika kuyaishi maisha haya mafupi katika Ulimwengu huu.
BINAFSI kuna TABIA moja inanikwaza sana kutoka kwa ndugu zetu hawa wa jinsi ya Me; ukikutana na mwanaume mathalan safari, kwenye majukumu ya kikazi au hafla za kijamii wengi watakuomba namba WHICH OFCOURSE IS NOT BAD lakini changamoto inakuja kwenye matumizi ya hiyo namba!!!
Asilimia kubwa ni kutongoza!!!! Jamani Kama ilivyo kwa wanaume wenzio mwanamke anaweza akawa mshirika katika biashara, kazi au madili mengine, sasa ukitanguliza NGONO utafunga MILANGO MINGINE ya kushirikiana kama wanajamii katika kuyaendesha maisha haya.
Baadhi ya wanaume huwa nashindwa kabisa kuwaelewa vichwa vyao vinawaza nini!!!!
Unakutana na mtu ana mahusiano au familia yake PLEASE HESHIMU PERSONAL LIFE YAKE NA KAMA HUNA CHOCHOTE UNAWEZA KUSHARE NAYE POSITIVE LET HER MOVE ON WITH HER STRUGGLE...
Usimrubuni mwanadada au binti wa watu ili ULETE UZI HAPA JF huku ukimwachia majonzi katika maisha yake!!!! Huna future na mtu au ana mahusiano yake msaidie kuyalinda na usiwe sababu ya kuvurugikiwa!!!!
Kuna wanaume wa kweli WACHACHE ambao anaweza kumsaidia MWANAMKE NA WALA ASIHITAJI NAMBA YA SIMU WALA SHUKRAN!!! Siyo wengine akipata nafasi ya kutoa huduma au msaada kwa mwanamke basi tayari ametengeneza NDOANA...
Wengi wa WANAUME HAPA WANALIA MAISHA MAGUMU HAYAELEWEKI, HONESTLY NADHANI PARTLY NI KWA SABABU YA MACHOZI MNAYOYASABABISHA KWA MABINTI ZA WATU!!!!
Jamani hii TABIA IMEKUWA SHIDA SANA KWENYE JAMII ZETU....
Majibu uliyopata humu yanakupa picha what is going on.
Wanaume wamepotea. Wengi hawamjui Mungu ndo maana wanafanya hayo wanayofanya.
Ukitaka kujua usiende mbali angalia nyimbo za hapa bongo wasanii wa kiume wakoje? Wapo kitofauti wanataka kufanana na wanawake wanasuka wanapaka makeup wanavaa hereni wanaimba kwa sauti za ajabu ajabu!!!
Men are in a crisis. Wanawake wamebadilika wanabeba majukumu ya kiume wanaume wanarudi nyuma.
Wanaume humu wengi wanajisifu kupiga miti na kumwaga manii zao huko na huko ndo urijali...bila kujua ni upumbavu mkubwa.
Mwanaume aliumbwa kiongozi ila amepotea ndo maana wanawake wanaongoza siku hizi na hata kufanya majukumu ya wanaume.
Mithali 31: 3 Usiwape wanawake nguvu zako;
Wala moyo wako usiwape wale wanaowaharibu wafalme.
Wanaume wengi wanapoteza nguvu za kiroho na kimwili kwa kuzini ovyo na wanawake. Ufalme wao unaharibika!!!!!!
Kama wewe ni mwanamke kamwe usitoe namba kwa mtu mliekutana nae kwenye basi au pilika pilika kama hajielewi. Ukimpa akileta uhuni mblock sahau. Isikuumize kichwa.
Sa nyingine wanawake pia wanapenda ngono ndo maana 'subconsciously' wanatoa namba na kukubali kulala na jingaume alilokutana nalo kwenye basi. Na akili zikirudi anaanza kulaumu!!!
TUISHI HUMU
Mithali 31: 30 ...uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Mithali 6:32 Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
Mhubiri 12:1
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.